[wanabidii] SITTA AOMBA MSAMAHA , AVUNJA KUNDI LAKE, AJIUNGA NA KUNDI LA LOWASA

Sunday, August 25, 2013
SITTA AOMBA MSAMAHA LOWASA, AVUNJA KUNDI LAKE, AJIUNGA NA KUNDI LA LOWASA.

Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), Samuel Sitta, amesema mahasimu wake kisiasa, wameimarisha mkakati wa kumchonganisha na wabunge, wanasiasa wenzake ili kufifisha jitihada zake za kupambana na ufisadi na madawa ya kulevya.

Sitta amesema mahasimu hao ambao wamekuwa wakimkosanisha na mwanasiasa makini ndugu Lowasa, wameanza kutumia baadhi ya vyombo vya habari, kuiaminisha jamii kwamba, anamuita Lowasa fisadi kitu ambacho hajawahi kusema hivyo, Sitta ambaye alipata wasaa wa kuongea na Lowasa hivi karibuni hapa Dodoma pamoja na mambo mengine alimuomba msamaha na kuomba kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kinyanganyiro cha urais 2015.

"Nimebaini kuwa upotoshwaji huo ni sehemu ya mkakati wa kundi la kisiasa ambalo kinara wake anautafuta Urais wa nchi kwa udi na uvumba huku akisema mambo mbali mbali ya kuwasingizie wenzake kwamba watanzania wajihadhari na rais muuza unga, .......sasa nimeamua kuvunja kundi langu na kujiunga na kundi la Lowasa ili kuwa na kundi imara zaidi nikiamini umoja ni ushindi" alisema.

Hata hivyo wakazi wa mjini hapa Dodoma wamekuwa na wasiwasi na tamko hilo la Sitta kwa sababu waziri huyo amekuwa kigeugeu kiasi kwamba hatabiriki na kuaminika kwa chochote anachosema, hivi karibuni alikaririwa na vyombo vya habari huko mwanza wakati akishiriki katika harambae alisema amechangiwa na waziri magufuri lakini baadaye waziri magufuri alikataa kumchangia waziri Sitta, naye mwanachama mmoja wa CCM mjini Arusha ndugu Mwanaisha Mchomvu alisema muungano wa kundi la Sitta na Lowasa itakuwa ndiyo njia pekee ya kunusuru CCM zidi ya chadema ingawa aliona kundi la wassira lina nguvu zaidi ukilinganisha na makundi mengine kama ya Bernard Membe na January Makamba.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments