[wanabidii] JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LITAADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA MKOANI KAGERA

Sunday, July 14, 2013
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
11 Julai, 2013
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaadhimisha siku ya mashujaa kila tarehe 25 Julai, ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana na kushinda vita ya Kagera mwaka 1978/1979.

Maadhimisho hayo  hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu yatafanyika tarehe 25 Julai 2013 katika mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba kwenye makaburi ya mashujaa yaliyopo Kaboya.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Sambamba na mgeni rasmi, watakuwepo viongozi waandamizi wa Serikali, vyombo vya Ulinzi na Usalama, vyama vya siasa, taasisi za dini na taasisi mbalimbali za kiraia.

Vyombo vya habari vinaalikwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo ni muhimu kwa Taifa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764742161

Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments