Na Maggid Mjengwa,
Ndugu zangu,
Tumeona, kuwa pale Addis Ababa, na mbele ya ' Simba wa Yudah'- Mfalme Haile Selassie, Nelson Mandela alitoa hotuba iliyosheheni hoja nzito na iliyowasisimua wajumbe na hata kuwabadili misimamo yao ya awali.
Na hapa ni kipande tu cha maelezo ya hotuba ile;
" Ndio kwanza nimetoka nje ya mipaka ya Afrika Kusini huku miezi kumi iliyopita nikiwa naishi mafichoni kama mtu ninayetafutwa. Nimekuwa mbali na familia yangu na watoto wangu. Nilipolazimishwa kuishi maisha haya, basi, nikafanya tangazo kwa umma , nikiujulisha, kuwa sitaikimbia nchi yangu, bali nitabaki kuendelea na mapambano nikiwa mafichoni, ndani ya ardhi ya nchi yangu. Nilimaanisha nilichosema na nitaheshimu ahadi yangu hiyo." – Nelson Mandela.
Baada ya kauli hiyo iliyomaanisha kuwa Mandela alikuwa tayari kurudi nchini mwake kuendelea na mapambano, basi, ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe. Nelson Mandela akawa amefanikiwa kujenga hoja na kuifanya ANC isafishike na ikubalike.
Baada ya hapo, Mandela akakutana na mtihani wa kumshawishi na kumbadilisha kimsimamo Kenneth Kaunda wa Zambia. Kaunda alikuwa bado akiamini katika njia na labda propaganda za PAC. Endelea na simulizi hii...
Mandela anasimulia juu ya kikao chake na Keneth Kaunda akiwa...http://www.mjengwablog.com/siasa/item/4128-simulizi-za-mzee-madiba-siku-mandela-alipomkabili-kaunda-kwa-hoja.html#.Ue5BNm2CDTo
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments