[wanabidii] MREJESHO WA KIKAO CHA WANAIRAMBA WAISHIO DSM - 03/08/2013

Tuesday, August 06, 2013

MREJESHO WA KIKAO CHA WANAIRAMBA WAISHIO DSM KILICHOFANYIKA TAREHE 03/08/2013.

Utangulizi

Kikao cha wanairamba na mbunge wao lilikuwa ni wazo binafsi( Daniel Manupa)  ambalo lilikua na nia nzuri nay a dhati kabisa ya kujadili maendeleo ya Iramba, ikiwa ni pamoja na kumhoji mbunge wa Iramba magharibi ndugu Mwigulu Nchemba kuhusu maendeleo ya jimbo lake, mikakati gani aliyonayo kwa ajili ya kutatua kero zinazolikabili jimbo lake la Iramba magharibi n.k.

Pia lengo la kikao hiki ilikua ni namna ya kuleta umoja miongoni mwa wanairamba, na kushirikiana katika kuiendeleza Iramba katika Nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, afya, maji, umeme pamoja na miundo mbinu kama barabara kwa maana hiyo kila mwanairamba awe chachu ya mabadiliko katika Nyanja tajwa.

Wanairamba tuungane kuijenga Iramba yetu, umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

.kichuguu.jpgUkiangalia picha hii, hiki ni kichuguu kimejengwa na mchwa, mdudu ambae ukubwa wake hata kidole chako ni kikubwa, lakini kwa kuwa wana umoja na ushirikiano ndio maana umeona kichuguu kimejengeka tena kwa udongo mwingi utadhani ni lori limeumwaga, wito wangu wandugu tushirikiane, tuweke pembeni tofauti zetu za siasa, dini na hata ukabila, tushikamane kuiendeleza Iramba . Baada ya huu utangulizi, naomba nikupatie mrejesho wa yaliyojiri katika kikao cha wanairamba kilichofanyika tarehe 03/08/2013, pale urafiki jijini dar es salaam.

AGENDA ZA KIKAO ZILIKUA KAMA IFUATAVYO

       i.            Kufungua kikao (Daniel Manupa)

     ii.            Ni jinsi gani elimu iboreshwe wilayani Iramba

  iii.            Upatikanaji wa maji kwa ajili ya binadamu na mifugo yao

  iv.            Upatikanaji wa nishati ya umeme katika vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo.

     v.            Uboreshaji wa miundo mbinu (barabara na mawasiliano ikiwemo barabara ya new kiomboi mpaka Ruruma ambayo iligeuka kuwa mto.

  vi.            Ajira kwa Vijana, pamoja na uwezeshwaji kwa Vijana kujiajiri(ujasiriamali)

vii.            Mengineyo yanayohusu maendeleo ya Iramba.

viii.            Maswali ,maoni na ushauri kwa mbunge.

  ix.            Kujibiwa kwa maswali yalioulizwa pamoja na hotuba fupi toka kwa Mbunge ndugu Mwigulu Nchemba.

     x.            Kufunga kikao – Mwenyekiti (Daniel Manupa)

KUFUNGULIWA KWA KIKAO

Mwenyekiti alifungua  kikao saa 10 jioni, kwa kualika uwepo wa Mungu katika kikao kile na kuzungumza machache ikiwa ni pamoja na kuwafahamisha wahudhuriaji kuwa kikao kile hakikuwa cha siasa, kwa hiyo hapakuwa na nafasi ya kuhubiri siasa katika kikao kile. Kikao kilihudhuriwa na watu wapatao 65 wakiwamo.

·        Mwigullu Nchemba (Mb)- Iramba Magharibi

·        Juma Kitilla – Mbunge aliyemwachia Mwigullu

·        Yahaya Nawanda – Mkuu wa Wilaya ya Iramba

·        Waandishi wa habari

·        Wanairamba

kikao.jpg

Hii ni sehemu ya watu waliohudhuria, Mwigulu akielezea mambo aliyoifanyia Iramba mpaka sasa.

 

Agenda 1: Kuboresha elimu wilaya ya Iramba.

Uboreshwaji wa elimu katika wilaya ya Iramba unahitajika kwa kiasi kikubwa sana, mabadiliko yapo kwa kasi ndogo sana, kwa maana hiyo jitihada zinahitajika sana kuboresha elimu katika wilaya ya Iramba, kwa kulingana na takwimu zilizopo sasa hivi wilaya ya Iramba bado ina upungufu mkubwa wa walimu pamoja na vitendea kazi kwa ujumla, lifuatalo ni jedwali linaloonesha  hali halisi ya miuondo mbinu katika wilaya ya Iramba kwa shule za msingi kati ya Mwaka 2010 hadi 2013.

 

S/NO.

MIUNDO MBINU

 

2010

 

% YA

 

2013

 

% YA

MAHITAJI

ILIYOPO

UPUNGUFU

UPUNGUFU

MAHITAJI

ILIYOPO

UPUNGUFU

UPUNGUFU

1

MADAWATI

28,468

22,382

6,086

21.4

23432

21,037

2,395

10.2

2

NYUMBA

1,428

490

938

65.7

2,095

556

1,539

73.5

3

MADARASA

1,898

1124

774

40.8

2,094

1,151

943

45.0

4

VITABU-KIADA

750,654

175,460

575,194

76.6

804,321

227,434

576,887

71.7

5

WALIMU

2,135

1,428

707

33.1

2,234

1,559

675

30.2

Pia  tukiangalia elimu ya sekondari kwa wilaya ya Iramba kuna upungufu mkubwa wa walimu na maabara kwa masomo ya sayansi, takwimu ya walimu waliopo Iramba katika shule za sekondari ni kama ifuatavyo.

IDADI YA WALIMU WILAYA YA IRAMBA 2010 - 2013

 

S/No

 

SHULE

2013

ME

2013

KE

JUMLA

2013

2010

1

TUMAINI S.S

8

7

15

16

2

USHORA S.S

6

3

9

4

3

MTEKENTE S.S

9

1

10

6

4

SHELUI S.S

13

4

17

10

5

KISIRIRI S.S

5

2

7

5

6

KINAMBEU S.S

11

6

17

9

7

KYENGEGE S.S

12

1

13

1

8

MTOA S.S

9

0

9

5

9

KASELYA S.S

10

4

14

6

10

MBELEKESE S.S

9

2

11

5

11

NEW KIOMBOI S.S

5

6

11

4

12

KIZAGA S.S

17

3

20

4

13

MGONGO S.S

5

4

9

5

14

TULYA S.S

7

1

8

2

15

MALAJA S.S

6

0

6

1

16

MUKULU S.S

5

1

6

3

17

NTWIKE S.S

5

3

8

4

18

URUGHU S.S

9

1

10

10

19

KIDARU S.S

5

0

5

3

20

NDAGO S.S

14

1

15

7

21

LULUMBA S.S

21

7

28

14

22

KINAMPANDA S.S

10

2

12

5

 

JUMLA

196

61

257

129

 

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa wilaya ya Iramba ndugu Yahaya Nawanda, ujenzi wa maabara 66 za masomo ya sayansi unaendelea katika shule 22 za wilaya ya Iramba ambapo kila shule itakuwa na maabara tatu, yaani chemistry, biology na physics laboratories , ujenzi wa maabara hizi upo kwenye lenta, pia kuna wadau wameahidi kumsaidia kuleta vifaa vya maabara, kwa maana hiyo kuna jitihada kubwa za kuboresha elimu wilaya ya Iramba japo bado kuna changamoto kubwa sana, ikiwemo walimu, nyumba za walimu, pamoja na vitendea kazi.

Pia kuna ujenzi wa hostel za wavulana na wasichana na  majiko zinaendelea katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Iramba.

WITO: Wanairamba ndio watakaoiboresha elimu ya Iramba kwa kushirikiana na serikali, hivyo ni vyema kama wanairamba wataguswa kuchangia sekta ya elimu kwa wilaya ya Iramba.

PENDEKEZO: Wahitimu wa vyuo wapewe nafasi za kufundisha elimu za chini huku wakisubiria ajira zao rasmi.

Agenda 2. Upatikanaji wa Maji kwa ajili ya binadamu na mifugo yao

Jitihada za kutatua tatizo kubwa la maji zinaendelea, changamoto kubwa ni kwamba sehemu nyingi za wilaya ya Iramba hazijafikiwa na umeme, kwa maana hiyo kufanya upatikanaji wa maji kuwa mgumu, kwa sababu maji yanahitaji mota kusafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine,  lakini hata hivyo mkuu wa wilaya alisema kuwa wanajitahidi, kuna baadhi ya vijiji vinapelekewa maji(visima kumi) kwa sasa, baadhi ya vijiji ni Mgundu, Kisimba,Kizonzo,Ng'ang'uri, Kibaya na Ruruma, n.k hivi ni baadhi ya vijiji ambavyo uchimbaji wa visima umeanza.

Kijiji cha nguvu mali tarehe 10/08/2013 uzinduzi wa visima vya maji utafanyika, pia kyengege na tulya maji nako maji yako mbioni kupatikana, hii ni kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ndugu Yahaya Nawanda.

Changamoto:

ü Upatikanaji wa mota na umeme

Mbunge amedhamiria kutatua tatizo hili la maji mapema iwezekanavyo.

Agenda 3. Umeme

Hakuna asiyefahamu kuwa sehemu nyingi za wilaya ya Iramba hazijafikiwa na umeme, hata vijiji vilivyo karibu kabisa na makao makuu ya wilaya kama vile Mdunku, Kizega na Ruruma havijafikiwa na umeme.

Upatikanaji wa umeme utasaidia mambo mengi sana na utaamsha uchumi kwa kasi, ukizingatia umeme unahitajika karibu katika kila eneo, ikiwemo maji, Biashara, Afya , Elimu na hata mawasiliano pia, kwa kuzingatia hayo kuna ulazima wa kupeleka umeme katika vijiji mbalimbali wilayani Iramba.

Kupitia mpango wa kuwasha umeme vijijini (REA) na mpango wa serikali vitasaidi kuwasha umeme katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya Iramba, kupitia miradi hii baadhi ya vijiji ambavyo umeme uko mbioni kuwashwa  ni maluga, kitukutu, uwanza, kitusha, zinziligi, kaselya, mbelekese, mugundu, mtenkete na new kiomboi.
pia  mkuu wa wilaya anafanya jitihada za kupeleka umeme katika vijiji vya ulugu, tulya, ndulungu na kidaru.

Matarajio:

Fedha zikipatikana maji,umeme na barabara hizi sekta zitafanikiwa sana.
Mpango wa REA na serikali vitasaidia sana upatikanaji wa umeme vijijini.

 

Agenda 4: Barabara

Inafahamika kuwa barabara ni moja ya mambo muhimu sana yanayopelekea kukua kwa uchumi kwa kuwa ni njia moja wapo ya kusafirishia bidhaa mbalimbali, ya kutuwezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, miundo mbinu kwa wilaya ya Iramba kwa baadhi ya sehemu inakera sana, mfano mmojawapo ni barabara ya kiomboi- Ruruma, hii barabara iliharibika sana kiasi cha kugeuka mto, kwa mujibu wa mbunge na mkuu wa wilaya barabara hiyo imeanza kujengwa kwa kiwango cha changarawe, pia barabara ya kidaru imeboreshwa  ipo kwenye hatua nzuri na inapitika sasa sio kama zamani ilivyokua hata taxi haiwezi kupita, pia kuna mpango wa kujenga lami sehemu korofi hasa kwenye mteremko mkali.

Mbunge Mwigulu akijibu swali la Elibahati N. Mpeta alisema, hata hivyo fungu la serikali halitoshi kujenga barabara zote, hivyo yeye anafanya tu ushawishi kupata fedha zinazojenga baadhi ya barabara za ndani ya wilaya.

Pia Mwigulu alisema barabara ya Mtoa imeshajengwa na kuwekewa daraja la chini kwa hivyo inapitika vyema tu.

Barabara ya kuelekea hospitali ya wilaya iliyopo Old kiomboi imesharekebishwa kwa kiwango cha lami na kuunganishwa na barabara kuu inayoelekea wilayani.

Barabara ya kinampanda kutokea kisana ipo kwenye mpango wa kutengenezwa, pia barabara zingine zitaendelea kutengenezwa kadri fedha zitakavyokua zinapatikana.

Agenda 5: Afya

Ubora wa huduma za afya ni muhimu sana katika jamii yeyote ile ikiwemo jamii ya wanairamba, huduma za afya katika wila ya Iramba zinaendelea kuboreshwa kila mara alisema mkuu wa wilaya ndugu Yahaya Nawanda, alisema wameamua kuboresha mchango wa mfuko wa afya wa jamii (CHF) kutoka shilingi 5000/- hadi shilingi 10,000/-kwa Mwaka, alibainisha kuwa huu mfuko unasaidia sana uboreshaji wa huduma ya afya kwa wilaya ya Iramba.

Mkuu wa wilaya aliendelea zaidi na kusema kuwa kuna jumla ya kaya 78,000 katika wilaya ya Iramba, kati ya hizo kaya 48,000 zimejiunga na mfuko wa afya wa jamii yaani CHF, pia kwa sasa kuna ambulance inayozunguka wilaya nzima kufuata wagonjwa wenye uhitaji wa ambulance na kuwahishwa hospitali ya wilaya.

Kuhusu kuchangia afya ndugu Nawanda alisema kiasi hicho cha fedha watu wanaweza kukipata kirahisi endapo watafanya shughuli za ujasiriamali, hivyo kupelekea uboreshwaji wa huduma za afya kupitia mfuko huo kuliko kutegemea zaidi hela za serikali zinazotoka kwa mafungu.

Katika kusaidia wananchi kufanya ujasiriamali, amehimiza sana watu kufanya ufugaji wa kuku kwani yeye mwenyewe anafuga na wanampa faida nzuri tu,pia  mkuu wa wilaya anampango wa kupiga marufuku usafirishwaji wa kuku kiholela kwenda mikoa mingine badala yake ameamua kujenga soko la kuku misigiri ambalo linazinduliwa tarehe 10/08/2013.

Katika kuonesha kuwa sekta ya afya inapiga hatua katika wilaya ya Iramba, ndugu Nawanda alisema kwa sasa kuna MOBILE CLINIC ambayo inawasaidia zaidi kina mama waliopo wilayani Iramba.

Changamoto:

ü Upungufu wa madaktari

ü Ukosefu wa vitendea kazi

ü Upatikanaji wa maji, pia mfumo mzima wa maji taka katika hospitali ya wilaya.

Matarajio: sekta ya afya itazidi kuimarika kadili fedha zinapopatikana, pia wanairamba tujitoe kuchangia uboreshwaji wa huduma za afya tusiiachie serikali peke yake .

Agenda 6: Ajira

Ajira kwa wahitimu wengi nchini imekua ni tatizo kubwa sana, ikiwemo wanairamba , wahimtimu ni wengi zaidi ya ajira zinazotolewa na serikali, kwa hiyo kuna umuhimu wa Vijana kujiajiri wenyewe, lakini watajiajiri vipi kama hawana mtaji wa kuanzisha hata biashara ndogo ndogo?

Changamoto ni nyingi sana katika sekta ya ajira, tatizo hili linabadilika kutoka na ongezeko kubwa la wahitimu na wakati huo huo waliotangulia kuhitimu unakuta hawajapata ajira, kufuatia hilo Mbunge wa Iramba magharibi ndugu Mwigulu Nchemba alitoa mapendekezo yanayoweza kusaidia  kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana wanaohitimu masomo yao vyuoni.

Mapendekezo ni kama ifuatavyo

ü Vijana kuwa attached katika ofisi za serikali hata kama watalipwa nusu mshahara, hii itasaidia kuwajengea uzoefu wa kazi.

ü Vijana wasio na kazi wajikusanye katika kudi linaloweza kusaidiwa kujiendeleza kiuchumi

ü Serikali ipunguze matumizi yasiyokua ya lazima, kwa mfano matumizi makubwa ya mafuta ya magari, allowances na safari zisizo na masilahi kwa taifa, ili hela inayopatikana kutokana na kupunguza kwa matumizi hayo isaidie Vijana kujikwamua kiuchumi kwa kuanzishwa miradi itakayoweza kutoa ajira kwa wingi kwa Vijana.

ü Soko la alizeti, pamba na ufuta liimarishwe, hii itaweza kutoa ajira nzuri kwa Vijana.

ü Uniforms za mashule, jeshi, polisi zitokane na viwanda vya hapa nyumbani hii itasaidia Vijana kupata ajira viwandani na kupunguza tatizo la ajira.

ü Pia ushauri kwa Vijana kama ajira imekua ngumu sana basi wafikirie plan B nayo ni kujiendeleza zaidi kielimu, kuliko kuendelea kusubiri ajira maana anaweza akasubiria zadi ya miaka 5, wakati angelikua anaendelea na masomo angekua amehitimu level ya juu zaidi.

 

Kutokana na hali ya ajira kuwa ngumu, ofisi ya mkuu wa wilaya imeanza kuwakopesha Vijana ili wajiajiri wenyewe, pia ofisi ya mkuu wa wilaya inawatafutia Vijana mashamba kwa ajili ya kilimo.

Kuna kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti mkuu wa wilaya amemshawishi muwekezaji kuwekeza wilayani Iramba ambapo mwekezaji huyo naye ni mkazi wa Iramba, amekubali kujenga kiwanda katika kijiji cha Ndago  ambacho kitatoa ajira kwa Vijana zaidi ya 1,000, pia kuna kiwanda kinajengwa kijiji cha ulemo nacho kitatoa ajira kwa Vijana zaidi ya 40.

Pamoja na hayo pia mkuu wa wilaya ametoa wito kwa wanairamba kurudi Iramba wakawekeze na kuijenga Iramba, maana kuna watu wengi tu wanakipato kizuri lakini wametelekeza kwao, aliongeza kuwa yeye anagawa viwanja kwa yeyote atakaye hitaji awasiliane nae ili apatiwe kiwanja na kujenga katika wilaya ya Iramba.

Aliongeza kuwa sasa hivi viwanja vinagawiwa misigiri, kwa anayehitaji ni vizuri akawahi mapema kununua viwanja hivyo.

 

Pia aliongeza kuwa kwa  sasa ofisi yake inajenga information  center  pale new kiomboi bomani, hii itawezesha Vijana kupata mawasiliano kirahisi ya mtandao ambapo kijana atachangia sh 500 tu kwa saa 1 kutumia mtandao, pia kufanikisha huduma ya photocopy na printing kwa bei nafuu zaidi.

 

alizeti.jpg

 

WITO: Wanairamba tukawekeze Iramba, hii itasaidia kutoa ajira kwa wanairamba wenzetu waliopo nyumbani.

 

 

Maswali na majibu yaliulizwa mengi na yaliweza kujibiwa palepale na wahusika, ambao ni Mbunge wa Iramba magharibi na Mkuu wa wilaya ya Iramba.

 

Pia kuna video ya tukio hilo bado nitawapatia na yenyewe, muone jinsi ilivyokua, asante sana kwa waliohudhuria, waliotoa kero zao, waliotoa ushauri, na wote walioshiriki kwa njia moja ama nyingine.

 

Msisite kuja kama itatokea nimewaalika tena kwenye kikao kingine

Mimi

DANIEL F. MANUPA

+255715854320

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments