
Nami nitapata fursa ya kutoa hotuba. Nitazungumzia umuhimu wa kuhifadhi historia kwenye maandishi ili iwe ni kumbukumbu ya miaka mingi kwa wengine kujifunza. Maana, historia haibadiliki, lakini inapotea.
Na taifa linalodai kuwa watu wake wameelimika tunalipimaje?
Jibu; Ni kwa kuangalia idadi ya machapisho yanayozalishwa kila mwaka. Kuangalia pia ubora wa machapisho hayo.
Na machapisho ni jambo moja, na kuyasoma machapisho hayo ni jambo jingine kabisa.
Tuna lazima ya kuwajengea watu wetu kiu ya kupenda kusoma. Ni moja ya malengo yangu ya kuandika kitabu cha ' Simulizi Za Mzee Madiba'. Kwamba watu watafute vitabu zaidi vya kusoma.
Kesho pale Makumbusho ya Taifa nitasimulia utoto wangu na jinsi nilivyoanza kuelewa maana ya vita vya ukombozi kutoka Ubaguzi wa rangi Afrika Kusini kutokana na kucheza mpira na watoto wa wakimbizi wanachama wa ANC waliokuwa wakikaa jirani na sisi pale Biafra Kinondoni.
Kesho kutakutakuwa na nafasi pia ya kuulizana maswali, kujadiliana na kupeana ufafanuzi, kama Watanzania.
Usiku Mwema.
Maggid.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments