Katika mambo yanayonishangaza ,kuniudhi na kunifadhaisha ni suala la kusikia "ni kwa ufadhili wa... " kwenye mambo yanayohusu ustawi wa Taifa letu. Hivi ni kweli kwa miaka hamsini ya uhuru bado, kupigana na magonjwa, kuimarisha sekta mbalimbali mathalan, kilimo, ufugaji pamoja na elimu. Naomba nieleweke kuwa sikatai misaada ila tunapaswa kujua kuwa misaada inapozidi huua uwezo wetu wa kufikiri ,kuamua na kutenda hivyo tunabaki tegemezi. Wafadhili sio kweli kwamba wanatupenda na kutujali Kama tunavyofikiri, kama kweli wanatupenda wangetuelekeza, namna ya kupata fedha za kugharamia ustawi wa Taifa letu. Napenda kutoa angalizo kwa viongozi wetu kuwa tabia hii inaidhalilisha nchi yetu na watu wake, lakini zaidi inaturudisha utumwani kwa mara nyingine, utumwa ambao utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza. Hembu tujiulize kwa rasilimali tulizonazo iweje tushindwe, ziko nchi zisizo na kitu kabisa au kidogo ikilinganishwa na tulivyonavyo, wao wameweza, wamewezaje? ni swali la kujiuliza na kutufundisha pia kuwa tuache kujidharau na kujirahisisha kiasi hiki.
--Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments