05/09/2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Asalaam Aleikhum,
MECHI YA SIMBA NA KMKM
KESHO Ijumaa, Septemba 6 mwaka 2013, klabu ya Simba itacheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Zanzibar, KMKM, katika mechi itakayochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Lengo kuu la mechi hiyo ni mazoezi kwa Simba ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu.
Kikosi kamili cha KMKM kimewasili jijini Dar es Salaam tayari na leo saa tano na nusu kamili nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City Lounge katikati ya jiji.
Simba inaendelea na mazoezi yake jijini na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 11 jioni ili kuwezesha watu wengi kwenda uwanjani kutazama mechi hiyo ikizingatiwa kuwa Ijumaa ni siku ya kazi.
KATIBA MPYA YA SIMBA
KUFUATIA tangazo la Mwenyekiti wa Simba, Mhe Ismail Aden Rage, kuhusu Mkutano wa Katiba uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu, klabu imeanzisha rasmi mchakato wa kuwa na Katiba Mpya itakayokwenda na wakati.
Kutokana na umuhimu wa mawazo ya Wana Simba ndani na nje ya nchi kufahamika kupitia mchakato huu, klabu imeanzisha email maalumu iitwayo maoniyakatibayasimba@gmail.com ambapo wana Simba na wapenzi wa soka kwa ujumla wanatarajiwa kuwasilisha mawazo na michango yao kuhusu nini kinapaswa kuingizwa katika Katiba mpya ya klabu.
Uongozi wa Simba unawaomba wapenzi na washabiki wa soka popote walipo duniani kuchangia mawazo katika njia hii. Mawazo yatakayochangiwa kwenye email hii yatatumika katika kutengeneza rasimu ya Katiba hiyo na rasimu hiyo itapelekwa kwenye matawi yote ya klabu kwa ajili ya kujadiliwa na wanachama.
Mawazo hayo ya wanachama yatasaidia katika kutengeneza Katiba ambayo hatimaye itawasilishwa kwenye Mkutano wa Novemba kwa ajili ya mapitio na kupitishwa.
Shime Wana Simba tujitokeze katika mchakato huu kwa faida ya kujenga Simba ya kisasa na yenye tija na ufanisi.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
-- TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments