[wanabidii] LAKINI WATU WENGI HAWAJUI

Monday, March 25, 2013

Hii ni kutokana na maneno mengi yanayosemwa katika jamii nyingi duniani,na maneno yenyewe haswa ni Dini,Mila na Utamaduni.


     Maneno hayo matatu ndiyo yanayofanya mjue mwisho mmoja tu,na yote haya yanatokana na jamii kuishi kwa kufuata elimu za kukaririsha(kasuka) na baada ya kukaririshwa huko kukajenga mazoea ambayo yataleta upinzani ktk uhalisia(ukweli/haki inayotoka kwa m/mungu),kwa maana hiyo ukweli utaonekana ni uwongo na uwongo utaonekana ni ukweli.


     Jamii nyingi duniani na hata hapa Tanzania zimeishi hivyo chini ya wasomi wengi waliokariri  (Mashekhe,Maaskofu,Maprofesa,Wanasiasa na Walimu wote kwa ujumla) na hawa wasomi ukariri huo wameupata kutoka kwa watu wale waliowapinga manabii waliokuja na mfumo wa Mungu na miongozo(vitabu) baada ya kukataa ukweli, mfano ktk watu wa Injili ya Isa(Yesu) alipingwa na Mafarisayo na Masadukayo na pia ktk watu wa Taurati ya Musa alipingwa na wachawi na ktk Qur-an aliyokuja nayo Muhammad Mayahudi wengi walimpinga na kuanza kuandika vitabu vya uwongo rejea Qur:5:41 na 2:79 na mfano wa hao wapingaji wa zama hizo za manabii ni kama tulivyowataja hapo juu,leo wapo na tunawaona na tunawategemea ktk miongozo yetu ya dini na maisha kwa ujumla,hivyo wakawatungia miongozo ya uwongo na kuwarithisha hao wasomi hapo juu na ndio matokeo ya uharibifu wa makundi mengi na elimu nyingi za uwongo duniani.


     Hawa wasomi wakawa ndio kioo cha jamii,kwa hivyo wakaiingiza jamii ktk upumbavu wa kumwabudu(kumtumikia)Twahuti(Kaisari) na sheria zake alizotungia watu na huku watu wakitaraji malipo mazuri(pepo) kutoka kwa yule aliyewaweka hapa duniani na hali ya kuwa ni kinyume chake.


     Tukirudi kwenye maana ya maneno yale matatu ufahamu wake ni:


Dini:-Ni mfumo wa maisha ambayo jamii husika inaishi kwa kuufuata(chini ya muongozo wake).


Mila:-Ni utaratibu-kanuni au sheria inayofuatwa na jamii bila kuchanganya taratibu na sheria nyingine yeyote.(kwa maana ukichanganya na sheria nyingine unakuwa umeshirikisha na unaitwa Mshirikina)


Utamaduni:-Ni kielelezo cha kuifuata mila ya jamii husika navyo ni kuanzia mavazi,makazi,namna watu wanavyoishi,mashairi n.k vyote hivi vinaonekana kuwakilisha jamii vinafuata mila Fulani,ukamilifu wa hiyo mila ndio dini yenyewe,huu ndio ukweli usiopingika lakini watu wengi hawajui.


     Kutokana na kuelewa hivyo tujiulize kwa ufupi kutokana na maneno ya kukariri ya kundi la wasomi wetu tuliowaeleza wanavyotuambia kwamba Waafrika hatukuwa na Dini,bali dini tuliletewa na Wazungu na Waarabu,je hii ni kweli? Jibu,sio kweli Waafrika walikuwa na Dini za makabila yao,kwa vile walikuwa na mila na tamaduni zao,kwa hiyo ziliitwa DINI ZA WAZEE WAO na zilikuwa na AMRI(sheria na hukumu) na usimamizi kamili wa watu nao-ni MACHIFU,VIONGOZI WA KOO.


     Kwa hiyo basi walipokuja wazungu nao walileta Dini zao kwa kuvuruga Dini za wazee kwa kuwapiga wazee wetu hata kuwauwa na kuweka Dini zao ambazo dini zao hizi waliziwekea jina lao nyuma ya pazia,swali je,baada ya wazungu kufanikiwa kuweka dini zao nyuma ya pazia ilikuwaje Ukristo na Uislamu ukaingia hapo?


     Kwa hivyo basi Dini yao hiyo ambayo imejificha ndani ya Ukristo na sisi watu tukawakubali na kuzisema mila za wazee wetu ni za kishenzi,katika hatua hii ya mafanikio yao ambayo yaliunda Serikali mbalimbali duniani chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa na zikasimamia dini yao ktk amri zao,tuliwatukuza wazungu(magharibi) na tukamuacha m/mungu pasi na kujua,mafanikio yao yaliendelea kuondoa tamaduni za Dini-Mila za wazee kidogo kidogo kwani tamaduni ina mazoea kuliko Dini-Mila,zimeondolewa hata kufikia leo tumeingia barabara ktk Dini yao,Mila yao na Tamaduni yao bila ya kujua tumeizoea hata kuipigania sisi wenyewe kwa damu zetu na mali zetu huku tukizidi kukandamizwa kubaki humo na kundi lile la wasoni waliokariri elimu zao pasi na wao kujua.


     Katika kuunda Dini yao hiyo kwa lengo la kuabudiwa(kutumikiwa) badala ya kumtumikia m/mungu na sheria zake walishirikisha madhehebu yote ya Ukristo na Uislamu ili watu wasijegundua kuwa wanaabudu kinyume ya wanavyoabudu watu badala ya m/mungu,na ktk kufanya kazi hiyo walishirikisha makundi ya wasomi waliokaririshwa kwa kuwafadhili ili wapoteze watu ktk muelekeo wa kweli ndio maana hata leo watu hawajui kama wanaabudu(wanatumikia) Serikali na dini(mfumo) yake ya DEMOKRASI chini ya muongozo wake wa katiba ya serikali ya Tanzania wakaingizwa ktk misikiti na makanisa na kuambiwa hizo ndizo sehemu anazoabudiwa(anazotumikiwa) m/mungu na huku kundi la wasomi wale tuliowataja likitia nguvu jambo hilo,mfano walivyotia nguvu-mfano Mashekhe na Maaskofu waliwaambia waumini wao wachangie ktk kutoa maoni ya katiba mpya ya serikali ya Tanzania,ilhali wameacha miongozo yao ndani ya vitabu vyao na mfano mwingine wa maneno aliyosema J.K.Nyerere:-alisema nanukuu,Dini-yatuhusu nini,dini itatufaa nini,ukabila utatufaa nini-unataka ukatambike!,haya ni maneno mabaya kabisa mbele ya m/mungu na maneno ya msomi aliyekariri:-rudi kwenye maana halisi ya Dini-Mila-Utamaduni uone maana yake halafu jiulize juu ya kauli hiyo(fikiria sana).


     Lakini watu wamefurahia kauli hiyo ambayo ndio imewatoa watu ktk kumtumikia m/mungu na sheria zake na wakabaki kuitumikia(kuabudu) serikali na dini yake ya DEMOKRASI bila ya kujua,lakini watu wengi hawajui na huku wakijua kuingia kwao misikitini na makanisa ndio wanamuabudu m/mungu na watafutiwa dhambi zao na kutaraji pepo.


     Naombeni muyazingatie maneno haya matatu Dini,Mila na Utamaduni na mfikirie sana ili mzinduke ktk usingizi mzito ambao watu wamelazwa na wajanja hawa Freemasons-Masih dajal-Mpinga kristo kwamba wameuzingira ulimwengu na wakalazimisha sheria za kumuasi m/mungu kwa wanadamu.


     Na ndio maana utaona leo hii watu wanasema kwa nini watanzania wamepoteza maadili na tamaduni zao?hii ni kauli za wale wasiojua lakini hawajui kama hawajui,unauliza utamaduni na maadili ya watanzania yapi?-na wewe ulifurahia neno lile la kuambiwa kwamba tumeondoa ukabila na udini,je?ulifikiria juu ya maneno hayo au ulikuwa kasuku?,inaposemwa maneno haya tumeondoa Dini-Mila-Tamaduni za wazee maana yake-tumeondoa Dini-Mila na Tamaduni za m/mungu na tunafuata Dini-Mila-Tamaduni za Wazungu(wamagharibi).


     Njia sahihi ni ipi? Qur-an 3:85-Na anayetaka Dini(mfumo) isiyokuwa ya Uislamu haitakubaliwa kwake na akhera atakuwa mwenye hasara.


     Nini maana ya Uislamu:-Uislamu ni neno la kiarabu kwa Kiswahili ni kujisalimisha kwa m/mungu,kwa hiyo ukijisalimisha kwake utafuata Dini-Mila-na Tamaduni yake-rejea maana halisi ya maneno hayo matatu.


     Kujisalimisha:-ni kufuata maelekezo yote(Amri) ya yule  anayekutaka ujisalimishe kwake.je-wewe hutaki kujisalimisha kwa m/mungu ili uitwe muislamu,yaani aliyejisalimisha kwa m/mungu-Au-tunataka kujisalimisha kwa Serikali ili tuitwe wanademokrasia twende pabaya(Jahannamu)(tufikirie).


     Huu-Uislamu na Ukristo kimtazamo wa maneno yanayotumika na vitendo vyake upo kinyume na maelekezo ya dini,mila na tamaduni za m/mungu waliokuja nazo manabii wote na vitabu vya m/mungu ambao hao manabii wote hawakuhitilafiana na kauli zao zilikuwa moja-kwamba kumtumikia(kumuabudu) m/mungu na sheria zake na kuacha sheria zote zilizotungwa na watu zisizokuwa za mungu,kwa hiyo hapa tunaona kugawanywa watu ktk haya makundi mawili ya Uislamu na Ukristo na hapa tunaona daraja lililovunjwa baina ya nabii Isa(Yesu) na Muhammad-kukazalishwa makundi haya mawili yenye madhehebu mengi kwa kila kikundi yote yanasema yanaamini mungu mmoja.


     Tunajua dini(mfumo) ya kweli ya mungu ni moja,sheria ya kweli na ya haki ni moja,sasa kwa nini haya makundi mawili yasikae na kutafakari kupitia vitabu vyao kisha waangalie usahihi na ukamilifu wa sheria za m/mungu upo kwenye kitabu kipi ili tukifuate na kiwe muongozo wetu ktk maisha haya ya dunia na tuachane na sheria zilizotungwa na watu ambazo hazina uadilifu ktk maisha ya duniani na kuepukana na kumshirikisha m/mungu ktk sheria zake na kubwa na la hatari zaidi ni kesho akhera kufikia mahali pabaya ndani ya moto wa Jahannamu(m/mungu atuepushie mbali).


     Kwa hiyo tukitaka uadilifu ktk maisha ya kijamii ktk kila nyanja,tukitaka umoja,amani,utulivu,haki,elimu bora,maendeleo,huduma zote muhimu,uadilifu kwa masikini,mafukara,wazee,wasiojiweza kimaumbile(walemavu),wajibu wa wenye mali kwa watu,ujuzi mbalimbali na mengineyo mengi:-yote hayo elimu na maelekezo yake kimaneno na kivitendo yote yamo ndani ya mfumo(dini) wa m/mungu kupitia vitabu vyake na mienendo ya manabii na wema waliopita na ukamilifu wa yote hayo yamo ndani ya kitabu cha Qur-an ni muongozo uliosahihi na uliokamilika ktk kila kitu kinachohitajika kwa walimwengu wote,chini ya wasimamizi-watu waliojisalimisha,wakakubaliana na maelekezo yote ya m/mungu na kuapa kwamba wataitii,wataifuata,wataitangaza,watasimamia kwa uadilifu maamrisho na makatazo ktk sheria ya m/mungu ndani ya Qur-an.


N.B:-


     Sheria isiyokua ya m/mungu haihukumu(haitoi maamuzi sahihi)-juu ya dhambi wala maasi yoyote ila ina halalisha dhambi na maasi yote.

     

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments