[wanabidii] UKISTAAJABU YA MUSA UTASIKIA YA KAWAMBWA!

Saturday, February 23, 2013
UKISTAAJABU YA MUSA UTASIKIA YA KAWAMBWA!
 
Nasikitishwa sana tena sana na kauli za viongozi wan chi hii.Dr Kawambwa amenukuliwa akijitetea kwamba TATIZO la wanafunzi KUFELI mitihani yao ni kwa sababu MITIHANI HAIKUVUJA! Hivi ni nani anayemuelewa huyu waziri? Waziri mzima kabisa anatoa utetezi wa kitoto kama huu anadhani nani atamuelewa? Utetezi huu unazua maswali mengi sana badala ya majibu:
 
1.      Hivi kumbe KUTOVUJA KWA MITIHANI ni TATIZO?
2.      Ina maana kwamba KUVUJA KWA MITIHANI ni SHERIA ya mitihani ambayo haikutekelezwa na wahusika (wezi wa mitihani) ili kuwafanya watoto wafaulu kama ilivyokuwa imezoeleka?
3.      Je, kuna haja ya kuendelea KUVUJISHA MITIHANI kwa minajili ya  kuwawezesha wanafunzi wafaulu ili mwisho wa siku tusitafute mchawi kwa matokeo mabaya?
4.      Kwa hivyo kumbe wa kulaumiwa ni WAVUJISHA MITIHANI ambao hawakutekeleza wajibu wao sawa sawa hivyo kupelekea wanafunzi wengi kufeli?
 
 
Sijamuelewa huyu waziri hata kidogo. Kama majibu ya hayo maswali hapo juu ni NDIYO basi tunapaswa KUWALAANI WAVUJISHA MITIHANI kwa nguvu zetu zote kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo hivyo kupelekea wanafunzi kutofanya vizuri. Lakini kama majibu ya maswali hayo ni HAPANA, kuna haja ya kuwapima akili mawaziri wetu ili kubaini kama wanafikiri kwa kutumia vichwa au kama wanafikiri kwa kutumia viungo vingine, ikiwemo vile viungo alivyowahi kubainisha Dr Didas Masaburi.
 
Mtu unaweza ukajiuliza hivi hawa wanasiasa maDr, maProf, nk walipata wapi hivi vyeo vya kitaaluma? Hivi huyu DR Kawambaw ni dakatari wa umbwa au ni daktari wa kitu gani? Kama ni dr wa umbwa kwa nini wasimpeleke kliniki ya wanyama kule SUA badala ya kumng'ang'anikiza kumtwisha madaraka ambayo hayawezi?
 
Ni ukweli usiopingika kwamba wizi wa mitihani hautakiwi na ni kinyume cha sheria za mitihani. Lakini anapotokea waziri AKAJITETEA kwamba WATOTO HAWAJAFAULU kwa sababu MITIHANI HAIJAIBIWA, tunapaswa kutafakari mara mbili kama kweli akili zake ni nzima au kama anastahili kwenda milembe kutibiwa.
 
Hata hivyo, pamoja na kutoibwa kwa mitihani, bado kuna watoto wanafaulu kwenda sekondari huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika! Hili la mbumbumbu kufaulu mitihani sio tatizo ila tatizo ni pale wanafunzi wanapofeli kwa sababu mitihani haikuvuja.
 
Mimi nilitegemea angejitetea kwamba wanafunzi wamefeli kwa kuwa wengi wao wameenda sekondari wakiwa hawajui kusoma wala kuandika. Sababu nyingine ambayo angetoa ni kufutwa mitihani ya mchujo ya kidato pili. Wanafunzi wanaenda hadi kidato cha nne bila kuchujwa unategemea nini kwenye mitihani ya mwisho? Kwa ufupi nisema kwamba bado sijamuelwa kabisa huyu waziri. Kama kuna mtu aliyemuelewa naomba anifafanulie nielewe. Nawasilisha.

Share this :

Related Posts

0 Comments