[wanabidii] TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA BAGAMOYO KWA KUKATIWA UMEME

Friday, October 11, 2013
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linaomba radhi wateja wake wa Bagamoyo kwa katizo la umeme lililotokea kuanzia siku ya Jumapili Oktoba 6, 2013 saa 7:30 mchana hadi Jumatano Oktoba 9, 2013 saa 5:25 usiku kutokana na kuharibika kwa transfoma kubwa la MVA 2.5 ya msongo wa kilovoti 33/11 iliyopo Mwanamakuka.

Transfoma mbovu imeondolewa na kuwekwa nyingine ya MVA 7.5 na umeme sasa unapatika wa kutosha.
Shirika linasikitika sana kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika kipindi chote cha tatizo hili.

Imetolewa na:     
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments