[wanabidii] TAMKO LA KULAANI KITENDO CHA WAZIRI KAGASHEKI KUKATAA KUONGEA NA VIONGOZI WA WANANCHI NGORONGORO

Wednesday, March 27, 2013

TAMKO LA KULAANI KITENDO CHA WAZIRI KAGASHEKI KUKATAA KUONGEA NA VIONGOZI WA WANANCHI NGORONGORO

 

JUWASAWINGO ni umoja wa watu wa Wilaya ya Ngorongoro, waliojitoa kutetea maslahi ya jamii ya wanangorongo ambao wamekuwa pembezoni kimaendeleo kwa miaka mingi. Jukwaa hili huwaunganisha wanangorongoro wenye taaluma mbalimbali kama wanachama. Na wanachama wa Jukwaa hili wanatoka vijiji vyote vya Wilaya Ngorongoro.

 

Kutokana na kuguswa sana na suala zima la Serikali la kutaka kumega kwa mara nyingine ardhi ya wananchi wa Ngorongoro kwa ajili ya uwekezaji. Kwa niaba ya wanajukwaa na wanangorongoro kwa ujumla tunaalani vikali kitendo cha Waziri Kagasheki pamoja na Mkurugenzi wa Mali Asili Dr Songoro kukataa kuongea na viongozi wa wilaya ya Ngorongoro waliotaka kuongea nao kwa pamoja badala ya kuongea na baadhi yao.Waziri pamoja na timu yake alingia katika ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya Ngorongoro kwa lengo linalosemekana kuwasomea tamko la Rais kuhusu kugawa maeneo ya vijiji. Hata hivyo viongozi wa Ngorongoro ili kuruhusu wote washiriki walitaka mkutano huo hufanyikie nje ya Ukumbi. Waziri hakukubali ombi hilo na kutoka ukumbini kwa hasira na kuelekea uwanja wa ndege kupanda ndege na kuondoka na kuwaacha viongozi wote wakiduwaa.

 

(i)   Malengo ya Safari za Waziri wa Maliasili Loliondo

 

Mh Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mara zote alizofika Loliondo, alifika kwa lengo la kutatua migogoro baina ya wawekezaji hasa Otterlo Business Corporation na Thomson Safaris na wananchi wa vijiji ambavyo ardhi yao hutumiwa na wawekezaji hao. Alifika kwanza kabisa kuwasikiliza na kuchukua maoni ya wadau na viongozi wa mila na wa kuchaguliwa na mara ya pili alikuja na wataalamu ili watoe elimu ya Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009. Katika safari yake ya jana (21.03.2013) inasemekana kuwa alifika kuwasilisha tamko la Rais kwamba Serikali imeamua kutenga ardhi kilomita za mraba 1500 kwa ajili ya uhifadhi wa vyazo vya maji, mazalia ya wanyamapori na mapitiio ya wanyamapori. Kwa taarifa za ndani tamko hilo lililenga pia kuhakisha zoezi hilo la kukata eno hiloliwe limekamilka kutengwa kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

 

(ii)  Viongozi na Wanangorongoro Wanataka  Nini

Viongozi na wanajamii wa Wilaya ya Ngorongoro wana kiu na shauku ya kuona Sheria za Nchi zikiwalinda na zikiheshimiwa bila kupindishawa kufuraisha kikundi kiomoja cha watu. Aidha, kwa kuwa ardhi za vijiji vya zinamilikiwa na vijiji kwa mujibu wa sheria za ardhi, Serikali za mitaa na kwa mujibu wa maelewano na Serikali ya Kikoloni ya Waingereza ya kuwaondoa

 

1


Serengeti mwaka 1959. Wanajamii wa wilaya ya Ngorongoro wanataka Serikali ikiri kuwa ardhi ni ya vijiji na haiwezi kupunguzwa bila wananchi wenyewe kuridhia. Pia Wanangorongoro kwa ujumla wao wanataka Serikali iwashukuru na kuwatambua kwa uhifadhi wa maeneo hayo toka enzi za kale na sio kufikiria kuwaondoa kwa awamu nyingine katika maeneo yao.

 

Viongozi na wananchi wanataka Serikali iwasikilize, washirikiane kuhusu uhifadhi wa maliasili na sio kuamua tu kwamba watatenga eneo bila kujali au kutafakari madhara. Mfano eneo hilo likitengwa takriban watu 40,000 watashindwa kumudu maisha yao ya ufugaji na watakuwa maskini. Kwa kawaida ufugaji wa asili ambao ndio unaofanyika kwa asilimia 100 katika Wilaya ya Ngorongoro hutegemea maeneo hayo ambayo Serikali imepanga kumega kwa ajili ya wawekezaji kwa kisingizio kuwa wanahifadhi mazingira.

 

JUWASAWINGO imetambua kuwa kwa miaka mingi sasa, serikali yetu imekuwa na nia ya kutaka kuifanya ardhi ya Wanangorongoro inayozunguka vijiji vinane kuwa sehemu ya TANAPA na kuwaacha wanachi bila ardhi ya kuchungia.Tunaamini kwa dhati kuwa mpango wowote juu ya ardhi hiyo yenye ukubwa wa eneo la 1500 (Ushoroba), uwe unatoka kwa nje ya nchi au ndani, kwa viongozi wa juu, kwa watu binafsi au vikundi vya watu, unapingana na matakwa ya wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro.Na watu hao , hawajui au wameamua kuupuuza ukweli wa mambo juu ya umuhimu na uhali wa wanachi wa Ngorongoro kuendelea kutumia maeneo hayo ambayo ndio kimbilio lao kipindi cha ukame.

 

Miaka ya 1950 wananchi wa Ngongoro waliokuwa wakiishi maeneo ya Serengeti ambao kwa sasa ni Hifadhi ya Taifa walirubuniwa na wakoloni na kuhamishiwa maeneo ya bonde la crater na maeneo ya loliondo.Kwa Mujibu wa wazee wa enzi hizo wananchi wa ngorongoro waliahidiwa hawatabuguziwa tena kutokana na kwamba maeneo yao yameshakuwa finyu zaidi.Waliadiwa watapata maendeleo mengi kwa kupitia mchango utokanao na maliasili. Lakini hali ilivyo sasa ni tofauti kabisa, wanachi wanaendelea kufukuzwa kwenye maeneo yao bila kufahamu watakapokwenda, wananchi wananyimwa kuchunga mifugo kweneye maeneo yao ya malisho ili kutoa fursa kwa baadhi ya watu kuendelea kunufaika na rasilimali walizopewa watanzania na Muumba wao.

 

Wakumbuke kuwa mizania linganifu kati ya haki za kibinadamu na ulinzi wa mazingira imewekwa bayana katika kanuni na mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ambayo hutoa uhuru kwa mataifa husika na wanachi wanaoishi maeneo yao kutumia rasilimali zao kwa uhuru bila madhara yoyote kwa mazingira na bila kukiuka haki za msingi za binadamu. Kwa sasa Wananchi wa Ngorongoro hawana uhakika kama miaka ijayo wataendelea kuwa na maeneo yao ya asili kwani kwa sasa jitihada nyingi za kuwaondoa Wananchi katika maeneo yao kwa kigezo cha kuifadhi mazingira zimekuwa zikiendelea.

 

Asilimia zaidi ya 80 ya ardhi ya Ngorongoro ni ama mbuga, hifadhi au mapito na malisho ya wanyama. Na kwa miaka ming sasa wanyama na mifugo wamekuwa wakila, kunywa na kulala pamoja.Wananchi wa Ngorongoro waliachia ardhi yao ambasyo sasa ni Hifadhi ya Serengeti ili itumike kwa manufaa ya nchi na hivyo kuchangia vyakutosha katika kukuza uchumi wa Taifa. Ni wakati mwafaka sasa na wao waruhusiwe kunufaika na kazi kubwa waliyoifanya pamoja na

 

 

2


uvumilivu mkubwa badala ya kuadhibiwa kwa manufaa ya wachache wanataka kuneemeka na rasilimali zilizotunzwa na Wangorongoro.

 

(iii)   Msimamo wa Wananchi na Viongozi

 

Baada ya waziri kukataa kuongea na viongozi na wawakilishi wa wananchi, waliamua kuwa wataendeleza msimamo wao kuwa hatakubali ardhi yao ichukuliwe na Serikali kwa ajili ya mwekezaji OBC au mwingine yeyote kwa vizingizio vya uhifadhi. Ikiwa Serikali itaamua kwa kutumia mamlaka waliyonayo kutenga na kutwaa ardhi ya vijij, jamii ya wanangorongoro watatumia mbinu zote kuzuia zoezi hilo. Wananchi kupitia viongozi wao ambao ni viongozi wa vijiji na madiwani wameamua kuilinda ardhi yao kwa ajili ya vizazi vijavyo.

 

Jukwaa hili linawapongeza na kuwaunga mkono viongozi wa wananchi wilaya Ngorongoro kwa kwa kutoridhia mpango huo wa uporaji wa ardhi ya wananchi. Umoja huu wa wanangorongoro unaona ni jambo jema kwa Serikali kuacha kufikiria kupunguza ardhi ya wananchi bali wafikirie namna ya kuwashirikisha wananchi hao katika kupanga mikakati ya kutunza rasimali zilozopo katika vijij vyao.

 

Tunawataka viongozi wa serikali wakubali kuwasikiliza viongozi badala ya kuwakimbia kwa kuogopa umoja wao au uwingi wao. Tunawasihi wapenda haki, waandishi wa habari na wapenda haki watuunge mkono katika kupinga kampeni hii mbaya ya kupokonya ardhi za wafugaji na wananchi kwa ujumla.

 

Imetolewa kwenu kwa niaba ya Wanangorongoro na

 

 

Onesmo P Olengurumwa

 

Mwenyekiti Msaidizi JUWASAWINGO

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments