[wanabidii] SHULE YA MKAPA TAABANI

Wednesday, April 03, 2013
Sekondari kongwe
Ndanda taabani
Na Mwandishi Wetu

WADAU wa elimu nchini waliopitian katika shule kongwe ya Sekondari ya
Ndanda, wilayani Masasi, mkoani Mtwara wameombwa kuisaidia kwa hali na
mali shule hiyo ambayo kwa sasa baadhi ya miundombinu yake iko katika
hali mbaya.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Morega Mongate, Mkuu wa Shule hiyo
iliyoanzishwa Julai mwaka 1928, ikimaanisha kuwa mwaka huu inatimiza
umri wa miaka 85. Na katika kipindi hicho, imebahatika kutoa wasomi
mahiri na watu mashuhuri, akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Benjamin Mkapa.

Mongate alisema kuwa, miongoni mwa matatizo sugu katika shule hiyo ni
pamoja na kukosekana kwa maabara ya uhakika, uchakavu wa mabweni, jiko
na hata maktaba ambayo ina uhaba mkubwa wa vitabu, hasa vya sayansi.

Ingawa ilianza ikiwa na wanafunzi chini ya 200, lakini sasa wakifikia
zaidi ya 1,000 lakini kwa miundombinu ile ile, Mongate ameomba
ushirikiano wa karibu kutoka kwa watu waliosoma, waliowahi kufanya
kazi au kuguswa na matatizo ya elimu nchini kuweza kuinusuru shule
yake.

"Ni matatizo yanayohitaji utatuzi ili kuyafanya mazingira ya kusomea
na hata kulala kuwa rafiki zaidi, lengo likiwa kuinua uwezo wa
kitaalumu kishule kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

"Ndanda ina historia ya kipekee, imetoa watu mashuhuri na wasomi
mahiri, lakini kwa sababu dhamira yetu ni kuendelea kubakiza jina zuri
la Ndanda katika sekta ya elimu, tumeona ni vyema kero zilizopo
zikapatiwa ufumbuzi," alisema Mongate.

Alisema kwa ujumla, kiasi cha sh milioni 135 kinahitajika ili kuipa
shule hadhi inayostahili, ikiwa pamoja na kufanya ukarabati mkubwa wa
mabweni likiwamo la kihistoria alilotumia Rais Mstaafu Mkapa, jiko na
ununuzi wa vifaa vya maabara na pia kuipa uhai maktaba.

"Kwa watakaoguswa wanaweza kuwasiliana nami kwa simu 0766 469 670.
Misaada mingine inaweza kutufikia shuleni au kupitia akaunti ya Mfuko
wa Maendeleo wa Shule ya Sekondari Ndanda yenye namba 7050 1200 175 ya
benki ya NMB, tawi la Masasi," alisema.
Mbali ya Mkapa, wengine waliosoma shule hiyo ni pamoja na Waziri wa
Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia.

Ends

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments