Siku moja Panya aliona mtego wa Panya uvunguni mwa kitanda cha Mwanadamu. Akahisi hatari. Panya akamwendea rafikie Kuku/Jogoo na kumwambie. Rafiki maisha yangu ya hatarini maana kuna mtego. Tafadhali nisaidie kuutegua. Jogoo akasema hiyo ni hatari yako mwenyewe. Utajiju. Pole sina nafasi.
Panya akamwendea rafikie mwingine Mbuzi. Mbuzi akasema we, tangu lini nikaingia uvunguni? Panya akasema wewe ni mkubwa unaweza tumia hata fimbo ukategua? Mbuzi akasema nenda zako Bwana. Sina muda huo.
Panya akamwendea Ng'ombe kwa shida yake. Ng'ombe akamcheka akasema mie naweza ponda pomba kitanda na hata hako kamtego. Lakini sitaki. Hatari ni kwako tu. Omba Mungu uwe na umbo kubwa kama mimi. Ndipo utasalimika. Sisi wakubwa hakuna hatari kama yako.
Panya akakwama kila upande.
Katika hali hiyo; nyoka mwenye simu akaingia ndani mwa Mwanadamu akiwinda panya yule yule. Kwa bahati mbaya, akanaswa mkiani kwenye mtego. Akawa anatapatapa. Mwenye nyumba akaja bila kujua akaketi kitandani. Katika kujihami Nyoka akamgonga Mwanadamu. Kwa vile alikuwa na sumu kali mwanadamu akafa pale pale.
Mipango ya maziko ikaanza. Siku ya kwanza walikuja watu wachache. Jogoo akachinjwa. siku ya maziko wakaja watu wengi; Mbuzi akachinjwa. Na siku ya kuondoa Matanga wakaja watu wengi zaidi. Ng'ombe akachinjwa.
Kumbe Panya akaishi na waliokataa kumsaidia wote wakafa.
Swali la kujiuliza, je Jogoo au mbuzi au ng'ombe wangemsaidia rafiki yao Panya wangefikwa na Mauti? Jibu unalo.
Serikali imeambiwa na kila mpenda amani kuwa ifanye kitu. Ina uwezo wa kuondoa matatizo yanayokabili wananchi wake, hususani suala la usalama. Kuna wakorofi wachache na ina uwezo wa kuwathibiti. Serikali aidha inakaa kimya au inadharau.
Nadhani sasa wanangoja nyoka wa sumu. Atawaletea madhara makubwa.
Mwisho wa hadithi.
Kessy
0 Comments