Kuna habari zinazohitaji kudhibitishwa kuwa mabasi matano yaliyoondoka mjini Bukoba kuelekea dar Es salaam yametekwa na abilia kufanyiwa vurugu zisizo za kawaida.
kwanza basi lilikuwa likitekwa moja baada ya jingine. Abiria walitakiwa kufungua masanduku yao na watekaji kuchagua wanachotaka. Wanawake wamebakwa. Watu wamepata vipigo.
Eneo yalipotekewa magari inaitwa Mlima wa Simba.
Kuna habari kuwa watekaji kinyume na ilivyozoeleka watekaji kufanya haraka, hawa walikuwa wanafanana waliokazini kana kwamba hawana woga wowote.
Habari nyingine zitakazodhibitiswha baadaye ni kuwa watekaji hawakuwa watanzania. (kwa maana ya lafudhi).
Kama kuna mwenye habari zaidi heri aziweke hapa.
Elisa Muhingo
0 Comments