WAZIRI anayeshughulikia Ulinzi wa Tanzania, Shamsi Vuai Nahodha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa MKATABA, hauna maslahi kwa Wazanzibari na lengo lake ni kuvunja umoja na mshikamano wa taifa hilo.
Nahodha alisema hayo jana alipozungumza na wananchi, wakiwemo wanachama wa Chama cha mapinduzi (CCM) Jimbo la Magomeni, Unguja.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kushajiisha maendeleo ya Jimbo la Magomeni. Nahodha ni Mwakilishi wa Mwanakwerekwe, Unguja.
Akifafanua: Nahodha alisema Muungano uliopo sasa umekuwa na tija kwa wananchi wa pande mbili za Tanzania Bara na Zanzibar, licha ya kuwepo kwa kasoro kadhaa.
Nahodha ni Waziri Kiongozi wa zamani wa serikali ya awamu ya sita ya Zanzibar. Alisema pande zote mbili, zipo katika mikakati ya kufanya marekebisho makubwa ya kasoro za Muungano.
Alisema wapo watu wachache wanaoleta chokochoko za kuwepo Muungano wa MKATABA, huku wakijua kwamba mfumo huo, lengo lake ni kuvunja muundo wa Muungano wa serikali mbili:
"Muungano wa MKATABA…hauna tija wala maslahi kwa wananchi wengi…isipokuwa lengo lake ni kudhoofisha na kuuhujumu Muungano," alisema Nahodha.
Alisema faida za Muungano liyopo ambao unafikisha miaka 49 ni kubwa sana, huku watu wa Zanzibar, wananufaika kiuchumi kwa kutumia sehemu moja ya Muungano kuwekeza na kufanya biashara.
Nahodha alisema viongozi vigeugeu ndani ya CCM, kamwe wasipewe nafasi ya kushika uongozi katika Chama hicho.
Nahodha hana mvuto kisiasa kwa Wazanzibari waliyowengi. Alisema CCM inahitaji viongozi imara, watakaokisaidia Chama hicho kushika madaraka ya kuongoza Dola kwa muda mrefu zaidi.
Nao: Mwakilishi wa Magomeni, Salim Awadh na Mbunge, Mohamed Chombo (CCM) waliahidi kuzipatia ufumbuzi kero zinazowakabili wananchi, ikiwemo maji safi na salama.
Awadh alisema kero kubwa ya wananchi wa Magomeni, ni huduma ya maji safi na salama. Alisema itapatiwa ufumbuzi karibuni kutokana na kuanza kwa mradi unaofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika – ADB..
http://mzalendo.net/habari/muungano-wa-mkataba-hauna-maslahi-nahodha.html
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments