Ndugu zangu,
Ubora wa jibini hutegemea ubora wa maziwa. Hivyo, kama jibini ni mbaya, basi, maziwa ndio mabaya.
Na katika maisha yetu haya jibini ni sawa na viongozi, na maziwa ni watu. Hivyo, hata viongozi wetu hawa wanatokana na jamii hii hii. Ndio, kama ni viongozi jibini, basi, wanatokana na watu maziwa.
Sasa basi, tunaweza kulalamika, kuwa tuna baadhi ya viongozi ambao ni wabovu na wenye kupwaya majukwaani. Kwamba wakisimama wao ni mabingwa wa kutoa kauli zisizo na busara wala hekima. Wengine utadhani wametoka kuvuta bangi au kwenye vilabu vya pombe ya mataputapu.
Unafanyaje basi, kama jamii, kama maziwa, inazidi kuwa na watu wasio na uelewa mpana wa mambo. Watu wasio na maarifa, wengine hata ya kujua kusoma na kuandika. Na kwamba, viongozi wetu, kama jibini, tunawatarajia watoke miongoni mwa watu hao?
Naam, kama jibini ni mbaya, basi, tatizo ni maziwa.
Ni Neno Fupi La Usiku.
Maggid.
Dar es Salaam.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments