[wanabidii] operation kimbunga na changamoto zake

Monday, September 16, 2013
Kama kuna jambo linaonyesha namna taifa letu lilivyopita katika changamoto kubwa za kiuongozi na rushwa ni hili swala la uhamiaji haramu na utaratibu wa namna ya kuukabili ulioanzishwa na mkuu wa nchi na kupachikwa jina la operation Kimbungaa. Kwa mtu anayeishi mitaani akikaa na kufanya kazi na jamii ya raia wa nchi jirani au anayetoka mikoa ya mipakani atakubaliana nami kuwa, uwezo wetu wa kupanga na kutekeleza mambo hasa haya yenye sura ya kitaifa ni mdogo mno kiasi cha kujidhalilisha wenyewe mbele ya jirani na wageni wetu. Kwa kifupi yapo mapungufu yanalifanya zoezi zima lisiwe na maana yoyote zaidi ya mtu kutembea uchi barabarani huku akijaribu kuwa lazimisha wanaomuona waseme eti amevaa nguo, waseme amevaa au hajavaa ukweli unabaki kuwa hajavaa. chukua mfano.

1. Wakati wanajua kuwa hakuna mtu anayeishi kijijini bila kufahamika na wanavijiji, kwani kila kijiji huwa kinakuwa na jamii za watu wanaofahamiana, wanatoka maafisa wa idara ya uhamiaji na kwenda kukamata raia kuwatisha na kuwadai rushwa. hawapitii kwa viongozi wa vitongoji wala wa vijiji.
2. Mjini kama Dar, wakati wanajua kuwa hakuna kitambulisho cha kitaifa chenye uwezo wa kumtofautisha kirahisi mtanzania na asiye mtanzania, badala ya kulimaliza hilo kwanza wanaruhusu afisa wa uhamiaji kuingia mitaa kama mtu aliyefunguli fisi kwenye zizi la kondoo, wanawapa mwanya matapeli kujichnganya na kuanza kukusanya pesa toka kwa walimu wanaotoka kenya na uganda na raia wa kutoka mikoa ya mipakani.
3. Kila tapeli sasa ana kitambulisho cha uhamiaji na kazi yake sasa ni kukusanya pesa toka raia wa kigeni na wale wanaotoka mikoa ya mipakani hasa Kigoma, Kagera na Rukwa, wasiotaka kupoteza muda wao kwa kwenda kuhojiwa polisi.
kwa ujumla hali huku mitaani ni mbaya, huwezi kutofautisha afisa halisi wa uhamiaji na feki maana wote wanajikusanyia pesa mwanzo mwisho. ushaihidi ni mwingi, nadhani mwisho wa hili zoezi, serikali itaona aibu kwamba wahamiaji haramu hasa katika miji kama Dar, watakuwa wameongezeka na wengine kujipatia hadhi ya uraia kienyeji kwa kutoa rushwa kwa matapeli na maafisa uhamiaji wasiowaaminifu.
 Ninaamini ingekuwa jambo la maana kuandaa utaratibu mzuri kwanza kwa kuhakikisha kila mtanzania anakitambulisho chake halafu utekelezaji wa zoezi hili uratibiwe vizuri zaidi. wala huhitaji kuwakamata, badala yake watajiondoa au kujisalimisha wenyewe. kwa mfano mtu asiye na ID ya kitaifa hatibiwi, hawezi pata Tigo-M au artell cash, hawi na account au line ya simu mapaka kibali cha polisi au uhamiaji. nani angepona.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments