[wanabidii] SAID ISSA WA ZANZIBAR NI KWETU NAE ASHIKILIWA NA POLISI?

Sunday, April 14, 2013
Jamani, simtakii balaa huyu ndugu yetu Said Issa (bin Isaa), lakini kimya chake hapa ukumbini hasa katika wakati huu wa kamatakamata wa magaidi, wana-uamsho, wavunja makanisa na wavunja misikiti kinanitia wasiwasi sana. Kama Shk Said upo hapa ukumbini tujulie hali nduguzo japokuwa kwa mstari mmoja, au kama mtu yoyote anajua chochote kuhusu huyu Bwana basi atukhabarishe.
Nimetembelea blogu la Zanzibar Ni Kwetu na nimekuta maelezo tu ya vipi unaweza kuleta pesa Tanzania kwa bei nafuu kutoka nje basi, without the usual fiery articles bashing and trashing our Union!
 
//Nkumba.

Share this :

Related Posts

0 Comments