Shauri la jinai dhidi ya ubinadamu linalomkabili Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto na mwandishi habari Joshua arap Sang linaendelea ICC. Unaweza kufuatilia kupitia TV zote za Kenya, zinaonekana kwenye Vingamuzi mbalimbali.
Lakini bila shaka hawa wazungu watashindwa kwa uovu wao dhidi ya Waafrika.
Ingawa ni hivyo, inabidi Afrika ijifunze na kutoingia mikataba isiyokuwa ya kibinadamu. ICC kwangu ina maana ikiwa ingekuwa Mahakama ya rufaa duniani, kwamba baada ya kesi za mahakama za kikanda, basi kimbilio la rufaa lingekuwa ICC.
Kila la heri William Ruto na Sang, Mungu atawavusha kupitia `daraja la ukweli' muondoke salama ndani ya 'msitu wa maangamizi' kwa Waafrika.
0 Comments