[Mabadiliko] Jana Nilipokea Simu Ya Mbunge Msigwa Kabla Ya Kukamatwa Kwake...

Monday, May 20, 2013

Ndugu zangu,

 

Jana nilielezea tafsiri yangu juu ya kilichotokea Iringa. Nikaweka wazi pia kuwa nilijaribu kumpigia Mbunge Msigwa.   Kwamba simu ililia bila majibu.

 

Muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake na Polisi  Mbunge Msigwa alinipigia simu. Msigwa alishasoma maelezo yangu mtandaoni.  Hata kama kulikuwa na kutofautiana kwa hoja , lakini tuliongea kirafiki kama ilivyo kawaida yetu.

 

 Maana, Msigwa tumefahamiana hata kabla hajawa Mbunge. Na anajua,  kuwa nina misimamo huru hata kama naweza kukosea kama wanadamu wengine. Na juzi hapa kwenye hotuba yake pale Tumaini University alinitolea mfano kwa wanafunzi. Na Msigwa mwenyewe akasema pale Chuo Kikuu, kuwa anapenda kuulizwa maswali magumu na sio wanahabari wanaomwuliza; " Mheshimiwa, unataka tukuulize nini?"

 

 

Na kwenye mazungumzo yetu ya simu, kauli ya Msigwa  iliyonisikitisha sana ni pale aliponiambia;

 

 " Maggid, siwezi kuendelea kuongea, naona jamaa wakekuja kunikamata!"

 

Leo nimefurahi kusikia kuwa ndugu yangu Msigwa  ameachiwa kwa dhamana. Kuwa wakati shauri lake likiwa mahakamani ataweza kujumuika na familia yake na hata kuendelea kufanya kazi yake ya uwakilishi wa wananchi wake.

 

Na bado naamini, kuwa Mbunge Msigwa kwa nafasi yake ya Ubunge, ana majukwaa mengi, ya Kitaifa na  hata Kimataifa, kuzungumzia , mbali ya mambo mengine, suala la WaMachinga wa Iringa na kuitafuta suluhu ya gulio lao la Jumapili walilozuiliwa na Manispaa. Kwa njia ya mazungumzo.

 

Maggid Mjengwa,

 

Iringa

 

0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz

 

 

 

 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments