[wanabidii] Wanawake na Wanaume tunapoamua ‘kujiachia’ na Madhara yake…

Thursday, March 28, 2013
By Asha D. Abinallah 

Msomaji, nimeona vema nishirikiane nawe katika hii hoja ya kujiachia kwa miili yetu katika kufanya mapenzi na wapenzi wetu. Hapa ninaposema kujiachia sina maana kujiachia wakati wa faragha kufurahia tendo… Bali nazungumzia kujiachia kwa bahati mbaya ama makusudi na kutojali ama kuzingatia ni idadi ngapi ya watu unashirikiana nao iwe kwa siku, juma (wiki), mwezi ama hata mwaka.

Suala lililopo hapa (hasa kwa akina mama/dada) wengi hujiweka katika kundi la kutokujiachia ovyo. Kwako msomaji naomba tulia na jitafakari ukiwa mkweli kwa nafsi yako kama upo kundi hili la kujiachia.

Kujiachia kupo tofauti, kuna kujiachia unakuwa na mpenzi mmoja mmoja lakini hadumu zaidi ya miezi mitatu hivyo kukufanya uwe umelala na walau watu 4-6 kwa mwaka (hivo kama ulianza huo mchezo kaika umri wa miaka 17 na upo miaka 25 ina maana umeshawahi lala na wanaume si chini ya 25).  Pia kuna kujiachia kwa kuchanganya wapenzi ama kutoka nje ya mahusiano ya mpenzi/mwenza wako. Huku kutoka kama ni kubadilisha kila siku huko nje ndiyo kujiachia kwenyewe na nafuu huwepo kwa yule ambaye ana-maintain mtu huyo anayetoka naye. Hata hivyo tuangalie sababu ambazo hutufanya tujiachie ni zipi…

Sababu za Wanawake na Wanaume Kujiachia

Kuwa na Mpenzi asiyemridhisha, inaweza tokea mtu ana mtu wake anampenda sana na wapo pamoja kama couple ila hatosheki kabisa wanapokuwa faraghani. Siku za mwanzo atajitahidi kuvumilia, ila inapotokea tayari starehe ya kutaka kufikishwa imemvaa, aweza jikuta akajiachia kwingine.

Kuwa na tamaa ya vitu hivyo kujiachia kwa kuhongwa kama namna ya kupata alicholenga. Hii ilikuwa sana kwa wanawake, ila tokana na kushuka kwa maadili kasi inaongezeka na kwa vijana wa kiume pia. Anaweza kuwa na mpenzi wake ama wapenzi wengi kwa ajili ya kuwa na machimbo tofauti ya kupata pesa ya kujikimu tamaa zake za vitu. Kwa vijana mara nyingi hutolewa na wamama maarufu kama Jimama.

Kuwa desperate sana na kutoweza ishi bila Mpenzi, kila anapoachika mara kishampata mwingine. Kuna kundi la watu hawawezi kabisa kuweka nafasi (gap) kubwa kati ya mpenzi wake ambaye kaachana naye na mpenzi mpya. Hii husababisha mhusika kujikuta yupo katika mahusiano na mtu ambaye hamfai na hivyo kuachika na kutafuta tena. Mwisho wa siku ndani ya mwaka wapenzi siyo chini ya 6.

Kuwa addicted kwa ngono (Hii ni wachache kwa wanawake na wengi wa wanaume) Huyu mtu anataka kufanya ngono mara kwa mara. Inapotokea mtu mpenzi wake hayupo atajitahidi kwa kila namna atafute mbadala ili kujiridhisha.

Kuwa tu na hulka ya Umalaya/Uhuni. Anakuwa kishazoea kuwa na wapenzi wengi… Hawezi kuwa na mpenzi mmoja, hawezi tulia katika mahusiano, kila siku kutafuta sababu za kuwa na mtu zaidi ya mmoja. Na huona kuwa hiyo ni part ya maisha yake na kuwa afanyalo ni sawa.

Ushawishi wa makundi… Inaweza kuwa kama mzaha na wengine wakadhani kuwa mtu mzima huwa na akili yake independent katika maamuzi. Kwa mtazamo wangu, makundi yanachangia sana kwa baadhi ya watu kujenga tabia ya kujiachia na kuona ni sawa hali awali asingeweza thubutu.

Ngono kuwa ndicho chanzo cha kipato cha kila siku, hii ni kwa wale ambao ngono hutumika siyo tu kwa starehe. Ngono huwa ni chanzo cha kipato… Makundi yametofautiana, kuna wale ambao ni wa hali ya juu na huchaji kwa bei za juu na pia kuna wale wa viwango vya chini na viwango vya chini pia wote tegemeana na maeneo wanayopatikana.

Kutojitambua na hivyo kuwa na huruma sana ya kumfanya kutoweza kabisa kukataa akiombwa tunda lake. Hii ni kwa wanawake ambao hawawezi kabisa kusema 'NO'. Hata kama hamtaki huyo mtu yeye humuonea huruma na kuona ni kheri tu akamalizane naye akamsaidie haja zake.

Kuwa na kilevi katika maungo ya watu wawavutiao. Mfano kuna mwanaume akiona mwanamke mwenye makalio makubwa anachanganyikiwa kabisa na hujitahidi kwa kila namna ampate huyo mwanamke. Kama vile baadhi ya wanawake wanavyoweza changanyikiwa kabisa na kifua, sura ama hata sauti ya mwanaume to the extent atajitahidi kwa kila namna kuweka mazingira ya huyo mwanaume amtongoze ili atimize kiu yake.

Kwa wanaume zinaongezeka;

Kuongeza kujiamini (confidence) na Ufahari kuwa yeye ni mwanaume kamili na lijali – Cha kusikitisha hapa ni kuwa siyo wanaume wote ambao wanalala ovyo wana uwezo wa 6/6.  Ila sababu mara nyingi wanawake tumejenga utamaduni wa kujificha hisia za kweli wakati wa tendo, wengi sababu ni wa kupita tu kwa huyu mwanaume humezea tu rohoni kwa uwezo wake mbovu katika uwanja huo wa faragha… Hasa kama ana pesa ndiyo kabisa!

Madhara ya Kujiachia kwa Wanawake na Wanaume pia…

Madhara kwa Ujumla wake – Wanawake madhara ni makubwa zaidi ya wanaume… It is not fair, ila ndiyo ukweli wenyewe! Kwa mwanamke kubadilisha wapenzi mara kwa mara, kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja na ikajulikana wazi, kutoka nje ya ndoa kwa kiasi kikubwa sana humbomolea heshima mbele ya jamii na cha ajabu zaidi kwa wanaume wenyewe! Kitendo kama vile mwanamke kuwa katika kundi la wanaume ambao zaidi ya mmoja wameshawahi lala naye na inatambulika ni wazi kuwa maongezi kila ugeuzapo mgongo huwa siyo mazuri juu yako. 

Maisha yamebadilika sana na tokana pengine na mazingira na kukosekana na wanaume ambao wana sifa ya kuwa wanaume inaweza changia kwa kiasi kikubwa mahusiano kutofanikiwa. Kimsingi inatakiwa umakini, hekima, subira ya kuweza kupata mtu ambaye anakufaa kuwa mtu wako kwa muda mrefu. Ni rahisi kusema na ngumu kutenda lakini inawezekana.

Bahati mbaya saana ni kuwa kuna baadhi ya wadada huona kama mzaha na kuona kuwa kuna viwango (standards) vipo sawa katika kumtazama mwanaume ambaye anabadilisha girlfriends mara kwa mara kama vile yeye ambavyo hubadilisha boyfriends mara kwa mara. Lakini with time hukua na kupevuka akili na kutambua kuwa hailipi…. Ama huamua kujilipua hadi utu uzima kwa kujua kuwa kama damage ishafanyika.

Pamoja na kuwa kunaweza kuwa mwanaume na mwanamke wenye sifa sawa kabisa katika kujiachia katika ngono; reputation ya hao watu katika jamii ni mbili tofauti. Na hata mwanaume akilaumiwa kama amekithiri atalaumiwa siyo kwa kuwa na wanawake wengi, bali kwa kutembea ovyo ovyo hata na wale ambao wanamchafulia tu jina na sifa zake.

Madhara Mengineyo:-

  1. Inaweza leta kutokujiamini kwa mhusika hasa kwa wanawake… Kila mara kujichunguza kasoro alizo nazo na kujiona kana kwamba ana nuksi ya kuachwa mara kwa mara. Na kama ni mzuri hili ndiyo humchanganya kabisa na kuweza kujikuta yupo kwa mganga na hali mchawi ni yeye mwenyewe.
  2. Inaweza leta tafrani kwa wale ambao wamechanganywa watakapo tambua kuwa wamechanganywa. Kuna wengine hupata hasa cha moto, na wengine huponea chupu chupu kudhurika tokana na tabia hizo.
  3. Kuvunjika kwa ndoa. Hii ni mara nyingi mwanaume anapomfumaniya mkewe. Kwa wanawake wengi husamehe makosa ya kusaliti kwa waume/wapenzi zao kwa sababu zozote zile ambazo hubeba wao. Ni mara chache wake huacha waume zao sababu ya wao kuwa na wapenzi nje.
  4. Kuchuja kwa uzuri hasa kwa wanawake… Wadada/mama wengi hupungua uzuri wao hasa nuru katika sura zao.
  5. Kushuka kwa maadili. Wakubwa katika jamii wamekuwa wakichukulia suala la mahusiano kwa wepesi na saa nyingine kutozingatia mazingira na hadhira na kufanya baadhi ya mambo mbele za watoto wadogo wanaokuwa na kuiga tabia za kujihusisha na mapenzi.
  6. Kushuka kwa heshima ya mhusika kwa jamii iliyo mzunguka tokana na matendo yake hayo.
  7. Magonjwa hasa ya zinaa na kuzidi kuongezeka kwa kasi kwa HIV/AIDS.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments