[Mabadiliko] michango katika jukwaa

Wednesday, January 22, 2014
Waheshimiwa na waishiwa,
Baada ya kurudisha g mail, kwanza nawatakieni heri ya mwaka mpya kabla mwaka haujachakaa kama mimi. Tudumu humuhumu kwenye mabadiliko na na kuendeleza mabadiliko chanya kwa faida ya jamii na nchi yetu.

Aidha sina budi kukiri (hasa kwa wale walio wengi ambao wala hawakutambua kwamba mwenyekiti hajaonekana ha ha) kwamba nilichukua likizo kidogo ya Mabadiliko si kwa sababu ya U-BBC wangu (Born before Computers) maana nimeweza kuingia kwenye wavuti mpya, bali kwa kuwa nilitaka kukaa na kutafakari kidogo kuhusu mwelekeo wa Mabadiliko.

Naendelea kukiri kwamba niliamua kupumzika kwa sababu nilianza kujisikia vibaya kuhusu baadhi ya michango na mijadala.  Mimi binafsi, na nakiri pia kwamba yawezekana ni kutokana na mtazamo wangu finyu, sivutiwi hata kidogo na hukumu bila uchambuzi.  Kwa mfano, baada ya Zitto kusimamishwa na chama chake nikaona michango mingi mifupimifupi ya kumlaani, msaliti, haini, mla rushwa n.k wakati upande wa pili bado kuna maswali hayajajibiwa hadi leo.  Inawezekana kweli yuko hivyo mimi sijui na nilitegemea kwamba wafuasi wa chama ambacho mimi ningependa kishike madaraka watumie uchambuzi wa kina zaidi siyo kushtumu tu. 

Vivyo hivyo upande wa Lowassa.  Fisadi yule, atakiona mwaka 2015.  Lakini nikiangalia pamoja na ufisadi wake anajua siasa na wakati wanamabadiliko tunamdismiss anaendelea kujijenga, si tu kwa kutoa pesa bali kwa kuongelea mambo ya sera.  Siwezi kumsameha kwa jinsi alivyobomoa elimu ya sekondari kwa shule zake za ukata, na sikubaliani na siasa yake ya maamuzi magumu bila maamuzi sahihi lakini ukweli ni kwamba naamini tunamdismiss at our peril.  Tunapenda mabadiliko ndiyo lakini tumefanya nini kumneutralise Lowassa, au Kinana au wengine.  Haitoshi kumlaani.  Wapi mikakati ya kuwashughulikia.  Hasa upande wetu wanamabadiliko lazima iwe kwa hoja siyo laana tu.

Na vivyo hivyo kwa wengine pia.  Mimi namheshimu Winnie Mandela kupita kiasi lakini siko tayari kumdismiss Graca Machel ambaye naye amefanya mengi makubwa na mazuri.  Kuna haki gani kuona kwamba kazi yake ni kuwasaka marais tu.

Najua mambo mengine ni utani lakini lazima niseme kwamba hii twitter style ya kuwadismiss watu kwa mstari mmojamoja unanikera kupita kiasi.  Huenda ni udhaifu wangu au hata uBBC wangu.  Labda wakati wa mapambano inabidi kuwadismiss na kuwahukumu watu bila kuwashinda kwa hoja sijui, labda nakuwa too academic, lakini nilitegemea uchambuzi zaidi.   Niliachana na wanabidii kutokana na udikteta wa mwenye jukwa na siwezi kurudi pale k(kama vile political correctness) wa sababu hiyohiyo lakini naona kuna kama aina ya mabadiliko correctness ambayo ni kuwadismiss wasiokubaliana na sisi.  Siafiki hii hata kidogo.

Nakaribisha maoni yenu.  Inawezekana na makengeza yangu yananisumbua.  Lakini katika maazimio yangu ya mwaka 2014 baada ya kutafakari kwa muda, nimeamua nisiogope kutwitterika na mimi kwa sababu sikubaliani nao. 

Tuwe na mwaka wa mabadiliko ya kweli yanayojengwa juu ya misingi imara, na vitendo lukuki.
Mabala

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments