MAADILI UTU NA MAENDELEO .
Na Benn Haidari.
Kupotea Kwa Maadili Na Utu katika Jamii zetu,Ina Uhusiano na Maendeleo ?.
Vitendo vya uovu vya kuuana ovyo ovyo,bila ya kujali vina uhusiano na maadili yetu?
Ndugu Salim Khatri,anauliza "Hivyo kupotea kwa maadili na Utu hayana uhusiano wowote na
maendeleo ?.
Nionavyo mimi ni kua Kiini Cha Kujadiliwa kwenye mada hii ni :
(1) Kupotea kwa maadili na Utu. (2) Jee kupotea kwa Maadili na Utu ni sehemu ya Maendeleo ; ama
kupotea huku kwa maadili na utu kuna uhusiano na maendelo?.
Ndugu Salim Khatri anasema hivi " Hivyo kupotea kwa maadili na utu hayana uhusiano wowote na
maendeleo ?.
Kwanza inatubidi kimsingi kuelewana nini fasiri ya neno "Maendeleo = Development ".
Kwa maneno mengine ni kusema "Maendeleo = Ustawi au Kustawisha au endeleza kutoka kwenye hali
kuelekea kwenye hali endelezo la uborejishaji na sio kuharibu na kubomowa .
Huu ndio uhalisi wa maana ya neno "Mandeleo " ni positive interpretation ya neno hili na halina ukinyume
mwingine wowote wa fasiri hiyo.
Kwa hivyo,ikiwa kimsingi tumekubaliana na kufahamu hapo,basi itakuwa ni vigumu kumuelewa ndugu Salim
Khatri,pale anaposema ".... kupotea kwa maadili na utu hayana uhusiano wowote na maendeleo ".
Ukweli ni kua "kupotea ni kwenda kinyume yaani potoshi za kua kinyume na "ustawi = maendeleo " ;
na ndio maana ndugu Namtasha ,akasema kua watu wanapofanya vitendo viovu haina maana kuwa uovu wa
vitendo vyao "..ndio maadili yetu ..." na wala haina maana kua uovu wa vitendo vyao katika jamii ifasirike kua
"....maadili yetu yamepotea ".Kwa kifupi ni kwamba waliopotea ni wao,kwa sababu ya vitendo vyao !!
Na vile vile inabidi kueleweka kwamba ukinyume wa Maadili na Utu hauhusiani na neno Maendelo,bali ni
dhidi ya Maendeleo .Maendeleo ni uboreshaji na ustawishaji.
Kinyume ya Development ni Regressive.
Kwa hivyo ndugu Salim Khatri,kupotea kwa maadili na utu labda ingehusiana na hali ya "Regressive ",na sio
neno "Development" = Maendeleo.
Nitamalizia kwa kusema kua vitendo vya kuuwana ovyo ovyo,rushwa,utapeli ,utovu wa adabu na heshima ,
ukosefu wa Nidhamu na Uadilifu,Unyapara,Uchangu Doa,Ushoga na Usagaji haya yote si Maadili yetu ;
wala kamwe si sehemu ya Maadili Yetu ,na asilan hayana na uhusiano wa aina yeyote na neno Maendeleo.
Maovu niliyoyataja hapo juu NI SILKA NA HULKA ZILIZO HATARISHI NA MAENDELEO NA MAADILI YETU.
Salams
Benn Haidari
Benn Haidari
Klintvägen 16 C 36
22100 Mariehamn
Åland
Suomi-Finland
Author of Modern Zanzibar Cuisine
Tel/Home: +358.18.13665
Mobile: +358.457.3424826
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments