[wanabidii] TAMASHA LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI WA MTANZANIA BAGAMOYO KUANZIA TAREHE 23 – 28 SEPTEMBA 2013

Saturday, September 07, 2013

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa)

TAMASHA LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI WA MTANZANIA BAGAMOYO KUANZIA TAREHE 23 – 28 SEPTEMBA 2013

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo imekuwa na utaratibu wa kuandaa Tamasha la Sanaa na Utamaduni kila mwaka. TaSUBa ikishirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wanakuletea Tamasha la 32 la Sanaa na Utamaduni na litaadhimishwa kuanzia tarehe 23 – 28 Septemba hapa Bagamoyo. Tamasha 
litafunguliwa tarehe 23 Septemba kuanzia saa 3:00 asubuhi na kufungwa tarehe 28 Septemba.

Kati ya shughuli zitakazofanyika ni pamoja na maonesho ya sanaa za jukwaani (Muziki, Ngoma, Maigizo, Vichekesho, Sarakasi n.k), maonesho ya sanaa za ufundi, warsha, semina na mafunzo mbalimbali kwa siku zote za tamasha pamoja na kongamano litakalojadili kaulimbiu Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii .

Tamasha hili la kimataifa la sanaa na utamaduni wa Mtanzania ambalo linategemea kukusanya wasanii, wadau na watazamaji wapatao 3,500 kwa siku kutoka sehemu mbalimbali za ndani ya nchi pamoja na nchi za nje.

Hivyo tunawakaribisha wasanii, vikundi vya sanaa, ofisi za balozi, wadau katika sekta ya Sanaa, Utamaduni na Utalii, wananchi wote kwa ujumla, taasisi na mashirika mbalimbali kuhudhuria na kushiriki katika Tamasha hili.

KARIBUNI SANA.

Kwa mawasiliano zaidi;
Mtendaji Mkuu,
TaSUBa,
S.L.P 32
BAGAMOYO

Email: taasisisanaa@yahoo.com
Au piga Simu;

0715472745
0655850405
0754310425
0712683408

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments