TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA
LT. COL. (MST) ISSA SALEHE MACHIBYA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KONGAMANO LA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA MJINI KIGOMA
Utangulizi:
Ukanda wa Ziwa Tanganyika uko Magharibi mwa Tanzania unajumuisha Mikoa ya Katavi, Kigoma na Rukwa. Ukanda huu umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu duni ya huduma za kiuchumi na kijamii. Aidha, kwa muda mrefu miundombinu hiyo duni imechangia Ukanda huu kuwa nyuma katika nyanja mbalimbali na hivyo kuwa eneo lenye mazingira magumu ya kuwekeza na hata kufanyia kazi.
Kero hii ya miundombinu duni inaelekea kwisha baada ya Serikali ya awamu ya nne kuchukua hatua za makusudi kuziondoa ambapo kwa sasa dalili njema na za kutia matumaini zinaonekana bayana na kwamba

Ukanda huu unaanza kufunguka kwa kasi. Hali hii inatokana na jitihada za Serikali ambazo imezifanya katika ujenzi wa barabara za lami, Viwanja vya ndege, Bandari katika Ziwa Tanganyika, Uimarishaji wa upatikanaji wa umeme wa uhakika, pamoja na kuboresha huduma za kijamii kwa ujenzi wa Hospitali, Mashule, Vituo vya Afya na Zahanati.
Fursa:
Kutokana na hali ya kijiografia ya nchi yetu na hasusan Ukanda wa Ziwa Tanganyika, ni wazi hiyo ni kete muhimu ya kuitumia katika kukuza uchumi wa Taifa. Ukanda huo una fursa kubwa ya kukuza uchumi kwa kufanya biashara na nchi za Maziwa Makuu za Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda na sasa kuna dalili njema za wafanyabiashara wa Uganda na Sudan ya Kusini ambao wameanza kufanya biashara na Ukanda huu, hali hiyo inaufanya Ukanda wa Ziwa Tanganyika kuwa ni lango kuu la kuingia na kutoka kwa nchi za Maziwa Makuu.
Ukanda huu umesheheni rasilimali nyingi na vivutio mbalimbali vinavyohitaji kutangazwa na kuwekewa mazingira mazuri ya kuvutia Wawekezaji. Ardhi yake ni nzuri yenye mvua za uhakika ambapo mazao mengi yanastawi kama vile Michikichi, Miwa, Mpunga. Mahindi, Ngano, Mhogo, Alizeti, Kahawa, Ndizi, Ufuta, Karanga n.k., Mbuga za Wanyama za Gombe na Mahale ambazo ni maarufu kwa Sokwe, Mbuga ya pili kwa ukubwa nchini ya Katavi iliyosheheni wanyama wa kila aina. Ziwa Tanganyika maarufu kwa maji yake safi, samaki wazuri na njia ya kusafiria kwenda Zambia, D. R. Congo na Burundi kupitia Bandari za Kigoma na Kassanga, MV Liemba ambayo ni Meli kongwe kuliko zote duniani, makumbusho ya Dr. Livingstone, njia ya watumwa, majengo ya kale ya Mjerumani, maporomoko ya Kalambo na madini mbalimbali kama vile Shaba, Makaa ya Mawe, Dhahabu, Chokaa, Galena, Cobalt n.k. na Eneo Maalum la Uwekezaji Kigoma (Kigoma Special Economic Zone "KiSEZ")
Kongamano:
Viongozi wa Ukanda huo walipata wazo la kuandaa Kongamano kutokana na kushabihiana kwa mambo mengi kwa Mikoa hiyo; kijiografia, utamaduni, kuwa nyuma kiuchumi na kuwepo kwa utekelezaji wa Mipango ya Serikali ya kufungua Ukanda huo kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara za kiwango vya lami kuiunganisha na mikoa mingine na kupata umeme wa uhakika. Aidha, ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2025 ambayo inahimiza kupanga kwa kufuata vipaumbele na kutekeleza mipango ya maendeleo ili kukuza uchumi wa mtu mmojammoja hadi taifa.
Wazo hilo lilifanyiwa kazi na kuzaa matunda mnamo tarehe 17 Oktoba, 2011 wakati Kongamano la kwanza la Uwekezaji lilipofanyika mjini Mpanda. Tarehe 24 Novemba, 2012 Ukanda wa Ziwa Tanganyika ulifanya tathmini ya Kongamano la kwanza na kuona kuwa lilileta mafanikio kadhaa ikiwemo kupatikana kwa wawekezaji katika Madini, Kilimo, Ufugaji, na Viwanda vya kuchakata mazao. Hivyo kwa mantiki hiyo imeonekana kuwa kuna haja ya kufanya Kongamano jingine ambalo litatoa mwanga kwa fursa ambazo zimeongezeka kwa ajili ya uwekezaji.
Kwa kuona umuhimu huo Viongozi wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika wameandaa Kongamano la Pili la Uwekezaji ambalo linatarajiwa kufanyika katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji mwezi Oktoba, 2013 na litajumuisha wadau mbalimbali nchini, mabalozi wa nchi za nje, Wafanyabiashara wa nchi jirani, Taasisi mbalimbali na wafanyabiashara wa nchi za nje. Kongamano hili Ukanda utashirikiana na Chama cha Wafanyabiashara Nchini (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) na Mamlaka ya Eneo Huru la Uwekezaji (EPZA). Aidha Kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Hitimisho:
Kwa niaba ya viongozi wenzangu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika Mikoa ya Katavi na Rukwa; nawaalika Wadau wote wanaotaka kuwekeza katika eneo hilo washiriki Kongamano ambapo watajionea fursa mbali mbali zitakazoelezwa na kuoneshwa siku hiyo. Nawahakikishia kuwa hali ya usafiri kwenda Kigoma na Kurudi ni nzuri, huduma za Hoteli ni za kisasa, usalama ni wa hali ya juu. Hivyo ni matarajio yangu kuwa wadau wote wenye nia ya kuwekeza watatumia mwanya huu kikamilifu.
NAWAKARIBISHENI WOTE KATIKA MJI WA KIJANI WA KIGOMA/UJIJI.
ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments