Wakati tunaendelea kutafakari Bajeti ya Mwaka 2013/14, nimekumbuka kitu ambacho napenda kuwashirikisha Viongozi wa Serikali yetu, na wajibu wetu sisi wananchi. Majuzi tu Jengo la Ghorofa lilianguka Dar es Salaam, tukio lilituhuzunisha sana, ingawa ilibainika baadaye kuwa maazimio ya tume iliyowahi kuundwa yalikaliwa na serikali. Kwa sasa nimeshindwa kuelewa. Baada ya ajali hiyo Rais aliwaita wadau mbalimbali vikiwemo vikundi vya Uokoaji, akawahushukuru, kuwatunuku vyeti, wakala vyakula wakatawanyika. Lakini Rais wetu hakusema anasidia vipi vikundi vya Uokoaji. Vikundi vya Uokoaji sio magari ya Zimamoto tu, vifaa vingine vilivyotumika pale vilitoka kwa Wachina wanaojenga daraja la Kigamboni, Vifaa vingine ni toka kwa mradi wa barabara wa magari yaendayo kasi. Hivi kama wasingekuwapo hao, tungeenda kuazima wapi vifaa, na je siku nyingine itakuwaje? Rais wetu na Serikali yetu walipaswa kujua Watanzania kwanza pengine walikuwa hawahitaji shukrani za msosi na vyeti vya makundi. Watanzania tunahitaji kujua vikosi vyetu vya Uokoaji vimewezeshwa vipi ili matukio kama hayo siku nyingine tujitegemee kuliko kutegemea majirani au huruma ya wachina????. Vikosi vya Uokoaji Tanzania katika maana ya Vitendea kazi vina uwezo gani? Vimewezeshwa? Ukitembelea kwenye stoo zao zingine hazina hata sepetu ya kusogeza mchanga kwa njia rahisi inayotumika hata vijijini. |
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments