[wanabidii] Abakwa, atobolewa macho, aingizwa vitu sehemu za siri

Saturday, August 17, 2013
Picture
Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 amekutwa amekufa katika makaburi ya Majengo katika soko la mjini Kahama mkoani Shinyanga huku mwili wake ukiwa ametobolewa macho na kuonesha kupigwa na kitu kizito usoni.

Mwanamke huyo ambaye hajatambulika jina lake wala anakotoka, alikuwa amevaa blauzi nyeusi yenye madoa meupe, viatu vyenye urembo wa rangi ya fedha, ni mnene kiasi, mweusi na mwenye nywele ndefu.

Mwili wa Mwanamke huyo amegunguliwa leo majira ya saa sita mchana baada ya watu waliokuwa wanachimba kaburi kuuona mwili huo pembeni ya eneo hilo na kutoa taarifa kwa Polisi.

Majirani wanaoishi eneo la makaburi hayo wanahisi unyama huo umefanyika usiku wa kuamkia jana huku, baadhi ya akina mama wakikiri kusikia sauti ya mwanamke akipiga yowe katika eneo la mnadani.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku mrakibu msaidizi wa Polisi Aziz Mayunga akitoa wito kwa wananchi kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.

--- wavuti.com haina ujasiri wa kuweka picha za marehemu ila kwa anayetaka kuziona tafadhali bofya  hapa uende mwenyewe kwenye chanzo cha taarifa hii blogu ya Bundala William Kijukuu cha Bibi "KJ" kuzitizama!


Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2cDbK7feR

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments