Wandugu,
NILIWASILISHA BUNGENI TAARIFA HII NA MAPENDEKEZO KWA NIABA YA ASASI ZA KIRAIA, MEI 29, 2013.
"KWA MWAKA 2009/10 Serikali ilikusanya TShs 4.5 trillioni (US$ 2.8 billioni) ikiwa ni kodi. Kati ya hizi karibu 30% ilitokana na VAT na kodi ya mapato huku malipo ya ushuru (Excise duties) ni 18% na ushuru wa forodha (import duties) ikiwa ni 9%. Makusanyo haya ya kodi na mapato ni 15% tu ya pato ghafi (GDP) na ni chini ya matarajio ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya inayokusanya 19% na ambayo kwenye nchi zilizoendelea hufikia 30%. Pamoja na mafanikio ya kuojngeza ukusanyaji wa kosi na mapato, serikali ilishuhudia hasara ya kutokusanya TShs 1.7 trilioni (US$ 1.07 bilioni). Hii ni takribani 17.6% ya bajeti yote ya nchi.
Iwapo serikali itatekeleza mapendekezo haya, upo uwezekano mkubwa kukusanya:
I. Maeneo Yaliyopo:
· Kutokana na Misamaha/ukwepaji Kodi = 1,658,500,000,000
· Kudhibiti Udanganyifu = 272,800,000,000
· Kuongeza Ufanisi TRA = 708,112,000,000
Jumla Maeneo Yaliyopo = 2,639,412,000,000
II. Maeneo Mapya:
· Dhibiti Misamaha 1% = 1,386,000,000,000
· Pesa – Fasta = 268,800,000,000
· Bandari Dsm = 2,880,000,000,000
Jumla Maeneo Mapya = 4,534,800,000,000
JUMLA YA MAPATO = 7,176,212,000,000
Hii ingefanya mapato ya serikali kwa mwaka 2013/14 kuwa karibu na au ziada ya 14.5 Trilioni. Hii ni 94.6% ya bejeti yake na hivyo kuwa na nakisi ya chini ya 5%."
KUNA HAJA GANI KUANZISHA KODI-KERO ZENYE KUUDHI KANDAMIZI KWA WASIONACHO HUKU MNASHINDWA KUKUSANYA KODI ILIYOWAZI KWA WENYE UWEZO WA KULIPA???
0 Comments