Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,134. |
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma. Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili, Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga, Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke. Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA. Katibu huyo amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (Nafasi 10), Afisa Vipimo II – Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II (Nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9, Afisa Mipango Miji daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16), Mhandisi daraja la II - Maji (Nafasi 13), Afisa Misitu daraja la II (Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu Daraja la II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7, Mkadiriaji Ujenzi daraja la II – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II – nafasi 1, Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu Majengo Daraja la II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7, Fundi Sanifu daraja la II (Ujenzi) -Nafasi 26, Mvuvi Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi (Maji) -nafasi 19. Nafasi nyingine zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II – Nafasi 6, Fundi Sanifu daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi Sanifu Daraja la II -Nafasi 6, Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi 7, Fundi Sanifu Daraja II – Ramani – Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la II –Maendeleo ya Jamii– Nafasi 3, Dereva Mitambo Daraja la II– nafasi 1, Mpiga chapa msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi - nafasi 3, Fundi Sanifu Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi Msaidizi– Nafasi 5, Mpokezi–Nafasi 1, Katibu Mahsusi daraja la III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi 100, Dereva Daraja la II – nafasi 178, Msaidizi wa Ofisi– Nafasi 30, Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1, Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II– nafasi 6. Aidha, kada nyingine ni Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) – nafasi 232, Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe daraja la II– nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi na Umeme, Afisa Biashara msaidizi– Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II – Nafasi 1, Mhandisi Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja la II – (nafasi 1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi Mwandamizi Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi Sanifu Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi Sanifu Msaidizi (Umeme) –Nafasi 4, Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi daraja la II -Jiolojia – nafasi 1, Mkufunzi Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II -Ubunifu Mipango Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II- Urasimu Ramani – Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani –Nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu Msaidizi (Ujenzi– nafasi 1), Fundi Sanifu daraja la II -Nafasi 4, Wakufunzi wasaidizi – nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II. Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili ni kwa ajili ya Waajiri walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la nafasi wazi 185 zilizoko katika tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya Taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali. Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013. Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Machi, 2013 Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz au Simu; 255-687624975 |
0 Comments