[wanabidii] NAKIONA KIFO CHA WANABIDII, BURIANI WANABIDII

Saturday, October 12, 2013
Wakuu

Jukwaa la wanabidii liko taabani, halina mvuto tena, mijadala yenye
tafakuri tunduizi haionekani tena, wachangiaji mahiri walio kuwa wana
mwaga nyanga hawaonekani tena! kwa sasa ni nadra sana kuona mjadala
mmoja wa wanabidii unafika angalau michango 25! Hiki ni kifo
ukilinganisha na jinsi jukwaa lilivyokuwa awali.

Kuna watu walisha tahadharisha kipindi kile cha ubabe na fukuza
fukuza, kuwa ubabe na matumizi ya nguvu kwa kuzuia fikra huru hazita
lijenga jukwaa bali ndio itakuwa chanzo cha kifo kwa jukwaa hili.
Naona kila dalili za kutimia kwa maono na kauli za watu wale walio
onya.

Wanabidii ya sasa imekuwa baridi na hakika inaelekea chumba cha
kuhifadhia miili iliyogota kusuguma damu. Wako wapi wanabidii? yuko
wapi mwanabidii aliye kuwa mwanabidii kuliko wanabidii wengine?
wahenga walisha sema "Asiye sikia la mguu daima huvunjika guu"

Buriani wanabidii. Amka kama una weza, nakulilia nione cheche zako
kama zamani, Mbona sikuoni? Unataka kulala kwa buriani bila hata
kuwaaga wanabidii wenye bidiii? utayaweza MABADILIKO ya kukikimbia
kifo? Kule Mabadiliko ndio kumekuwa kwenye Mabadiliko maana wengi
walio kuwa wanamwaga tafakuri tunduizi kupitia wanabidii sasa wote
wamejikita MABADILIKO.

kubali kufia wanabidii na maono butu au kimbilia Mabadiliko kwenye
Tafakuri tunduizi kutoka kwenye vichwa vyenye kariba kubwa kwenye nchi
hii.

Usiseme umeambiwa! soma alama za nyakati.
--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
Mobile: +255 (0) 713 24 67 64
Alternative: +255 (0) 784 24 67 64
Skype: Mohamedi.Mtoi
Twitter: @mohamedimtoi
Facebook: http://www.facebook.com/mouddymtoi
--

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments