Ndugu zangu,
Kama Mwanafasihi na mshahiri mahiri Shaaban Robert angelikuwa hai ,basi, kwenye hili la mjadala wa Katiba yumkini angetamka;
" Turufu huenda kwa mchezaji...!"
Maana, tunaukumbuka mjadala ule kwenye simulizi ya Mfalme Rai. Ni juu ya mjinga na mwerevu. Naam, mkulima ni mjinga na mwenye duka ni mwerevu. Kwa nini kuna wenye kuamini hivyo?
Ndio, wenye kuamini hivyo wanadhani, kuwa kwa vile mkulima anashika jembe tu, basi, hana halijualo.
Na kwa vile mwenye duka anafanya kazi ya kuhesabu pesa, basi ni mwerevu.
Lakini, kama mwenye duka naye hupata hasara, ina maana nae ni mjinga?
Na ni mkulima anayesemwa kuwa ni mjinga ndiye mwenye kuwalisha wengine, wakiwamo wafanyabiashara.
Na kwa vile wakulima wenye kusemwa kuwa ni wajinga ndio walo wengi, basi, hekima na busara ni kwa Mfalme kuhakikisha kuwa hao ndio walio nyuma yake.
Lililo jema ni kuwasikiliza. Maana, turufu siku zote huenda kwa mchezaji.
Maggid.
Iringa.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments