Posted: 14 Aug 2013 10:33 PM PDT Trafiki feki akiwa amesimama akiwa amevalia sare za trafiki huku ameshikilia jadala lake la kazi.- ANA CHEO CHA SAJINI,VITABU VYA KOTOZA FAINI
- WANANCHI WATOA USHUHUDA JINSI WANAVYOMFAHAMU
Na Waandishi Wetu MSEMO wa mjini mipango, umejidhihirisha wazi baada ya Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kumkamata askari bandia wa kikosi cha usalama barabarani akiwa amevalia sare za trafiki akiendelea na kazi pasipo kugundulika kwa siku kadhaa kuwa anafanya uhalifu. Trafiki huyo bandia mwenye cheo cha sajini, (jina halikupatikana) alikamatwa na Polisi akiwa 'kazini' maeneo ya Tabata Kinyerezi akiwa amevaa sare mpya ya Askari wa Usalama Barabarani, kikoti cha kuakisi mwanga na kofia nyeupe. Pia trafiki huyo alikuwa na jalada pamoja na kitabu cha kutoza faini (Notification) kwa madereva wanaopatikana na makosa ya kukiuka sheria za usalama barabarani. Gazeti hili lilishuhudia trafiki huyo feki akiwa amekamatwa na Polisi na kisha kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi Kati, huku akijifanya amepoteza fahamu. Mashuhuda waliozungumza na gazeti hili, walisema wanamfahamu trafiki huyo kwa muda mrefu kiasi kwamba madereva wengi wanamuogopa, kwani akikamata gari hakuna cha majadiliano kama ilivyo kwa wengine, bali anawatoza faini moja kwa moja kati ya sh. 20,000 hadi 25,000. "Yule tunamfahamu kwa uchapaji kazi, alikuwa hataki rushwa hata kidogo, akikukamata ujue umeumia, lazima akuandikie 'notification'," alisema dereva mmoja anayemfahamu trafiki huyo kwa muda mrefu. "Wakati wa foleni alikuwa akisimama barabarani na kuanza kuyaongoza magari, lakini alipoona imekuwa kubwa zaidi alikuwa akiondoka kwa kuhofia kujulikana," alisema shuhuda mwingine. Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam anayemfahamu trafiki huyo, alisema; "Namfahamu huyu jamaa mambo yake ni mazuri sana nyumbani kwake, hivi sio trafiki... ahaaa haiwezekani bwana." Aliongeza kuwa; "Yule trafiki huwa anatanua sana kwenye baa na kama kulikuwa na ugeni wa viongozi hasa wa nje alikuwa akisema anawahi kwenda kulala, kwani ataamka mapema kwenda kuongoza misafara." B a a d h i y a m a d e r e v a wanaomfahamu trafiki huyo, walisema hawaamini kama kweli mtu huyo ni trafiki feki kwani wakati mwingine alipokutana na askari wenye vyeo vidogo chini yake walimsalimia kijeshi. Mashuhuda hao walisema trafiki huyo alikuwa akifanyakazi kwenye maeneo ya Mkuranga na wakati mwingine alionekana akiwapangia kazi vijana walio kwenye vikundi vya Polisi Jamii ambao wanasaidia kuongoza magari. Kwa mujibu wa watoa taarifa hao, vijana wa Polisi Jamii walipomkamata dereva amekiuka sheria za barabarani, walielekezwa kwa trafiki huyo ambaye bila mjadala aliwaandikia notification. Watu waliotoa maoni kuhusu tukio hilo, walilihusisha na uzembe katika Jeshi la Polisi kiasi cha kushindwa kujitambua. "Hawa wenzetu Jeshi la Polisi hawajajitambua, haiwezekani watu washindwe kutambuana wakati wanafanyakazi pamoja na mtu huyo," alisema John Edward. Lakini pamoja na kulishutumu Jeshi la Polisi, baadhi ya watu walionekana kufurahishwa na kitendo cha trafiki huyo feki wakisema ni mbunifu wa ajira. "Ingawa amefanya makosa kwangu mimi naona ni mbunifu wa ajira na amelisaidia sana jeshi la Polisi kwani walikuwa wanakaribia eneo lake la kazi madereva walikuwa waangalifu sana ili kuepuka kupigwa notification," alisema Edward.  |
Posted: 14 Aug 2013 08:59 PM PDT Rehema Maigala na Darlin Said KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Ponda Issa Ponda, amesomewa mashtaka yanayomkabili chini ya ulinzi mkali wa Polisi wodini katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).Ponda alisomewa mashtaka yanayomkabili jana jioni mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hellen Liwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Tumaini Kweka .Ilidaiwa na upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa huyo, Shekhe Ponda, anakabiliwa na mashtaka mawili aliyotenda Juni 2 na Agosti 11, mwaka huu sehemu mbalimbali.Ilidaiwa kuwa Shekhe Ponda alichochea vurugu sehemu mbalimbali za Tanzania. Ilidaiwa kuwa Shekhe Ponda, Agosti 11, mwaka huu alihamasisha vurugu. Pia inadaiwa kuwa Juni 2, mwaka huu Ponda alishiriki tena kuhamasisha vurugu. Sehekhe Ponda alikana mashtaka hayo na kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 28, mwaka huu, ambapo mshtakiwa ataendelea kuwepo hospitali kwa ajili ya matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusomwa kwa mashtaka hayo, Wakili wa Shekhe Ponda, Juma Nassoro, alisema hati hiyo ina makosa kwani Agosti 11, mwaka huu siku ambayo anadaiwa kutenda kosa hilo, alikuwa tayari amelazwa hospitalini, hivyo wataleta pingamizi la kufuta kesi hiyo itakapotajwa. Alisema leo walikubaliana a f a n y iwe ma h o j i a n o kwa kumtuhumu kufanya uchochezi maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Morogoro."Tulipinga yasifanyike mahojiano hayo kwa kuwa Shekhe Ponda ameishawasilisha malalamiko yake Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutokana na polisi kudai kuwa hawajampiga risasi Shekhe Ponda," alisema wakili huyo. Pia alisema Ponda ameishapeleka malalamiko yake Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Aliongeza kwamba mahojiano hayo hayakufanyika kutokana na hali ya Shekhe Ponda kutokuwa nzuri. "Lakini baada ya saa tatu wamemsomea mashtaka kuanzia saa 10 jioni," alisema.Nje ya MOI ulinzi uliimarishwa na hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia wodini kuangalia wagonjwa kwenye block aliyolazwa Shekhe Ponda. Magari ya Polisi yasiyopungua manne yalikuwa yameegeshwa eneo hilo yakiwa na askari polisi waliojidhatiti kwa silaha.Wafuasi wa Shekhe Ponda walisikika wakilalamika baada ya kuzuiwa kuingia wodini kumuona na kuhoji; "Kila sehemu mnatuzuia, tunahitaji kumuona Shekhe  |
Posted: 14 Aug 2013 09:00 PM PDT Na Leah Daudi CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetengua uamuzi uliotolewa na Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera kuwavua udiwani madiwani nane wa chama hicho uliofikiwa juzi mkoani humo hadi itakapoamuliwa vinginevyo na Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa itakayokutana .Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye, alisema madiwani hao waliokuwa wamesimamishwa kazi wanatakiwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida wakisubiri uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika Agosti 23, mwaka huu, mkoani Dodoma. Alisema kikao hicho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Kagera.Nape alisema utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa wabunge na madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho. Alifafanua kuwa uamuzi unatakiwa kupata baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na ndio utekelezwe. Alisisitiza kuwa uamuzi ulitakiwa kupitia katika Baraza la Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa ndipo uchukuliwe na sio vinginevyo. Alisema tayari wamepokea barua za kukata rufaa kutoka kwa madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa hoja kwamba taratibu zilikiukwa wakati wa kufikia uamuzi huo. Juzi Halmashauri Kuu ya CCM ilitangaza kuwafukuza uanachama madiwani hao Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba ambaye pia ni Diwani wa Kashai, Yusuph Ngaiza, Alexander Ngalinda (Buhembe), Samuel Ruhangisa (Kitendaguro), Dauda Kalumuna (Ijuganyondo), Deus Mutakyahwa (Nyanga) na Robert Katunzi (Hamugembe).Wengine Richard Gasper (Mihembeni) Mulundi Baduru Kichwabuta (Viti maalum).  |
Posted: 14 Aug 2013 09:02 PM PDT Grace Ndossa na David John SERIKALI imesema mtandao wa majangili wanaoua tembo mkubwa wenye watu walio na uwezo kifedha ambapo wapo ndani na nje ya nchi .Siri hiyo ilifichuliwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii .Alisema tayari Serikali ina majina ya mtandao unaojihusisha na biashara ya ujangili wa meno ya tembo na baadhi yao wapo pia wafanyabiashara wakubwa waliopo ndani na nje ya nchi."Tayari majina tunayo ya mtandao wa watu wanaojishughulisha na ujangili wa meno ya tembo huu ni mkubwa ambao una pesa nyingi, hauna tofauti na ule wa dawa za kulevya,"alisema A l i s e m a s i o k w a m b a wameshindwa kufanya kazi bali wanaendelea kupatataari fa nawameandaa operes heniuhai itakayosak aw alewo teambao wanahusikan aujang ilihuo .Alionge zakuwawanaen delea kufuatilianch i inay onunuamenohayo am baponch i zili zopoBarala Asianimiongo nimwazinaz ohusi kanabiashar ahiy o.Ali sema siorahisi ku shindav itahi yokwaku tumiavyombovya habar i. "Mnaj uah ii nivita kubwa na niwaamb iekuwavita hiihuw ezi kushindakw a kutu miav yom bovyahabari, hiv yoWatanzan iakuweninaamaninatun ajitahidiku hakikis ha tunamaliz atatiz ohili,"alis ema.Katikah atuan yingi ne,alisema mfumowademokrasia uliopounacha ngia kurudishanyuma jitihada mbalimbali zinazofanywa, kwani watu wakikamatwa na kupelekwa mahakamani kesho yake wanaonekana mtaani. Alisema wanaobainika kufanya biashara hiyo ya ujangili hata Polisi wamo na wengine wameshafukuzwa kazi na wengine kusimamishwa, hivyo hizo zote ni jitihada za Wizara yake.Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo John Lembei alisema kuwa kamati yake imeiomba Serikali kuondoa kodi ya asilimia tatu ambayo ilipitishwa na bunge kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya utalii na asilimia kumi ambayo yalikuwa yanawasilishwa Serikalini kwani inachangia kuondoa huduma za jamii zilizokuwa zikitolewa kwenye jamii inayozunguka hifadhi hizo. Alisema kamati imeomba serikali kama kweli wanataka kuendeleza sekta ya utalii basi kodi hiyo ifutwe vinginevyo hifadhi hazitakuwa salama na ujangili utaongezeka kwa kiasi kikubwa."Hifadhi hizi za TANAPA na ngorongoro ilikuwa miradi ya kusaidia jamii inayowazunguka kwa kuwajengea shule, hospitali, maji, pamoja na huduma zinginezo hivyo kutokana na bunge kupitisha kodi hiyo wameondoa huduma hizo,"alisema Lembei.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:04 PM PDT Na Mwandishi wetu, Arusha JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia wakazi watano wa kijiji cha Kisimilijuu wilayani Ar ume r u , wa k i t u h umiwa kukamatwa na magunia 352 dawa za kulevya aina ya bangi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema magunia hayo yalikamatwa jana, kutokana na msako maalumu unaoendelea mkoani humo. "Tumeyakamata wakati wa operesheni ambayo tumeiendesha kwa siku mbili katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha na kufanikiwa kupata magunia hayo ambapo 225 tayari yametekezwa kwa moto na yaliyobaki yatachukuliwa kama uthibitisho mahakamani,"alisema Kamanda huyo. Aliwataja watuhumiwa watano waliokamatwa wakati wa msako huo kuwa ni Esubhati Daudi (24), Atumii Daudi (28), Lemali Saitoti (40), Thomas Semile (60), Lomayani Thomas (42), wakazi wa kijijini hapo walikamatwa. Alisema watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi kukamilika. Alitoa onyo kuwa jeshi hilo halitawaonea haya watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, kwa kuwa wanaenda kinyume cha sheria ya nchi.  |
Posted: 14 Aug 2013 10:09 PM PDT Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, mkoani Mtwara, Bw. Dusntan Mkapa (kulia), akimshukuru Meneja wa Kanda ya Kusini wa NMB, Bi. Lilian Mwinula, mara baada ya kukabidhi msaada wa vitanda na magodoro kwa Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu jana. Msaada huo una thamani ya sh. milioni 5.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:07 PM PDT Na Amina Athumani WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira amesema Rais Jakaya Kikwete amesisitiza atawajibisha mawaziri wote watakaozembea kutimiza majukumu yao ikiwemo mipango ya maendeleo nchini. Hayo aliyasema juzi jijini Dar es Salaam wakati akieleza mkakati wa Serikali katika kutekeleza mfumo ujulikanao kama 'Matokeo Makubwa Sasa'. Waziri Wassira alisema, katika utekelezaji wa mfumo huo watendaji hasa mawaziri watakaozembea majukumu yao watawajibishwa na kiongozi mkuu wa Serikali ambaye ni Rais. Alisema, lengo la mfumo huo ni kuleta matokeo mazuri ya uchumi kwa muda mfupi. Pia alisema, mfumo huo utagharimu zaidi ya sh. trilioni 8.9 kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo Serikali itawekeza kiasi cha sh. trilioni 2.9 huku sekta binafsi zikitarajiwa kuwekeza sh. trilioni 6. Alisisitiza kuwa, mafanikio ya mfumo huo yatategemea na ushiriki mkubwa kutoka katika sekta binafsi Wa z i r i Wa s s i r a alizihakikishia sekta binafsi kwamba Serikali iko pamoja nao katika shughuli za kibiashara. Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi na Makampuni Binafsi nchini, Ally Mafuruki alipongeza hatua ya Serikali kusitisha kuagiza samani nje ya nchi kwa ajili ya matumizi ya Serikali ambayo sasa itazinunua katika soko la ndani. Mwenyekiti huyo pia ameitaka Serikali iweke v i g e z o v y a u b o r a i l i wazalishaji wa ndani wa samani hizo wazitimize.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:09 PM PDT Na Rachel Balama MA H A K A M A K u u Kanda ya Dar es Salaam imeombwa kutengua hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu dhidi ya wafuasi 52 wa Shekhe Ponda Issa Ponda, waliohukumiwa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela. Kwa kuwa, hakuna ushahidi wa kuonesha kwamba washtakiwa hao waliandamana isipokuwa hakimu aliwatia hatiani kutokana na kujiridhisha kwamba washtakiwa walitenda kosa wakati anaandika hukumu. Wafungwa hao, kupitia wakili wao, Mohamed Tibanyendela wanapinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu ambapo pamoja na mambo mengine, wanadai hakimu hakuzingatia matakwa ya msingi kisheria ili kuwatia washtakiwa hatiani. Akiwasilisha rufaa hiyo jana mbele ya Jaji Salvatory Bongole, wakili Tibanyendela alidai, hakimu hakuwa na ushahidi wa kujiridhisha kwamba kulikuwa na njama za kukubaliana kutenda kosa miongoni mwa washtakiwa na badala yake alikuwa na dhamira ya kuwatia hatiani wakati akiandika hukumu hiyo. Alidai, hukumu iliyotolewa na ushahidi uliorekodiwa una upungufu mkubwa kwenye ushahidi wa Serikali hivyo hakukuwa na msingi wowote wa kiushahidi kisheria wa kuweza kuwatia hatiani washtakiwa. Alidai, katika hukumu hiyo mwongozo wa kuandika hukumu kisheria haukufuatwa na badala yake washtakiwa wote waliingizwa kwenye kundi moja na kutiwa hatiani kwa makosa yote bila kuchambua vifungu vya sheria kwa makosa waliyoshtakiwa nayo. Wakili alidai hakimu alishindwa kuchambua ushahidi uliotolewa mbele yake, ni dhahiri kwamba hakimu alitoa hukumu bila kubainisha anawatia hatiani washtakiwa kwa sheria ipi. Alidai, katika hukumu hiyo ushahidi haujajitosheleza isipokuwa hakimu alitengeneza ushahidi wake kwa kuwa alikuwa na dhamira yake ya kuwatia hatiani washtakiwa kabla ya hukumu. Aliendelea kudai kuwa, vitu kama panga, visu, mabango na vinginevyo haviwezi kuthibitisha kosa lilifanyika ambapo kwa ushahidi uliotolewa na washtakiwa unaonesha kwamba baadhi ya washtakiwa walio waongoza polisi kwenda kuwakamata washtakiwa wengine na washtakiwa hao hawakukamatwa wakati mmoja. Pia wanadai kuwa, katika hukumu hiyo, hakimu alijikanganya kwa kumwachia huru mmoja wa washtakiwa na kuwatia hatiani washtakiwa wengine. Machi, mwaka huu, Hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu washtakiwa hao wa kesi ya kula njama na kufanya maandamano isivyo halali kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kuwatia hatiani katika makosa yaliyokuwa yakiwakabili. Washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Februari 15 mwaka huu. Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya tukio Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama za kufanya maandamano isivyo halali. Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha uvunjifu wa amani. Shtaka la tatu ilidaiwa kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walikiuka amri ya Jeshi la Polisi ya kutoa zuio la kufanya maandamano, n a k u f a n y a mk u s a n y i k o uliosababisha vurugu na uvunjifu wa amani. Katika shtaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:15 PM PDT Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Saruji Tanga (TCCL) na TDI imezindua ujenzi wa uchimbaji msingi kwa ajili ya kupanua kiwanda hicho mkoani Tanga ili kuongeza uzalishaji wa saruji awamu ya pili tani 775,000 kwa mwaka. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambao ulifanyika jana kiwandani hapo eneo la Pongwe mkoani humo, Mwenyekiti wa Bodi ya TCCL, Lau Masha alisema awamu ya kwanza ya upanuzi wa kiwanda ilifanyika mwaka 2009-2010 na awamu hii ya pili itakamilika mwaka 2015. Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola la kimarekani milioni 165 hadi kukamilika. "Ndipo, tuliposimika mtambo wa pili wa kusaga saruji, mashine ya kupakia saruji ambavyo kwa pamoja viliongeza uwezo wa kusaga saruji kwa asilimia 73, kufikia tani milioni 1.3 kwa mwaka," alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi. Alisema, uwezo wa uzalishaji clinker ulibakia tani laki tano kwa mwaka, hivyo kuwalazimu kuziba uwiano huo wa clinker na saruji kwa kuagiza clinker kutoka nje. "Kama mnavyojua bidhaa hii (clinker) kutoka nje inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwepo kuyumba kwa thamani ya fedha za kigeni, mfumuko wa bei na uharamia katika eneo la Ghuba. "Mradi huu umekuwa kwenye maandalizi kwa muda mrefu, hivyo tunayo furaha kubwa kwamba leo (jana) tunazindua uanzilishi wa ujenzi wake," aliongeza Mwenyekiti huyo. Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo alisema mradi huo utahusisha ujenzi wa 'kiln' mpya, pamoja na 'crusher' eneo la kuchanganyia malighafi, mtambo wa kusaga udongo na mkaa. "Gharama za mradi huu unakisiwa kuwa dola za kimarekani milioni 165 na ujenzi wake unategemewa kumalizika kwenye robo ya kwanza ya mwaka 2015. "Bodi yetu ina imani kwamba wahusika na wadau wote wa mradi huu watatekeleza wajibu wao kikamilifu, kuhakikisha kumalizika kwa ujenzi wa mradi huu kwa muda uliopangwa," alisema. Mbali na kuongeza uwezo wa kuzalisha clinker ili kuendana na uwezo wa kusaga saruji alisema mradi huo pia utasaidia kupunguza gharama za uzalishaji, pia utaongeza ubora na wingi wa saruji hapa nchini. "Mradi huu unadhihirisha imani waliyo nayo wawekezaji kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika juhudi zake za kuhakikisha utulivu na amani nchini, pamoja na mazingira bora ya kibiashara. "Kama kawaida yetu kwa miaka mingi, Tanga Cement (Kampuni ya Saruji Tanga) itaendelea na juhudi zake za kuendeleza huduma kwa jamii, ikilenga katika nyanja za afya, elimu, mazingira na maendeleo ya jamii," aliongeza Mwenyekiti huyo wa Bodi. Awali Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa, mwaka jana kampuni yake ilitumia zaidi ya sh. milioni 400 kwenye huduma za kijamii ambapo kati ya hizo asilimia 37 ilikuwa kwa Mkoa wa Tanga peke yake.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:16 PM PDT Na Rehema Mohamed MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imedai aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda na wenzake wawili waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uchochezi wana kesi ya kujibu na hivyo kutakiwa kujitetea. Mbali ya Kibanda, washtakiwa wengine ni Meneja Uendelezaji Bi a s h a r a wa Kamp u n i y a Mwananchi Communications (MCL), Theophil Makunga na mwandishi wa Tanzania Daima Samson Mwigamba. Washtakiwa hao walikutwa wana kesi ya kujibu jana na Hakimu Mkazi Warialwande Lema, muda mfupi baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao na Wakili wa Serikali Beata Kitau kudai kuwa hawana mashahidi wengine. Baada ya kusema hayo, Wakili wa utetezi Issaya Matambo, aliomba wapewe nafasi ya kuweza kuwasilisha hoja za kisheria iwapo wanaona washtakiwa wana kesi ya kujibu au la. Hata hivyo, Hakimu Lema alisema kuwa ameshapitia ushahidi wa upande wa Jamhuri na kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu na hivyo wanatakiwa kutoa utetezi wao. "Baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao na kwa kuzingatia ushahidi uliopo mahakamani, mahakama inaona washtakiwa wote wana kesi ya kujibu hivyo waje kutoa utetezi wao," alisema Hakimu Lema. Hakimu Lema amepanga washtakiwa hao waanze kujitetea Septemba 3, mwaka huu. Katika hatua, nyingine mshtakiwa wa kwanza Mwigamba jana hakuwepo mahakamani ambapo mzamini wake Rose Moshi alisema kuwa anaumwa. Alisema kuwa, mshtakiwa huyo amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas Arusha ambapo Hakimu Lema alimtaka mzamini huyo kuja na vielelezo vya kulazwa kwake tarehe ijayo ya kesi la sivyo atatoa amri akamatwe. Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mwaka jana, wakikabiliwa na mashtaka ya kuandika na kuruhusu kuchapisha makala ya uchochezi. Makunga, ambaye ni mshtakiwa wa tatu aliunganishwa katika kesi hiyo kutokana na kampuni yake kuchapisha gazeti la Tanzania Daima likiwa na makala hiyo inayodaiwa kuwa ya uchochezi, wakati alipokuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MCL. Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo, kutokana na makala inayodaiwa ya uchochezi iliyochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima la Novemba 30, 2011, iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho 'Waraka Maalumu kwa askari wote'. Makala hiyo inadaiwa kuandikwa na Mwandishi wa Safu ya Kalamu ya Mwigamba, Samson Mwigamba ambaye ni mshtakiwa wa kwanza. Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo, wakidaiwa kuandika na kuruhusu kuchapisha makala yenye uchochezi dhidi ya askari wa majeshi mbalimbali nchini.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:19 PM PDT Na Reuben Kagaruki KAMPU NI yaBia Tanz ania(TBL)imeend eleak uwamoja ya vyanzoviku uvyamapa toyaSerikali kwaku lipa kodiya Ongeze kol aThamani(VAT) ya sh. bilioni345 k wa mwak a.Ha yoyalisemwaDar e sSalaamjanana Mwenyeki ti waB odi ya Wakuru genziyaTBL , Waz iri MstaafuCleopa Ms uya,wakatiwaMkutano w a wana hisa. Alisemamalipohayoni ongezeko laasilimia 10.6za idi yamwa kaul iopita. "Kiwang ohiki ni sawana upu ngufu waasilimia16yaushuruwalengolilil owekwa na Se rikali," alisemaMsuy a.Aliba inishakuwa fedha taslimu zilizotokana na uendeshaji zilifika sh.bilio ni311. Kwam ujibuwaMs uyaka tikafedha hizo, sh. bil ioni 70z ili tumika kulipiakodi yakampun inazilizobaki zilitu mikakwaa jili yakulipa riba, mtaji na kulip agawio . "Bodii liid hinisha gawiola kihistori alash. 300kwa h isaambayoiliku wa kiasic haasilimia zaidi ya 50yagawi ola mwakajana,"alisema.Aliwaambia wajumbe wa mkuta nohuokuwaubora wa bidhaana ubore shaji h udumakwawatejavimeen deleaku wa sehemumadhu buti yamalen gonadhamira kwa wateja wa kampuni kwa wateja wake. Kwamuj ibu w aMsuya, Tan zania Distille riesLTDi meendeleakuwana kiwango kizuri katika uzalishaji ambapo mwishonim wamwaka ulikuwakwa asilimi a17.4 ."Kwamwaka huuu lishuhudia kuzind uliwakwa MwanzaTraditional Beer,k iwandachakuzalisha kinywaj isafi cha bei nafuukwakufikiaasilim ia1 65kwamwak a iki lingani shwana mw aka jana. Kwa upande wa mwaka huu ali sema w ameende leanajuhudi zakufikiamalengowal iyoj iwekeakwa kutumia uong oziwa mfu mowamotishakwanga zizoteza kiutendaji ka tikakamp uni.Alisemana mnampya ya kiutenda ji yarasil ima li wa tuimesaidiaubore shajiwafursaza rasi limali wa tunamuelekeo mzima washughuliza ki utendaji. Kwa kipindi kijacho, alisema ufanisi wakampun iyaTBLutategemea uchumie nde levu, kiwang o chaongezekolaushuru,, bei yamafuta , gharama za umemenamaji,kupan uka kwamt and aowa mi undom binunat hama niyasar afuyaTanzania. " Katika mazingira haya naamini kuwa t ukiunganishap amoja utendaji wetu,uwajibikaji wetupamojanafursa hizi ,tuta hakikisha kuwa ka mpuni yaT BLitaibukakuwaimarazai di n a kuweza kuhimiliushind anikwamaslahi yawanahisa, wadauwabiashara na uchumi kwa ujumla ,"al isema.Kwaupandemwingine , Msuyaalisema matokeo mazuri yakampuni yameto kanana mchangowak ila mmojakama mabalozi wa zur iwakampuni.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:20 PM PDT Na Mwandishi Wetu BENKIya CRDB im ezindua hudum ampyay amikopoyany umbainayoj ulikan a kam aJijenge yenyelengolakuwawezeshawa tejawak epamoja na wafanyaka zikup ataf ursa yakumiliki nyum baauuk arabati wa nyumbakwaghar am anafuu. A kizungumza katikahafla yauzinduzi wahuduma hiyojanaDares S alaam,mkurugenzimten daj i wabenki hiyo, Dkt. Char lesKimeialise mab enki hiyoime amua ku fikiahatu ahiyoili kuwaw ezeshawananchi wengi kumilikinyumba . Ali semakuwatafiti mbal imbali hapanchi ni zin aoneshakuwaku na upungufu wan yumba zaidi yamilioni tatuhuk ukila mwakazikijen gwanyu mba e lfuishi rini pekeehiv yokamaha tuazamakus udi z isipochukuliwa hali itazidikuwambaya. "Hu dumahiiitawawez eshawatukumi liki nyumbakwa gha ramanafuu zai diambapomu da wakure jeshaniha di miak a20ikilinga nishwan aainanyi ng inezamikopoambayo hu tole wanaben ki hii,"alise maDkt. Ki mei. Ai dhaali ongezakuwa watu wengiw ameshind wakumiliki nyumb akutokanana gharamakuwa juulak inisa sa benkih iyoimeanzis hanj iambadal aya kukopeshanyumbaam bap omteja atatakiwa k ulipa kia sichaas ilimia18yafedhahizokwamwaka. A ki fafanu a zai di ku husianana huduma hiy oDkt. K imei alis emamfumowaku jenganyumbahivi sasakwakuji wekeaa kibani wakizam ani haliambay oinam fanya mfany aka zi k ufa nyakazi kwamiaka20au30bila kumiliki nyumba. Hivyokutokana na hali kama hiyo watejamb alimbalinawa fanyakazi sanjari nawajasiria ma li watawezakupataf ursazak upa tami kopoya nyumb aamb ayo ribaza keni naf uunazinaendMt anzania  |
Posted: 14 Aug 2013 09:22 PM PDT JUMLAyash.b ilioni 180zinatarajia kut umikakatikamradi waujenziwanyumb a 1 0,000kwa ajili ya wa tumishiwaumma zinazoje ngwanaWa kalawaMajengoNchini (TB A),anari poti Fatuma Mshamu. Ha yoyamebainishwajanak atika ziaraya kutembelea ny umb ahizozilizopo Bun ju BDar es Salaamnamratibuwamra di huoMhand isi Majengo,Hum phre yKillo wakati akitoa taa rifakwaN aibuWaziriwa Ujenzi, mhandisi Gerson Lwenge. Alise ma katik aaw amuyakwanzayamradihu osh.bili oni 2.2z ilitumikanahadi sas a n yumba 155 zimeanza ku jengwanakati yahiz onyumb a 25zipo katika hatua yaku wekamaba ti. Kati kaz iarayakutembelea mradihu oMh and isi Lwengealisem a, Wakala wamaj engoni watuwakwanzakutu miamfum owa uje nzitokanchiyaU turukiambaouna ghar ama n afu ukwani bei yakunu nu an yumba it akuwani sh.mil ioni30tu tofautin amajeng oyanayojengwanawaha ndisi wengine kwani gh ara ma zaohuwajuusana. A lisema, jengo la serikali ni kuona watum ishi wa kewo tewa na kaakatikanyumbazen yeubo ranakati yanyu mbahizozitapan gishwanafed hazitaka zopa tikanazitatumi ka katikauj enz i wanyumb azingine. Mra dihuounata rajiwaku kamilikaOktobam wak ahuuha tahivyomhandis ihuyoal iwata kaku ongeza kasi ya ujenziili kukamilika kwa wakatiuliopan gwa.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:25 PM PDT NaGladne ssTheonest aliy ekuwaBu koba HALMASHAURI yaMjiwa Bukoba hainama gari yama jitak akwa ta kribani miaka16nah ivyokulazimika kutumi amag ari yawa tubi nafsi katikak utoahudum ahi yokwawananchi.Akizungumza na Majira hivi karibuni K aim uAfisaAfyawa ManispaayaBu koba, Swau muMsofealise ma kuwa Manisp aa imeshi ndwakununuamagariyamajitaka kw akipind i hich ochotekutok ananam agarihayoku uzwa kwa gharama kubwa ambapo gari moja linauzwa kiasi cha sh.milioni 900 .Alisem ak uwakutokana nagharamahiz okuwa kubwa mwaka 2008,M anis paaililazi mikakutoa zabun ikwakam punibina fsi zaRwab izin aMu kwano amb azok ilamojaina g arimojak waajil iya kusai dia k utoahudumayaunyonyaji majitakakwa wananc hi. "Tumesh indwaku nu nuagari la majitakakutoka nanagha ramazaunu nuziwagari hilokuwa ku bwandio ma anailitul azimukutumiaka mpunibin afs i iliziwezekutusaid iakwaaj iliyauto aji wa hud umahiyokwawan anchiwa mji waBuko ba," alise maMsofe .Kai muAfisaA fyahuyoa lisemakuwaMa nispa ainaj ipang akatika ununuziwag arilamajitakalakini haijajuli kan ani li ni wa tatek elezasualahilo. Aid ha, kwa upande mwingine Ms ofealise makuwapa moja nakuw epokwa maga rihayolakinibado wakaziwaBukobawamek uwahawayat umi i magari hayonabad ala yak ewamekuwawakit irir ishakinyesizi wani kupitia mto Kano ni. Majirailizungumza na baadhi yawan anchi ambapoha wakutakama jinayaoyaandik wegazetini ambapowalisema wamek uwa hawatum ii magariy a majitakaya kampuni hizo kutokana na kuwalipisha gharama kubwa ambazo wamekuwa wanashindwa kuzimudu. Mwandishi wa habari hii aliwasiliana kwa njia ya simu na mmoja wa madereva katika kampuni ya Rwabizi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema kuwa hivi sasa mji huo una gari moja tu na lingine lilienda Kahama. Kwa siku Mji wa Bukoba unazalisha lita 232,876.7 za maji taka jambo ambalo linaonyesha kuwa magari hayo hata kama yangekuwapo yote mawili hayawezi kukidhi mahitaji ya mji mzima.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:26 PM PDT MKUUwaWilayayaI gunga mkoani T abo ra, Eliba rik iKinguamewaasavio ngoziw adini kutojihusish a namasual aya siasanabadala yake wajengemi singiya kirohokwawaumini ilinchi iendeleek uwanaamani,anaripoti Abdalla hAmi ri, Igunga .Ha yoaliyasemamw ish onimwawikika tika tamas halauzin duzi waalbam u yan yimbozai njili ya, AnnaNzog iijulikan ayo kwajinalaNjo onitumwimbi e b wana uliof an yikakati ka ukumbiwaShuleyaMsingi St.Leo the Great uliopo mj ini Igunga. A lisem a kuwabaad hiyaviongozi wadiniwameku wawa ki jihusishana masuala yasias anakuacha kumtumikiaMu nguh ali ambayoina letamfarakano katika shughuli zamae ndeleo. Aliongezakuwabaadhiyawananchi wam ekuwa wakitum ia fedha nyingi kwakufanyamamboyasiyompendeza Mungu badala ya kuwekeza katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kutoa sadaka. "Ndugu waumini mliokusanyika katika tamasha hili, leo nimeona niyaseme haya kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kwenda kwa waganga wa kienyeji na kudanganywa na hatimaye kujiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinamchukiza mwenyezi mungu," alisema Kingu. Katika tamasha hilo lilienda sambamba na harambee ya kuchangia kwaya ya Jerusalemu ya Kanisa la Moravian mjini Igunga kwa ajili ya kusaidia watoto yatima, wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Aidha, katika harambee hiyo jumla ya sh.milioni 1.4 zilichangwa ambapo mkuu huyo wa wilaya alichangia kiasi cha sh.650,000. Naye mlezi wa Kwaya ya Jerusalemu ya Kanisa la Moravian mjini Igunga, Nyanza Sulwa aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa liendelee kuwa na amani. Alisema kuwa ili nchi izidi kuwa na amani ni vyema wananchi waendelee kumuomba Mungu kwani kumekuwa na viashilia mbalimbali vya uvunjifu wa amani ambapo watu wamekuwa wakimwagiwa tindikali na kupigwa risasi pasipo makosa yoyote. Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la Moravian mjini Igunga, Isaya Misayo aliwataka waimbaji wa nyimbo za injili kutotanguliza masilahi mbele na badala yake wafanye kwa ajili ya kumtumikia Mungu. Aliongeza kuwa kumekuwa na baadhi ya watu wanaotumia mambo ya dini kwa nia ya kujipatia vipato vyao binafsi na kuwaasa waachane na tabia hizo.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:28 PM PDT BENKI Ku uyaTanzania(BoT) KandayaK as kazini A rushaimewatah adhar ishawa nanchi kuchukuahatuamape majuu yawimbilanoti bandi ahapanchini kwa ku wa takawawem akini wakatiwakutoa amakupo ke anot i mpya ili kue pukak ufili sikanata ifakuyumbakiuchumi,anaripoti Richard Konga, Aru sha. Aidhab enk ihiyoimean zisha utaratibu wak utoa elimukwawa nanchii li kutamb uanoti bandianahalali kupitiaala mahalisi zilizokok weny enoti hal ali na kusisitiz akwaw ananchikuwama chokwa kuzitambu a alamahizoilikuep ukakuruhusumatumiz i ya not ifekikuingia kwenye mzunguko wak awa ida. A kizungumzakwenyemaonyes hoyawakulima Na ne nane , Kandaya Kaskazin i, M enejawaFe dhanaUtawalawaBenki hiy o,Eve na Ndesing oalisemakuwaB oTimeanzak utumia m aonesh oya wakulima an enan ekutoa elimu ya utambuziw an otiza ke. Ali sema mao nyeshoyali yofany ikajijiniArushawanan chizaidiya 10,000w am epatiw aelim u ya utambuz iwaalamaza notimpyalengo ikiwani kuwa fikiawananchi zaidiwaliop ohapanchi ni kupitiamatawi yake. HatahivyoNdesingo alibainisha kuwamat umiziyan oti bandia kwa ja miiyamek uwa yakipunguamwak ahad im wakakut okananajamiiku wana uelewa wanoti ha lisi nabandiana h ivyo kup unguza kasi ya mzung ukowan otibandiakwakiasikiku bwa. Ai dhaalisema kuwa BoT kupitiama tawiyakeha panchiniimejiza titikuwa elimis hawa nanchi juuya utambuz iwan otimpya naalam azake ilij ami iizi elewena kutofautisha notih alalinabandia. Alisemanoti band ia iwapo zitaach waziende lee kuwepokwenyemz ungukowamatumizi ya kawai daipohat arik wajamii kufilisikasa njari nataif akup otezauchum i wak e, kwah iyoa liitakajamiikuwamakin isan apindi wana pokuw awan apokeaamakutoa notimpyak wakuanga lia a lamazakehalisi zikiwemo zakificho . Ak izungumziana mnaya kutamb uanoti hal alizashil ingi500, 2,000,5,0 00na10 ,0 00,alis emazinaala maya kif icho ambayounaw ezakuit ambuakwak uipapasa kuangal iakwe nyemwanganakwambaal amahizo kwenye n oti bandia hazip ona walanoti hizo hazinauboraun aotakiwa . Ndesingoaliit ahadharisha jamii kuwa makini paleinapofanyam alipoya n otimpyakwa kuc hungu zakwama kini al amah izokablaya haija pelek wak wa matumi hiyokwamtu mwingine.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:40 PM PDT Na Queen Lema, Meru HALMASHAURI ya Meru mkoani Arusha imeingia katika kashfa baada ya kutoa zabuni kwa mkandarasi ambaye hana ofisi wala makazi maalumu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika baadhi ya vijiji hali ambayo imesababisha halmashauri hiyo kushindwa utoa huduma bora ya maji kwa wananchi. Hayo yamebainika mara baada ya Naibu Waziri wa Maji, Binilith Mahenge baada ya kutembelea baadhi ya miradi ambayo ipo chini ya halmashauri ambapo inadaiwa kuwa halmashauri hiyo ni moja ya halmashauri yenye vyanzo vingi vya maji lakini haina maji. Akisoma taarifa hiyo Mhandisi wa Maji wilaya hiyo, Maningo Mohamed alidai kuwa kwa kipindi cha mwaka 2010 mpaka Aprili mwaka jana mkandarasi kutoka katika Kampuni ya Free World Co. Ltd aliingia mkataba na halmashauri hiyo kwa malengo ya kufanya kazi lakini hakuweza kufanya kazi hiyo na badala yake alikuwa anatoa visingizio vikiwemo vya kucheleweshewa bajeti ya Serikali kwenye sekta ya maji. Mhandisi Mohamed alidai kuwa mara baada ya kupewa mkataba mkandarasi huyo aliisumbua halmashauri kwa kuwa hakuwa na vifaa lakini pia hata ofi si hali ambayo iliendelea kukwamisha miradi ya maji katika wilaya hiyo hivyo kusababisha madhara makubwa ya uhaba wa maji. "Hi i k amp u n i i l i p ewa mkataba lakini kwa bahati mbaya walidanganya kuwa wana ofi si baada ya kuwafuatilia kwa undani tuliweza kujua na kutambua kuwa hana uwezo lakini tulishindwa kumuondoa kutokana na sheria juu ya wakandarasi zinavyobana,"aliongeza mhandisi huyo. Akiongelea uhaba wa maji katika wilaya hiyo alidai kuwa linaendelea kukua kwani kwa sasa lita zinazohitajika ni lita za ujazo elfu kumi na tano mia tano wakati zinazozalishwa ni lita elfu sita tu kwa siku jambo ambalo linasababisha uhaba mkubwa wa maji. Mhandisi Mohamed alibainisha kuwa uhaba huo wa maji unasababisha madhara makubwa kwani wananchi wa wilaya hiyo wanalazimika kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta maji huku shughuli za kila siku zikiwa zinakwama. Awali Naibu Waziri wa Maji, Dkt. Mahenge alidai kuwa suala la mkandarasi ambaye hana ofi si wala vifaa ni la kuhuzunisha kwani huo ni uzembe wa baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo kushindwa kuwakagu wakandarasi kabla ya kuwapa mikataba ya kazi. Dkt. Mahenge alisema kuwa suala hilo linatakiwa kuwa la kwanza na la mwisho na uongozi wa Halmashauri unatakiwa kuomba hata msaada kwa makandarasi wakorofi kwani wanasababisha hata miradi ya halmashauri ikiwemo maji kukwama. Aliwataka hata viongozi wa Halmashauri nao kuhakikisha kuwa wanatafuta mbinu mbalimbali za kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maji kwani huduma ya maji iliyopo bado haiwatoshelezi kabisa wananchi ingawaje wilaya hiyo ni moja ya wilaya hapa nchini yenye vyanzo vya kutosha vya maji.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:42 PM PDT Na Veronica Modest, Musoma MOJA ya changamoto inayosababisha Mkoa wa Mara kuendelea kuwa kinara sugu wa ugonjwa wa malaria ni kutokana na wananchi kuwa na imani potofu juu ya matumizi ya dawa za malaria pamoja na matumizi mabaya ya vyandarua wakati wa kulala. Wakichangia hoja ya namna ya kudhibiti ugonjwa huo katika Mkoa wa Mara juzi katika kikao cha wadau wa malaria wadau hao walisema kuwa kuna kila sababu ya kutafuta njia sahihi ya kupambana na ugonjwa huo kwani Mkoa wa Mara umeonekana kuwa tatizo kubwa. Akiwasilisha mada yake mbele ya wadau hao Mratibu wa kampeni ya unyunyiziaji wa dawa ya kutoka nyumbani, Yusufu Mwita alisema kuwa mkoa umezidi kuwa kinara wa ugonjwa huo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na wananchi kuwa na imani potofu juu ya dawa za malaria pamoja na elimu duni. Alizitaja sababu za mikoa mingine kufanikisha kampeni hiyo kuwa ni pamoja na mwitikio mzuri wa matumizi mazuri ya tiba sahihi ya dawa za malaria,matumizi ya vyandarua wakati wa kulala na ushirikiano mzuri wa wananchi katika zoezi zima la unyunyiziaji wa dawa ya ukoka majumbani. Mwita alisema kuwa Mkoa wa Mara unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizo ya ugonjwa huo kwa asilimia 25.6 mwaka 2012 na asilimia 30.5 kutoka mwaka 2007 huku Mkoa wa Kagera ukipunguza maambukizo hayo kwa asilimia 8.5 mwaka 2012 na asilimia 41.2 kutoka mwaka 2007. Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa alisema kuwa licha ya juhudi mbalimbali za wadau na taasisi mbalimbali kujitokeza katika kupambana na ugonjwa wa malaria lakini juhudi hizo hazionekani kuleta maendeleo kama mikoa mingine inavyoleta mabadiliko katika kupunguza tatizo hilo. Tuppa alisema kuwa umefika wakati sasa malaria itangazwe kuwa ni tatizo kwa mkoa wa Mara hivyo liboreshwe kwa kila wilaya kukaa na kujadili ili kuhakikisha wanatoka na mpango mkakati wa kupambana na ugonjwa wa malaria. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewelle alisema kuwa moja ya mambo yanayosababisha ugonjwa huo kuendelea kuwa sugu katika mkoa wa Mara ni pamoja na uchafu kwa kuwa watu waliowengi hawazingatii suala la usafi wa mazingira katika maeneo yanayozunguka makazi yao. Aidha Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Elias Goroi alisema kuwa ili kufanikisha kazi hiyo ni lazima ushirikishwaji wa wadau pamoja na wahusika wa maeneo uwepo katika kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo husika hali ambayo itasaidia katika kumwondoa hofu mwananchi wa kawaida na hivyo kazi hiyo kukamili |
Posted: 14 Aug 2013 09:44 PM PDT Na Esther Macha, Mbeya WANANCHI wa Kata ya Mshewe Kijiji cha Njelenje Wilaya ya Mbeya wamelalamikia kukosekana kwa maji kwa muda wa miaka 10 licha ya uongozi wa kata hiyo kuendelea kuwachangisha michango ya mabomba wananchi hao Walisema ni jambo la kusikitisha kuona uongozi uliopo unafanya kazi ya kuchangisha michango tangu mwaka 2009 mpaka sasa na dalili za kuwepo maji hakuna na hata kusomewa mapato na matumizi ya fedha hizo hayapo. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umebaini kuwa maji ambayo wanatumia wananchi wa kijiji hicho ni yale ambayo yanatoka kwenye chanzo ambacho ni makaburi ya watu ambayo hata hivvyo hayana usalama wowote ambapo gazeti hili lilibaini kuwa maji hayo ambayo yapo kwenye chemchem. Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Njelenje, Rashid Odati alisema kuwa toka wameanza kuchangia maji ni muda mrefu, kwani maji yaliyopo ambayo wanatumia ni hatari kwa afya za wananchi kutokana na maji wanayotumia kutoka kwenye chanzo ambacho kipo karibu na vyoo na makaburi ya watu. "Hapa tulipo hatuelewi hatma yetu ni nini kwani maji tunayotumia ni hatari sana kwa afya zetu hebu ndugu mwandishi wa habari angalia hicho chanzo kipo kati kati ya makaburi kwa hali hii sidhani kama kuna uhakika wa sisi wananchi kupata maradhi," alisema mkazi huyo. Akizungumzia kuhusu viongozi alisema wamekuwa na sababu nyingi za kutoa kwa wananchi ambazo hazina umuhimu wowote kutoka kwa wananchi kwani fedha ambazo zinachangwa na zimekuwa kama mtaji kwao wa kuendeshea maisha yao. "Mfano huyu diwani wetu† amekuwa na amri zake kwa wananchi kwa kutumia cheo chake kukandamiza wananchi , sisi hatutaki diwani awe mwiba kwetu kwa kutumia† nafasi yake kama fimbo kwa wananchi," alisema Odati. Mkazi mwingine, Teddy Mwakaje alisema kutokana na shida ya maji hakuna maendeleo yeyote ambayo wanafanya kutokana na muda mwingi kutumia kutafuta maji kwani hata yaliyopo kwenye chazo nayoi bado ni tatizo kuyapata licha ya kutokuwa na usalama wa kutosha. Akizungumzia tatizo hilo la maji Mwenyekiti wa kitongoji cha Kizota, John Kapange alisema kuwa kero hiyo ya maji ni ya muda mrefu katika kijiji hicho na kusababisha wananchi kutoka usiku wa manane kwenda kutafuta maji kwenye visima. Akijibu malalamiko hayo ya wananchi Diwani wa Kata ya Mshewe, Fabian Mwakasole alisema tatizo hilo la maji katika Kijiji cha Njelenje ni la muda mrefu na kwamba toka anaingia madarakani mwaka 2010 amelikuta.
 |
Posted: 14 Aug 2013 09:46 PM PDT Na Florah Temba, Moshi KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi mk o a n i Ki l ima n j a r o , wamelazimika kutumia mifuko ya plastiki (malboro) kujikinga na maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwi, huku wengine wakichangia kondomu, jambo ambalo ni hatari na linaelezewa kuwa moja ya chanzo cha ongezeko la maambukizo mapya ya ugonjwa huo mkoani humo . Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwikatika Mkoa wa Kilimanjaro, kimepanda kutoka asilimia 1.9 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 3.8 mwaka 2011/2012. Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali, linalojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwimkoani Kilimanjaro (KACA) Faraji Swai alisema wananchi wa maeneo ya vijijini wako hatarini zaidi kupata maambukizo ya ugonjwa ya ukimwikutokana na kwamba wengi bado hawajafikiwa. Alisema Shirika la Kacakatika utoaji elimu ya mapambano dhidi ya Ukimwikwa jamii, wamefika katika baadhi ya vijiji mkoani Kilimanjaro na kuwakuta wananchi wakitumia mifuko ya plastiki (malboro) kama kinga ya kujikinga na maambukizo ya Ukimwihuku wengine wakichangia kondomu jambo ambalo liliwashangaza. Alisema vijiji ambavyo walikuta wananchi wakitumia malboro kujikinga na Ukimwina kuchangia kondomu ni pamoja na Kahe, Mikocheni, Newland na TPC vyote vya Wilaya ya Moshi, huku baadhi ya mitaa katika Kata ya Njoro Manispaa ya Moshi wakikutwa nao wakichangia kondomu moja zaidi ya mtu mmoja. "Ni jambo la kushangaza kwani yapo maeneo katika Mkoa huu wa Kilimanjaro ambayo tumefika kutoa elimu ya kujikinga na maambukizo ya Ukimwina wananchi kutueleza kuwa wao hutumia malboro kama kondomu kujikinga na ugonjwa huo huku wengine wakifua kondomu mara baada ya kutumia ili kutumia tena wakati mwingine au kumpa mwenzake naye ajikinge, kwa kweli hii ni hatari sana," alisema Swai. Alisema maeneo ya mjini kondomu zimekuwa zikizagaa kwa kukosa watumiaji lakini yapo maeneo ya vijijini yenye uhitaji mkubwa na hayajafikiwa jambo ambalo limesababisha kasi ya ukimwikatika maeneo hayo kuzidi kukua. Alisema maeneo mengine ambayo yameonekana kuwa na kasi ya maambukizo ya Ukimwina yanauhitaji mkubwa wa kondomu ni Kibosho, Mwika na Marangu Mtoni hivyo kunahitajika jitihada za makusudi za kuwanusuru wananchi wa maeneo hayo. Swai aliongeza kuwa zipo sababu nyingi ambazo zinachangia kasi ya maambukizo mapya ya Ukimwiambapo ni pamoja na umaskini wa kupindukia ambao huwafanya wasichana wengi hususan wa vyuo vikuu kujiingiza kwenye biashara ya kuuza miili. Alisema sababu nyingine ni baadhi ya watu ambao wameshajitambua kupata maambukizo ya Ukimwikuueneza kwa makusudi, ulevi wa kupindukia, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya na hivyo kujiingiza kwenye biashara za ngono. "Kwa sasa wananchi wengi hawaogopi tena Ukimwi, wanaona ni hali ya kawaida lakini sisi kama shirika tumekuwa tukijitahidi kutoa elimu hasa kwa vijana kwani kama hatutakuwa makini tutaipoteza nguvu kazi ya taifa hapo baadaye," alisema. "Sheria ya Ukimwiinasema mtu ambaye atabainika kuambukiza ugonjwa huo kwa makusudi ashtakiwe, sasa tunaomba ifanye kazi na Serikali iweke mkazo katika hili, ihakikishe wale wote watakaobainika kukiuka sheria hii wanachukuliwa hatua kali za kisheria," alisema. Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, akizungumzia ongezeko la maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwikwa mkoa huo, alisema imeonekana kupanda mara dufu, hivyo kuwataka wananchi mkoani humo kubadili tabia na kuepuka ngono zembe.
 |
Posted: 14 Aug 2013 09:49 PM PDT Na Rehema Mohamed MAHA KAMAyaHakimuMk azi Kisutuimemtia ha tiani wak alawampiraw amiguuwaFCL umpopokutok an chini Ko ng oIsmail Banduk a, baada yakukir i k utendamakosamatatul ikiw emolakuishi nchini bila yak ibali.Wakalah uy oalikuja nchini kwa ajili yak ufanyamaz ungumzonakipawa zamani waSimba Ju ma Kasejailiakaichezee timu ya FC Lupopo ya Kongo .Wakalahuyoj anaa lif ikishwa mahakama ni hapo mbe leyaHakimuHellenLiwa,a mbap ow akili waserikali kutoka Idaray aUhamiaji PatrickN gayomela alimsomea mashtak ayake.Akisomama shta kaha yo, Ngayomela al idaikuwakat ikakosala kwan zaBanduk aana daiwakuwa Agosti7, mwakah uukatika eneolaM agomeniKond oaakiw araiawa Kongo ali kutwaak iishinc hini bila yaki bali. Katik ashtaka la pili ilidaiwa kuwa, mshtakiwahu yoalimdang anyaofisauhamiaji w amp aka waTund uma kwamba anaing ianc hinikwaajili ya matembezihu kuaki jua k uwaana ingiakama wakala wa mpira wamiguu . Il i daiwakati kash takala tatutarehe hiyohiy o,alikut waaki jihusis hana kaz iyauw akala wampirawa miguub ila yakuwanakibali .B aadaya kusomewa mashtaka hayo, m shtakiwahuyoalikiri kutendamakosa hayo na ma hakamailimtia ha tian i. Kablayakusomewa adhabu, Hakim uLiwaal imtakaBanduka aililiema hakam aili isimp e adhabukubwa ambap oaliomba apeweadhabundogokw asababuhakuwa anajuashe riazauham iaji nch ini.Alise makuw a yeyealiingianchini kw a kutu mi akibali chaShi rikisholaMpirawaM iguuD uni ani(FIFA) ambachokinamruhusu kufanya kazi duniani k ote. "Naombamsamah a, s itarudiakufanya kosa hili tena,sikunyingine niki jaTanzan ianitaombakibali hatachabi asharaili niweze ku fanyakazi yangu,"a lidai.Hatahivyo Hakimu Liwa alimuel ezamshta kiwah uy okuwakutojuashe ria siosabab uyaku tenda mak osana k umpaad habu yakif ungochami ezimitat ujelakw akila kosa aukulipa fainiy ash.150,000kwama kosam atat ua liyotenda. Mshtakiwa amelipa faini.  |
Posted: 14 Aug 2013 09:55 PM PDT Na Elizabeth Mayemba HOMA ya pambano la Ngao ya Jamii imezidi kupamba moto, baada ya Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga jana kuingia kambini Makao Makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Kila mwaka bingwa wa ligi kuu ambapo safari hii ni Yanga na mshindi wa pili Azam FC huwa wanacheza mechi hiyo maalum ya kufungua msimu mpya wa ligi kuu. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini inatarajiwa kufanyika Agosti 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza Dar es Salaam jana Msemaji wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto, alisema timu yao tayari imeshaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo huku wachezaji wakiendelea kufanya mazoezi. "Timu yetu imeshaingia kambini hapa Makao Makuu ya klabu yetu na wachezaji wanaendelea na mazoezi kama kawaida kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo ambalo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali," alisema Kizuguto. Alisema kwa upande wao wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mpambano huo na lengo lao ni kuifunga Azam FC na kutwaa taji hilo. Kwa upande wa wapinzani wao Azam FC waliorejea juzi kutoka Afrika Kusini walipoweka kambi ya wiki mbili, wao wapo kwenye klabu yao , Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mchezo huo wa kuashiria kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umeteka hisia za wengi na kila timu inaonekana kupania kushinda ili kuwasha taa za kijani kuelekea mbio za ubingwa. Yanga iliifunga Azam FC katika mechi zote tatu za msimu uliopita. Yanga watakuwa na hasira za kutaka kulipa kisasi kwa timu hiyo ambayo imekuwa ikiwasumbua, lakini safari hii wamepania kuanza kuifunga kuanzia Ngao ya Jamii hadi kwenye ligi kuu. Katika kujiandaa na msimu, Yanga walicheza mechi saba za kirafiki na kushinda tatu, kufungwa moja na sare tatu.Walizifunga Mtibwa Sugar 3-1, SC Villa ya Uganda 4-1 na 3Pillars ya Nigeria 1-0, na kutoa sare ya 1-1 na Express, 2-2 na URA zote za Uganda na 0-0 na Rhino FC mjini Tabora, wakati walifungwa 2-1 na Express ya mjini Shinyanga. Kwa Azam kabla ya kwenda Afrika Kusini walicheza mechi nne na kushinda tatu, 1-0 na kombaini ya JKT, 4-0 na African Lyon na 5-1 Ashanti United. Na ikiwa Afrika Kusini, ilicheza mechi nne na kufungwa tatu na kushinda moja, ilifungwa 3-0 na Kaizer Chiefs, 2-1 na Orlando Pirates na 1-0 na Moroka Swallows, wakati yenyewe ilishinda 1-0 dhidi ya Mamelodi Sundown  |
Posted: 14 Aug 2013 09:52 PM PDT Na Mosi Mrisho TANZAN IAimeingiafainali mzungukowa pili wa mas hindanoyatenisi'F irstLad y' yanayoe ndelea Na irobi ,Ken yaambapokeshoyanafikiatamati.Akizun gumza Dar es Salaam jana,RaiswaCham achaTenisi Tanz ania (TT A),M eth useleMbojoalisem a mash ind anohayoyanaen deleavizurinaTan zania mzunguk ow akw anzailishika nafasi yapi lihu kuKenya ikishikanafasiyak wanza ."Ti mu zetuza Tanzania zinatuwak ilishavizur i hukona wanafanyavizuri katikamashind a nohayonatunatege meawatatuleteaubing wa nchinikwe tu,"alisema Mboja.Mboja aliongeza kuwa katika mzungu komw ingine wa wanawake wenyeum richiniyamiaka 12Tanzania ilipeleka washiriki watatu na mshiriki mmoja aliweza kupita na atashiriki na mchezaji mwingine kutoka Kenya. Al i s ema ms h i r i k i h u y o akifanikiwa kucheza vizuri dhidi ya Mkenya atajiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele  |
Posted: 14 Aug 2013 09:57 PM PDT Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara jana alitangaza wajumbe watakaosimamia mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dkt. Fenella alisema wajumbe wa kamati hiyo itakayokuwa na watu 10 itakuwa na jukumu la kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kamati hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq huku ikiwa na wajumbe wengine kutoka katika sekta mbalimbali nchini. Wajumbe wengine katika kamati hiyo iliyoundwa na Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Waziri Fenella alisema mbio hizo zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne kukiwa na mbio ndefu za kilomita 42, mbio za kati kilomita 21, mbio za kujifurahisha kilomita 5 na mbio fupi ambazo ni maalumu kwa viongozi zikiwa za kilomita 3. "Mbio hizi zina lengo kuu la kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na amani kwa Taifa letu. Tunategemea Watanzania wengi, ikiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, wanafunzi wa ngazi mbalimbali na wananchi kwa ujumla wataungana na kushiriki mbio hizi," alisema. Naye Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema wazo kubwa la kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni kutaka kuwakumbusha Watanzania k u u e n z i umo j a , ama n i , mshikamano ulipo pamoja na uhuru wetu. Mratibu huyo alisema, mpaka sasa wanariadha zaidi ya 300 kutoka nje ya Tanzania wameomba kushiriki mbio hizo za aina yake hapa nchini. "Sisi kama vijana tukaona kuna haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa kudumisha urithi wa amani, mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu zetu," alisema. Melleck alisema mbali na mbio hizo kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha kubwa la burudani litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni mkesha wa kusubiri siku ya Uhuru. Mbali na hayo Waziri Fenella naye alizitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha wanazidhamini mbio hizo kwani zina manufaa makubwa kwa taifa.  |
Posted: 14 Aug 2013 10:01 PM PDT Na Ester Maongezi KAMPUNI ya 'Hall of Sam B and Promotion Companies' wameandaa pambano la ngumi la dunia uzito wa kati (WBF) kati ya bingwa wa bara la Afrika, Francis Cheka na Philly William wa nchini Marekani litakalofanyika Agosti 30, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa pambano hilo, Jay Msangi, alisema kuwa pambano hilo litakuwa ni la raundi 12 na uzito wa kilo 76 pamoja na kusindikizwa na mapambano mengine manne.Msangi alisema mbali na pambano hilo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya Mada Maugo pamoja na Thomas Mashali pambano la raundi 12. Msangi alisema aliamua kuwakutanisha Maugo na Mashali katika pambano la utangulizi ili kuweza kuvunja majigambo kati ya mabondia hao wawili."Unajua Maugo na Mashali kila mmoja anajigamba kuwa yeye ni bondia bora baada ya Cheka, yaani baada ya Cheka kushika nafasi ya kwanza ya ubingwa wa Afrika wa pili ni wao hivyo swali la jibu hilo nani ni nani litapatikana siku hiyo," alisema Msangi Pia kutakuwa na pambano la uzito wa juu kati ya Alphonce Mchumia na Deandre McCole wa Marekani, Ibrahimu Classic wa Tanzania atakipiga na Simba wa Tundani wote wa Tanzania na kutakuwa na pambano kati ya Cosmas Cheka na Allan Kamote. Msangi alisema mpambano huo utukuwa wa kihistoria nchini, hivyo amewataka mashabiki wa mchezo wa ngumi nchini kujitokeza kwa wingi ili kujionea ushindani utakaojitokeza.Viingilio katika pambano hilo litakuwa viti maalum ni sh.150,000, VIP gold 50,000 na 20,000 kwa viti vya kawaida.Tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia keshokutwa huku mgeni rasmi katika pambano hilo atakuwa Frankois Botha bingwa mara mbili wa Dunia  |
0 Comments