[Mabadiliko] KUHUSU LUDOVICK RWEZAHURA

Wednesday, July 17, 2013


 Ndugu zangu,

Nami kama wengine nimepokea taarifa za Ludovick kupewa dhamana kuhusiana na kesi inayomkabili.

Nimeona pia jina langu likihusishwa naye kwa namna moja au nyingine kuhusiana na suala la Kibanda. Nilishaamua muda mrefu kukaa kimya kwenye suala hili kwa vile liko kwenye vyombo vya usalama.

Hata hivyo, maelezo yangu kuhusiana na Ludovick na nilivyohusiana naye kwenye kazi zangu na hususan usaidizi wake kwenye  Mjengwablog nilishayatoa kwenye vyombo vya usalama. Nilishafafanua hapa pia. Sina maelezo mapya. Nikiwa nayo najua kwa kuyapeleka. Na hata mwenye maelezo kunihusu mimi juu ya Ludovick  na hata Kibanda naye anaweza kufanya hivyo.

Nilishasitisha usaidizi wa Ludovick kwenye Mjengwablog mara tu tuhuma dhidi yake zilipodhihiri.  Na inaendelea kuwa hivyo hata sasa hadi hapo ukweli utakapodhihiri na tuhuma na kesi dhidi yake zitakapofikia tamati.

 Binafsi namshukuru Mungu kwa kumweka hai Kibanda, kuninusuru mimi na familia yangu na janga kubwa ambalo lingeweza kunitokea mimi , familia yangu na wenye kunihusu. Kwa jambo ambalo sihusiki nalo hata chembe.

 Naamini Mungu ataendelea kunilinda mimi na  familia yangu  kwa yajayo pia.

 Asubuhi Njema.

 Maggid

http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments