SEHEMU YA KWANZA.
Sote tunajua jinsi Mwl Nyerere alivyopinga mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 kwa kusema tunataka kujenga nchi yenye umoja na Mshikamano wa Taifa na baadaye akatofautiana na wenzie akina Kambona,kutoka mwaka 1965 mpaka 1992 ndipo ulikuwa ukomo wa mfumo wa chama kimoja.,Kipindi hicho chote mpiga kura alikuwa anakwenda kwenye Sanduku la Kura kwa kutia tiki kura ya ndiyo au hapana kwenye picha ya mgombea ,mgombea anakuwa mmoja,kama humtaki ,acha.Hivyo ilibana chaguo huru kwa wapiga kura.
Wanaharakati na wadau mbalimbali walipambana na mfumo huu kandamizi kwa muda mrefu na hatimaye tukafanikiwa mwaka 1992,ambapo sasa ukawa ni uhuru wa wananchi kuchagua mgombea wanayemtaka.Lakini mfumo huu haukubadirisha mfumo wa taasisi za Vyama vya Siasa ila ulifanikiwa kuleta vyama vingi vya Siasa ambavyo kila chama kitasimamisha mgombea wake,hivyo kama vyama vipo kumi(10)basi wagombea watakuwa 10.
Wanasiasa ni watu wa ajabu sana,wale wale waliodai kwamba mfumo wa chama kimoja uliwabana,haukuwapa wigo mpana wananchi demokrasia ya Kuchagua,ndio wakawa wanateua jina moja na kulipeleka katika Mkutano mkuu kwa Kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Ndani ya chama hawaruhusu demokrasia ya wagombea kushindana kuomba kura ya kuchaguliwa,ila nje ya chama wanaomba demokrasia ya kushindana kuchaguliwa.,Vyama vya upinzani ambavyo vilitakiwa kuwa vyakwanza kuasisi demokrasia halisi vimeonekana vikiikwepa demokrasia vilivyoidai.
UCHAGUZI WA 2008 ULIO MWINGIZA MBOWE MADARAKANI KWA AWAMU YA PILI.
Kutokana na Chama kukua,tulifurahia kwamba sasa hatutakwenda nyumbani kwa mtu kumuomba atuongoze,bali tutatangaza nafasi za kuomba uongozi wa kuchaguliwa,watu watachukua fomu,Vikao vya kisheria vitatangaza mfumo mzima wa mwenendo wa uchaguzi,sifa za wagombea,muda wa kampeni na maadili ya kampeni.Hii tuliifurahia sana kwasababu tulitaka tuwaoneshe CCM jinsi uchaguzi unavyoweza kuwa huru na wa Haki.Tulitaka kuionesha Tume ya Uchaguzi Taifa ni jinsi gani unaweza kuendesha Chaguzi kwa uwazi,uhuru na bado ukawa na taasisi Imara.
Tulitaka tutume ujumbe katika Jamii ya kimataifa kwamba CHADEMA ikichukua dora,itaheshimu misingi ya demokrasia,ikiwemo namna tutakavyoendesha chaguzi zetu za nchi,tumpata mwenyekiti wa kitongoji,kijiji,Diwani,Mbunge na Rais kwa mfumo ulio wazi,huru na unaowajibika.Mana tulitaka Kutenda kwa Vitendo tunayoyahubiri na Kuyasimamia.
Tulishangaa ghafula baadala ya kumpongeza aliejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa ili ashindane na Freeman Mbowe ambaye alikuwa anatafuta kipindi cha pili,ikabaki kuwa taharuki ya hofu na wasiwasi juu ya Ujasiri wa Kijana mdogo Zitto Kabwe kugombea nafasi kubwa katika chama namna hiyo na kushindana na Mbowe.
Taharuki hiyo ikaleta maneno machafu Kwa Zitto Kabwe kwa kuonekana hamuheshimu Mbowe,kwanini anaitaka nafasi hiyo wakati Freeman bado hajamalizia kipindi cha pili,Kwanini Zitto asimsubiri Mbowe amalizie Kipindi chake cha Pili.,Wengine wakasema muda huu ni muda wa kujiandaa kuelekea uchaguzi Mkuu 2010,ambapo Kama Chama tunahitaji kwenda kwenye uchaguzi tukiwa hatujagawanyika.
Wazee wa Chama,wakaitwa na Kuwaita Freeman Mbowe na Zitto Kabwe wakiita ni kikao cha Usuruhishi!!!eti Kugombea nafasi ya Uenyekiti ni Mgogoro hivyo ulitakiwa Usuruhishwe na Wazee.
Wakamuomba Zitto Kabwe akubali kumwachia Freeman kipindi cha pili,yeye akiombwa asubiri Freeman akimaliza kipindi chake cha pili.,Basi kutokana na mvutano huo ikabidi Zitto Kabwe akubali kuachia nafasi hiyo ili Wapiga Kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano mkuu wakachague Mtu na Kivuli(kura ya ndiyo au Hapana).
Uchaguzi ule ntaukumbuka jinsi ulivyoichafua demokrasia halisi,ningekuwa Freeman Mbowe nisingekubali kushindanishwa na Kivuli,kwani ni heshima kushindanishwa na binadamu mwenzangu kuliko kushindanishwa na Kivuli.
Wanachama tulikubali yaishe,ili tujenge umoja wa uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwan 2010,na Serikali za Mitaa 2009.
SEHEMU YA TATU KAMBI RASIMI YA UPINZANI BUNGENI.
Uchaguzi wa 2009 na 2010 ukawa umekwisha,tayari Freeman Mbowe alikuwa ameshinda uchaguzi jimbo la Hai akiwa Mbunge na Zitto Kabwe alikuwa ameshinda ubunge Kigoma Kaskazini.
Wakati huu,demokrasia ikawa Iinatakiwa kuwakutanisha Wabunge wote wa chadema,ambapo watatakiwa kushindania nafasi ya Ukiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni.
Wanasiasa wawili hawa Zitto Kabwe na Freeman wakaonesha nia ya kuomba kinyang'anyiro hicho cha nafasi ya juu huko bungeni.
Mbinu za kukwepa ushindani ikajirudia tena,Kwa Mwenyekiti wa Chama kusema kwamba bunge letu linafuata mfumo wa jumuiya ya madora,ambapo Kiongozi wa chama anapokuwepo bungeni basi moja kwa moja anakuwa kiongozi bungeni.
Hivyo kwasababu mwenyekiti wa Chama Taifa yupo bungeni basi automatically ndiye atakuwa kiongozi wa Kambi rasimi ya upinzani Bungeni na Naibu Katibu Mkuu utakuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungen.
Vyama vya Upinzani lazima tusitafsiri vibaya misingi ya demokrasia,demokrasia isiwe demokrasia unapotafuta maslahi fulan,halafu ikawa siyo demokrasia unapokuwa una maslahi tayari.
SEHEMU YA NNE.KUELEKEA UCHAGUZI MKUU CHADEMA
Sababu zile zile zilizotumiwa kukwepa wanachama kushindania nafasi za uongozi wa juu wa chama mwaka2008,zinaelekea kuwa sababu hizo hizo zinazotaka kutumiwa kukwepa wanachama kushindania nafasi za juu za uongozi katika chama,kwani sababu zile zilikuwa umamluki wa CCM,Kujenga umoja na Mshikamano wakati huu wa kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu.
Wanachama tunatambua thamani ya jukwaa la ushindani,kwamba wanachama wanaomba nafasi wanazoziona wanatosha kuziongoza,Wanachama watachujwa na wapiga kura ambao ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa,Watajieleza ni nini Wanataka Kukifanyia chama?,Wamekifanyia nini na maswali mengine Mengi.,Wanachama watawajua nani aliye na hoja za Msingi na Maono ya Kukiongoza Chama.
Haki kubwa kuliko zote zaUanachama wa Mwanachama ni KUWA NA HAKI YA KUFIKIRI,KUAMUA NA KUCHAGUA CHAGUO ALITAKALO PASIPO KUSHINIKIZWA NA MTU.
ANGALIZO MARA BAADA YA UCHAGUZI KATIKA UUNDAJI WA KURUGENZI
Wananchi wanataka Mabadiriko,Hawajaona utayari wa CCM kuwaletea Mabadiriko.,Wanaitegemea CHADEMA ,NCCR na CUF kuwaletea Mabadiriko.
Kwa chadema,Katiba inasema Wakurugenzi wote na Maafisa wa Chama Wataomba nafasi hizo kwa Katibu Mkuu Taifa,baada ya Katibu Mkuu kuteuliwa na Kuidhinishwa na Kamat Kuu,Baraza kuu na Mkutano Mkuu.
Katiba atayawasilisha Majina ya wanao omba nafasi hizo za Ukurugenzi na Uafisa,Kamati kuu itawajadili na Kuamua kwa kura.
Hivyo baada ya Kamati kuu kuamua,ndipo Katibu Mkuu atawaajiri.
WAKURUGENZI WOTE NA MAAFISA WALIOPO,HAKUNA HATA MMOJA ALIYEPITIA MCHAKATO HUO WA KUOMBA NA KUJADILIWA NA KAMATI KUU.
Uenyekiti wa Chama,Ukatibu Mkuu ,Ujumbe wa Kamati Kuu,Baraza Kuu na pengine Mkutano Mkuu ni Katiba na siyo vinginevyo.
Viongozi wetu wa Chadema lazima Muiheshimu Katiba hata kama ni Mbovu,Msipo iheshimu Katiba basi Hamuwezi Kuwaheshimu Wanachama wenu,chama Chenu,Katiba ya nchi na wananchi wenu.
Hatuwezi Kutwaa uongozi wa nchi nje ya Katiba ya Chama na ile ya Nchi,kinyume chake ni uasi.,mkifanya hivyo pia mtaondolewa kwa uasi.
USHAURI KWA CHADEMA.
Kwasasa kuna wimbi kubwa la wanachama na Viongozi wao kupenda kutumia informal communication(Mawasiliano yaliyo nje ya Katiba) hiki ni kiashiria cha kukosekana kwa uhuru wa kutoa maoni ndani ya chama,kama Uhuru upo basi ujue viongozi wetu na wanachama wetu wanaogopa Vitisho,Wanaogopa kuitwa majina mabaya wanayobambikiwa na viongozi wasio penda kusikia ushauri wa kiongozi mwenzie au mwanachama.
Madhara yake ni wimbi kubwa kutoa ushauri kupitia Jamii fourum hivyo Chama kushindwa kupata raslimali adhimu ya mawazo na Mbaya zaidi siri za chama kuwa hadharan.
Ni Mawazo kutoka Kwa Mwanachama na Kiongozi.
Asante.
UHURU WA KWELI,MABADIRIKO YA KWELI.
-- Sote tunajua jinsi Mwl Nyerere alivyopinga mfumo wa vyama vingi mwaka 1965 kwa kusema tunataka kujenga nchi yenye umoja na Mshikamano wa Taifa na baadaye akatofautiana na wenzie akina Kambona,kutoka mwaka 1965 mpaka 1992 ndipo ulikuwa ukomo wa mfumo wa chama kimoja.,Kipindi hicho chote mpiga kura alikuwa anakwenda kwenye Sanduku la Kura kwa kutia tiki kura ya ndiyo au hapana kwenye picha ya mgombea ,mgombea anakuwa mmoja,kama humtaki ,acha.Hivyo ilibana chaguo huru kwa wapiga kura.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments