[wanabidii] uchaguzi Lugoba na njaa kali

Friday, February 15, 2013
mchakato wa kuitangaza Chalinze kuwa wilaya umepamba moto huku vijiji na kata vikigawanywa upya na chaguzi zikitarajiwa kufanyika mwezi wa tatu.

hata hivyo maeneo ya vijiji vingi yamekumbwa na njaa kali hivi sasa mahindi yanauzwa debe shilingi 17000 na hayapatikani hasa maeneo ya lugoba.

wakazi wa Lugoba tunatarajia kuwa uchaguzi huu utasababisha tuletewe chakula cha msaada ili tupate nguvu ya kwenda kupiga kura.
jana Jukwaa la habari kupitia shirika lake la kukusanya habari na kusambaza TANIPRESS lilitembelea  vituo kadhaa vya uandikishaji eneo la lugoba na kukuta vikiwa wazi bila watu.

sababu wananchi wa hapa wamegoma kujiandikisha wakidai kuwa njaa imewapiga kwa kipindi kirefu wakiahidiwa kuletewa chakula cha msaada bila kukiona.

uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 3 wala hakuna chama cha siasa zaidi ya CCM kinachopumua maeneo haya kwani kijiji cha Lunga kimeganywa kuwa vijiji viwili kikiongezeka cha Lugoba kata ya Lugoba.

Share this :

Related Posts

0 Comments