[wanabidii] Watanzania na Mtangamano wa Afrika Mashariki

Friday, September 20, 2013
Wapendwa Wanabidii,

Naomba mnisaidie kupata ufafanuzi juu ya mambo kadhaa kuhusu mtangamano wa Afrika Mashariki kama ifuatavyo?

  1. Hivi kuna tofauti gani kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Shirikisho la Afrika Mashariki?
  2. Katika mchakato wa mtangamano wa Afrika Mashariki (East African Integration) Watanzania katika makundi mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa wamenufaikaje na mtangamano huo?
  3. Kuna haja ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashairiki kuingia kwenye ushirikiano wa kisiasa na kifedha? Mnadhani kunaweza kuwa na manufaa gani mahsusi kwa Watanzania?
  4. Kuna mambo yoyote ambayo yatatia hofu kwa Tanzania na Watanzania kuingia kwenda mbali zaidi kwenye huu ushirikiano?
Asanteni sana?

Sitta Peter

Share this :

Related Posts

0 Comments