[wanabidii] Ben Wa Saanane - Nimesikitishwa sana na kauli iliyonukuliwa kutolewa na Nape Nnauye(Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM).

Thursday, August 08, 2013

..."Nimesikitishwa sana na kauli iliyonukuliwa kutolewa na Nape Nnauye(Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM)". - (Imeandikwa na Ben Wa Saanane)...

Gazeti la MAWIO la tarehe 8/8/2013 toleo namba 055 ukurasa wa 5 lililikua na kichwa cha habari NAPE NA CCM
'Ni ama Aiue Ama Imuue'
Katika kauli zake nyingi zilizokosa umakini Kwanza kama mwanasiasa Kijana(Namaanisha Muonekano yaani Physical appearance bila kujali weledi wa kifikra) na Pia kama Mwanasiasa msomi mwenye Taaluma ya diplomasia,Taaluma ya Uandishi wa Habari(Kutoka Chuo kikuu cha Acharya maana Syllabus yao naifahamu na ilihusisha somo la saikolojia) na pia kama msomi wa shahada ya uzamili aliyemudu kuandika Tasnifu(Thesis) na ikapitishwa na Maprofesa hakupaswa kutoa kauli hizo ikiwemo kauli hii iliyokera sana, kwamba Wajumbe wa Tume ya Katiba wanaounga mkono serikali 3 ni wazee na wanasubiri kufa.
Hii ni kauli ya kipuuzi kabisa na inadhalilisha taaluma zote nilizotaja hapo juu na weledi anaopaswa kuwa nao.Kauli hii haidhalilishi taaluma tu,bali hata Mwenyekiti wake aambaye ametimiza miaka zaidi ya 60.Kauli hii inawadhalilisha viongozi na wanachama wote wa chama chake na serikali waliovuka umri wa ujana kwa mujibu wa sheria zinazotambulika na vigezo vyote vya kinadharia.Zaidi Kauli hii inatudhalilisha vijana maana hata sisi ipo siku tutakuja kuwa wazee.Sasa kauli hii inaweza kutumika dhidi yetu kwamba tukipewa mamlaka tunaweza kuharibu kama waliopewa ridhaa na vyama vyao bila kujali itikadi wanaweza kuwa na mtazamo wa aina hii.Ni kauli mbaya na ya kibaguzi

Kumbe Kauli ya Kumuita Dr.Slaa Babu ,Haikumaanisha kauli ya kipinzani?Nakumbuka Dr.Slaa aliwaambia Wanachama wa CHASO(Taasisi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni Wafuasi wa CHADEMA) kuwa akiitwa Babu ni heshima kubwa kwake maana uzee unaashiria hekima na busara.Lakini sasa kauli za Nape kumbe zililenga ubaguzi dhidi ya wazee na sio kwa nia njema.Kumbe Nape nnauye anapomtazama Mwenyekiti wake,Katibu mkuu wake,Makamu mwenyekiti wake,waziri mkuu,Makamu Wa Rais,Spika Wa bunge anaona kwamba hao wote wanasubiri kufa?Ni jambo la ajabu kuwa Nape alituhumiwa kushiriki kuasisi CCJ,huku akijua washirika wenzake waliotajwa yaani Mzee Samweli Sitta ni mzee na hivyo anasubiri Kufa pengine yeye akifikiria kuwa atakua na fursa muhimu ya ku-takeover chama cha CCJ?

Kauli hii ni ya kulaaniwa na vijana wote bila kujali itikadi zetu za kidini na kisiasa.Mwanzoni niliposikia kauli hii niliona tweets za MzeeReginald Mengi akitoa ushauri wa busara kwa Nape na kumuonya kuwa
'Yeye(Nape) Sio Mungu'.Mlolongo wa kauli za kukurupuka ulioanishwa leo hasa ule wa kuwapa mafisadi siku 90 za kujivua Gamba,kauli hii dhidi ya wazee name naongeza Kauli ile ya kuwa Wachagga sio watu wa kujichanganya nao(akilenga rhetorics za Ubaguzi dhidi ya CHADEMA ) bila kujali kuwa ndani ya CCM kuna viongozi na pia serikali ya chama chake ina Mawaziri ambao wana asili ya uchagani na ama wameoa au kuolewa na wachagga ni ulimbukeni.
Kijana yeyote katika jamii iliyostaarabika mwenye ujasiri wa kuwatukana wazazi na hata wakwe zake kwamba
'Ni wazee wanaosubiri kufa' anazua maswali mengi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM anapotangaza maneno hayo inamaanisha kuwa anaeneza sera za chama chake kilichounda serikali inayoshindwa kuwalipa wazee wa Afrika Mashariki kwa sababu tu ya dhana na fikra potofu kuwa ni
'Wazee wanaosubiri Kufa Kesho'? Bila shaka kama sio msimamo wa chama chake basi Madaraka aliyopewa ni makubwa sana kwake

Wazee ni tunu inayopaswa kuheshimika.Kupitia Itikadi zetu tujifunze kushinikiza kupitia ujana wetu kuhakikisha vyama vyetu vinatunga sera zinazoheshimu wazee.Kwa kufanya hivi tutakua tumejenga utamaduni na misingi inayoheshimu wazee
Nape Nnauye atoke hadharani sasa kueleza alichomaanisha kuhusu kauli hii na hayo mengine yaliyonukuliwa.Asipofanya hivi,vijana tumuhesabu kama msaliti wa vijana na tujitenge na kauli hii aliyoitoa.Labda pengine msimamo huu ni wa chama chake ambacho naamini kuwa vijana wanaoheshimu wazee hawataiunga mkono
Msomi Mzuri ni Yule anayechagua cha kuongea,Mwanasiasa mzuri ni Yule anayechagua maneno.Kijana mzuri na makini ni Yule anayeheshimu tunu za uzee bila kushinikizwa na itikadi au mazingira yoyote.Binadamu mzuri ni Yule anayeheshimu uhai wa mwenzake.Binadamu mstaarabu ni Yule anayeheshimu mamlaka ya kiroho na pia anayeheshimu katika falsafa ya 'Law of Nature'.

 

Chanzo: https://www.facebook.com/ben.saanane/posts/10201099725988237

--

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments