[wanabidii] Taarifa ya Serikali ya kuzuia tovuti ya gazeti la Mwananchi kuchapisha habari

Tuesday, October 01, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kama mnavyofahamu, Serikali  imeyafungia  magazeti ya Mtanzania na Mwananchi kwa kuzingatia  Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 1977. Gazeti la Mwananchi limefungiwa kwa muda wiki mbili kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013 na Gazeti la Mtanzania limefungiwa kwa muda wa miezi mitatu au siku 90 kuanzia tarehe 27 Septemba, 2013.

Aidha tunataka umma ufahamu kuwa Serikali  haikukurupuka  kufungia magazeti hayo. Uamuzi huo ulifanyika baada ya
kufuata taratibu zote za msingi ikiwemo kuwasikiliza wahusika.

Hata hivyo, tumeona gazeti la Mwananchi baada ya kufungiwa limeendelea kuchapishwa kwenye mtandao wa Internet kinyume cha amri  iliyotolewa. Kufanya hivyo ni kosa na  Serikali  tumewaandikia kuacha mara moja la sivyo, Serikali italazimika kuchukua hatua kali zaidi.

Aidha kampuni ya New Habari 2006 baada ya kufungiwa moja ya magazeti yake, imeanza  kuchapisha gazeti la 'Rai' kila siku tangu tarehe 29 Septemba mwaka 2013 bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Hilo nalo ni kosa,  Serikali  inawataka kuacha mara moja kuchapisha gazeti hilo kila siku na warudie ratiba yao ya kuchapisha mara moja kwa wiki mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI –MAELEZO
TAREHE   1/10/2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments