[wanabidii] CHADEMA KIDEDEA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA

Sunday, July 14, 2013
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeubuka mshindi wa viti vinne vya madiwani katika jiji la Arusha, Uchaguzi huo uliahirishwa mara mbili baada ya kutokuwepo mazingira salama ya kufanya uchaguzi huo katika muda uliopangwa.

Inasemekana kiongozi wa kampeni kwa Upande wa CCM amekimbia jiji la Arusha na sasa anaelekea KIA ili kurudi Dar mara moja baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo. Tunawapongeza sana wananchi wa Mkoa wa Arusha kwa kufanya Uchaguzi kwa amani na utulivu na kwa kuchagua watu na Chama wanachokitaka wao. Aidha, tunaipongeza Serikali na hasa Mkurugenzi SIPORA LIANA kwa kuwa Imara katika kusimamia Uchaguzi huu uliokuwa na vuta nikuvute nyingi.

Tunawapongeza na CHADEMA na hasa Madiwani waliochaguliwa pia Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema kwa kuwa Imara katika uchaguzi huu; tunawataka sasa kuanza kutekeleza ahadi ili kuwa na MATOKEO YANAYOONEKANA

Share this :

Related Posts

0 Comments