TAARIFA KWA UMMA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUKANUSHA UVUMI KUWA WATEULE WA WAZIRI WAMESAINI POSHO MBILI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUKANUSHA UVUMI KUWA WATEULE WA WAZIRI WAMESAINI POSHO MBILI
Wizara ya Maliasili na Utalii inakanusha uvumi ulioandikwa nakuchapishwa na gazeti la Raia Mwema mnamo tarehe 07/08/2013 ukurasa wa kwanza lililobeba kichwa cha habari UFISADI kama wabunge, wateule wa waziri wasaini posho mara mbili ikiwa na ufafanuzi kuwa yumo Ofisa Takukuru,walipwa na taaasisi wanayoichunguza. Taarifa hii ilikuwa na muendelezo zaidi ukurasa wa tatu wa gazeti hilo.
Wizara inasisitiza kuwa uvumi huo siyo kweli kutokana na sababu zifuatazo:
Wizara inasisitiza kuwa uvumi huo siyo kweli kutokana na sababu zifuatazo:
Wizara ya Maliasili na Utalii imesikitishwa na kitendo cha gazeti la Raia Mwema, gazeti ambalo limejijengea sifa na kuaminiwa na jamii kwa kutoa taarifa za uhakika zinazofuata maadili ya utoaji taarifa kwa vyombo vya habari, kuchapisha habari zinazochafua jina la Wizara, Wabunge na Serikali kiujumla bila kujihakikishia ukweli wa taarifa hizo kutoka wizara husika.
Kwa taarifa hii, Wizara inalitaka Gazeti la Raia Mwema kufuta uvumi waliochapisha kwenye gazeti lao kama ilivyotajwa hapo juu na pia kuiomba radhi Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuchapisha habari ambazo si sahihi na pia kuchafua jina la Wizara.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
12/08/2013
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments