[Mabadiliko] Kwanini Tanzania ni masikini: Enzi za ukoloni, miaka hamsini baada ya uhuru na miaka kadhaa ijayo

Wednesday, November 13, 2013
Kuna watu nimewakuta wakijadili "kwanini Tanzania ni masikini na nchi za Ulaya kama Ujerumani na Uingereza ni matajiri?"
 
Nilivutiwa na mjadala wao, nikaketi kuwasikiliza. Mmoja wao alimjibu mwenzake "hizo nchi mbili ulizotaja walitutawala kwahiyo walichukua mali zetu nyingi wakafanyia maendeleo kwao"
 
Mwingine akachangia "mbona sasa ni miaka 50 baada ya uhuru lakini bado malighafi zinapelekwa huko huko nchi za nje na sisi tungali masikini vile vile kama zamani? Tatizo liko wapi? Kwanini tusiongeze thamani ya bidhaa hizo hapa hapa kwetu kasha tuwauzie huko nje zao la mwisho kama vile mikufu, pete za dhahabu?"
 
Wote walikaa kimya kwa muda!
 
Mwingine akachangia "hatuna viwanda! Hatuna viwanda hata vya kuchakata mazao kuyaongezea muda wa kuhifadhika. Mazao yaliyomengi yanalazimika kuuzwa baada ya mavuno kwa bei ya chini yaani bei ya kutupa"
 
Mwingine akachangia, kwanini hao wanaoitwa wawekezaji wanakuja kuwekeza kwenye miundombinu ambazo zilikuwepo tangu zamani kama vile kiwanda cha saruji wazo, mitambo ya umeme, migodi n.k?
 
Kwanini wawekezaji hawawekezi hapa Tanzania kwenye nyanja zingine kama vile viwanda vya kutengeneza; magari, pikipiki, simu, laptop?!
 
Kwanini wawekezaji hawawekezi kwenye viwanda vya nguo tunaishia kununua mitumba na mafundi wa mtaani wanabaki ku-repair viraka tu?
 
Kwanini wawekezaji hawawekezi kwenye viwanda vya kushona viatu ili hali pale kariakoo kuna vijana wanakopi na kupesti mitindo ya viatu vya nje?
 
Mwingine aliuliza kwanini baadhi ya watajiri waKitanzania wapo teyari kujenga nyumba za mamilioni (au kununua magari ya kifahari) ilihali anaweza kutumia hela hiyo kuanzisha mradi utakao mnufaisha yeye na mamia ya waTanzania?
 
Nilisikitika kumsikia mmoja wao akisema "aaah ilimradi mkono unaenda kinywani na watoto wanaenda haja basi hakuna shida; ndiyo maisha".

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
KARIBU MABADILIKO MPYA: Jukwaa hii sasa linapatikana katika mwuonekano wa Kisasa: www.mabadiliko.com tafadhari tembelea na jisajili huko
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments