[Mabadiliko] Kesho Nitahutubia Kwa Mara Ya Kwanza Kijijini Kwetu Nyeregete...!

Saturday, November 30, 2013
Ndugu zangu,

Matukio mengine ni ya muhimu katika maisha ya mwanadamu. Kesho Jumamosi nitahutubia kwa mara ya kwanza kijijini kwetu Nyeregete. Ni kijiji alichozaliwa baba yangu. Naisubiri kwa hamu siku ya kesho.

Ni kijiji nilichocheza utotoni kila nilipopata likizo ya shule. Na kesho nitasikilizwa na ndugu na jamaa wa kijijini kwetu.

Ni kwenye tukio la harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kikundi cha wanawake kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi kwa shughuli za kilimo.

Nitaongea kuhusu elimu na maendeleo. Watu wengi wakiwemo wazee wa kijiji wamealikwa. Na pengine hakuna hotuba ngumu kama ya kuhutubia kijijini kwenu. Si wamesema, nabii hakubaliki kwao.

Natumaini hakuna atakayenirushia yai viza!

Usiku Mwema.

Maggid.
Iringa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments