[wanabidii] MAMBO 5 YA KUZINGATIA JUU YA MATUMIZI YA MITANDAO YA JAMII

Wednesday, November 13, 2013

Siku hizi, katika kila watu kumi wanaotumia mtandao, basi angalau watano kati ya hao wanatumia mitandao jamii. Kuna baadhi ya watu wamegeuza mitandao hii kuwa kama ni sehemu ya mawasiliano, ama ya mtu kwa mtu au ya kibiashara. Siku hizi, si kitu cha kushangaza kusikia mtu maarufu au kiongozi fulani atakuwa kwenye Facebook saa fulani kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi / mashabiki wake. Mitandao hii ni kama vile Facebook, Twitter, Jamiiforums nk, hivyo basi, hatuwezi kuepuka ushawishi wa mitandao jamii katika jamii yetu.

Matumizi bora ya mitandao jamii huweza kuleta faida nzuri sana, ila huwa kinyume pale inapotumika sivyo, ama kwa kutokujua ama kwa kuamua. Hivyo leo hii tuangalie mambo kadhaa ya kuepuka unapotumia mitandao jamii.

1. EPUKA KUJIACHA WAZI KWENYE MITANDAO JAMII.

 

Kuna baadhi ya watu wamegeuza mitandao jamii ni dunia yao nyingine kabisa, wao kila kitu wanachokifanya utakiona kwenye mitandao jamii, kala nini, anadate na nani, kavaa nguo gani nk. Mitandao jamii ni uigaji (Simulation) ya maisha ya halisi.Tukiwa kwenye maisha halisi, sio watu wote wanaoweza kujua maisha yako kwa undani,kwani kuna vikomo, kuanzia wale mulio nyumba moja, munaofanya kazi pamoja nk.

Ingawa kwenye mitandao jamii wengi wanaweza kuchunga kwa kutumia michungo ya ufaragha (Privacy setting) lakini si wote wanaojua hilo, pia tumeona mamia ya akaunti za watu zikivamiwa na wavamizi wa mtandao (Hackers) na kuweka hadharani taarifa zao nyingi. Hivyo epuka kuweza kila kitu kwenye mitandao jamii, kula na kikomo na pia anza kuchunga marafiki zako juu ya nani anaweza kuona nini. Unaweza kuangalia Video HAPA jinsi ya kuchunga ufaragha kwenye Facebook.

2. JICHUNGE KWENYE UTUMAJI.

Je ushawahi kusikia mtaani wanasema jamaa ana gubu (anaongea sana?), kwenye mitandao jamii pia kuna watu wana gubu, wanachonga sanasana. Hawa ni wale watu ambao kila dakika wametuma kitu kipya, hii sio tu hufanya kupoteza mvuto kwa wanaokufuatilia, bali pia umuhimu wa makala zako hupungua. Binafsi huondoa watu aina hii kwenye mlisho wa maboresho (activities feeds) bila hata kujiuliza.

Hivyo, ili kuepuka kutengwa au kuonekana unachonga sana, chunga idadi ya maboresho unayotuma kwa siku.

3.EPUKA KUTUMA MAKALA ZA NGONO, DINI AU SIASA KAMA WEWE SI MUHUSIKA.

Hivi ni vitu ambavyo huathiri watu wengi sana, chukulia mfano wewe ni rafiki wa bwana X, unafungua Facebook au Twitter yako unakutana na picha ya ngono imejaa kwenye mlisho wa maboresho toka kwa rafiki yako. Ukweli ni kuwa utajisikia vibaya mno ama kama na wewe ni wa aina hiyo. Hii pia ni sawa na kwa mambo ya dini na siasa.

Nchi yetu ikiwa ni nchi isiyo na dini, ila watu wake wamechanganyika mnomno, kwenye kila marafiki zako wawili, kuna mmoja ni wa dini nyingine, hivyo epuka kutuma makala za dini zinazoudhi, zenye kebehi au kuudhi wengine. Jaribu kuwa mtu ambaye utaweza kuishi na watu wote. Mfano huu pia tuuchukue kule uraiani, kuna baadhi ya watu hukimbiwa, hivyo chukua tahadhari kabla ya kukimbiwa.

4. USIHAMISHIE HASIRA ZAKO KWENYE MITANDAO JAMII.

Kuna baadhi ya watu, wakishauziwa nyumbani, hasira zinaishia kwnye mitandao jamii,amini usiamini, mitandao jamii haiwezi kukusaidia kutuliza hasira zako zaidi ya kukupotezea muda na kujidhalilisha. Ni sawa na yule mtu mwenye ugomvi na mke / mume wake halafu anapita kila nyumba kutangazia mapungufu ya mwenza wake, jamii nzima inajua, siku mutakaporudiana, watu wote washajua mapungufu ya mwenza wako, je utafuta toka kwenye vichwa vyao? Kwenye mitandao jamii vilevile, kuna baadhi ya watu kuhifadhi kila unachotuma na siku ya siku watatumia kuja kukashambulia. Kaa mbali na mitandao jamii kama unaona hauwezi kuchunga mhemuko (emotion) wako.

5.Siyo kila mtu lazima awe rafiki yako.

Chukulia mfano mitaani tunamoishi, kuna watu wa aina mbalimbali, na siyo kila mtu ni rafiki yako, kuna baadhi ya watu hata hautaki kuwasogelea kutokana na tabia zao, hii ni sawa kwenye mitandao jamii. Epuka kukubali maombi ya urafiki toka kwa kila mtu, haswaa ambao hauwafahamu. Marafiki sio tu huweza kutumika kujenga taswiura yako, bali kuna baadhi ya marafiki si marafiki, hivyo chunga marafiki zako la sivyo ipo siku utakuja kujuta.

Hayo ni mambo muhimu kwa ajili ya afya ya utumiaji wa mitandao jamii, usisahau kulike Kurasa yetu ya Facebook kwa makala mbalimbali za IT kila wiki https://www.facebook.com/dudumizi

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments