[wanabidii] TAHADHARI KUHUSU WATU WANAO FANYA UTAPELI MTANDAONI KWA JINA LA TAASISI YA RAFIKI ELIMU

Thursday, February 28, 2013
TAHADHARI KUHUSU WATU WANAO FANYA UTAPELI MTANDAONI KWA JINA LA TAASISI YA RAFIKI ELIMU.

Uongozi  wa  Taasisi  Ya  RafikiElimu  Foundation  unapenda  kuwahadharisha  wananchi wote  juu  ya  kuibuka  kwa  kundi  la watu  wanaofanya  utapeli  mitandaoni  kwa  kutumia  jina  la  Taasisi  ya  RafikiElimu ( RafikiElimu Foundation.) 

Siku  ya  Ijumaa  ya  leo  tarehe  28  FEBRUARI  2013  mnamo  majira  ya  saa  5  kamili asubuhi, ofisi  yetu  ilitembelewa  na  mwanadada  aliye jitambulisha  kwa  jina  la  HAWA  MUSSA. 

Mwanadada  huyu  baada  ya  kujitambulisha, aliomba  kuonana  na  HUMAN  RESOURCES  MANAGER  wa  Taasisi  ya  RafikiElimu, baada  ya  kumuona alionesha  fomu  aliyopewa  kupitia  mtandaoni  na  watu  waliojitambulisha  kwake  kama  RafikiElimu  Foundation.

Watu  hao  walitoa  tangazo  kupitia  mtandao  wa  ZOOM TANZANIA  wakidai  kuwa  wana wa- link, wahitimu  mbalimbali  wa  vyuo  vikuu    na  taasisi  mbalimbali  zisizokuwa  za  kiserikali  kwa  ajili ya  kufanya  kazi  katika  taasisi  hizo  kama  volunteers.  

Mwanadada  huyu  akaendelea  kueleza  ya  kwamba, baada  ya  kuona  tangazo  hilo  alivutiwa  na  kutuma  maombi  ambapo  walimjibu  kwa  kumpatia  fomu  aliyo takiwa  kuijaza  na  kuirejesha  kwao.  Baada  ya  kujaza  fomu  hiyo, walimtumia  barua  pepe  nyingine  na  kumwambia  kwamba  maombi  yake  yamekubaliwa, kisha  wakamtumia  fomu  na  kumwambia  aijaze, aimbatanishe  na   CV  yake, na  kuwatumia  pesa  kiasi  cha  shilingi  Elfu  Tano  ( TSh. 5,000/=)  kwa  njia  ya  MPESA   kwenda  namba  0763906931  (AMBAYO  MBAYA  ZAIDI,  WAMEISAJILI  KWA  JINA  LA  RAFIKIELIMU). 

Baada  ya  kuwatumia  pesa  hiyo, wakamwambia   aripoti  na  fomu  yake  iliyojazwa na  kuambatanishwa  na  CV kwa  HUMAN  RESOURCES  MANAGER   wa  Taasisi  ya  RafikiElimu  (ambaye  kwenye  barua  hiyo  walimtaja  kama  Mr. ALBERT  EMMANUEL  ) siku  ya  tarehe  28  FEBRUARI  2013  saa  5  kamili  asubuhi.

Sisi  Taasisi ya RafikiElimu tumeshangazwa  sana  na  taarifa  hii kwa  sababu  kwanza,  hatukutoa  tangazo  la  aina  hiyo, lakini  pili  huwa  hatuwatozi  watu  pesa  ili  kuwatafutia   nafasi  za  kujitolea. Tumefadhaishwa  sana. 

Tumebaini  kuwepo  kwa   utapeli unaofanywa  na  watu  kwa  jina  letu,   hivyo  moja  kwa  moja  tumekwenda  kuripoti  tukio  hili  la  uhalifu  katika  kituo  kidogo  cha  polisi  kilichopo  katika   Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam, sehemu  ya  Mlimani  na  kupewa  RB  namba    UD/RB/849/2013  WIZI  KWA  NJIA  YA  MTANDAO. Tumelitazama  tangazo  hilo  katika  mtandao  wa  Zoom Tanzania.  Tangazo  hili lililowekwa  mtandaoni  mnamo siku  ya  tarehe   05 FEBRUARI  2013  lilisomeka  kama  ifuatavyo :
Picture
UDHAIFU  WA  TANGAZO  HILI:

i.  Namba  waliyo  weka  haipo (  IT  DOES NOT  EXIST  )
ii.   Wanasema  " We are looking for Highly motivated individuals to volunteer in differentprivate Organisation... (RafikiElimu  Foundation,  hatushughuliki na  private  organizations bali  NON-GOVERNMENTAL  ORGANIZATIONS).
iii.  Namba  za  simu  walizo  weka, hazipo  kwenye  blogu  yetu.
iv.   Katika  tangazo  lao,  hakuna  link  inayo  onyesha   anuani  ya  blogu  yetu.
v.   Wametoa  tangazo  lao  kwa  lugha  ya  kiingereza, sisi  kama  RafikiElimu  Foundation  hatujawahi  kutoa  tangazo  kwa  lugha  ya  kiingereza.
vi.  Kiingereza  walicho  tumia  ni  kibovu  sana.  
vii.  Anuani  ya  barua  pepe  waliyo  tumia  ni  batili  na  wala  haipo  kwenye  taarifa zetu  za  kwenye  blogu  yetu.   Anwani  ya  barua  pepe  waliyo   tumia  ni  : graduatevolunteer@gmail.com    wakati   anuani  ya  barua  pepe  ya  taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  ni   :  rafikielimutanzania@gmail.com


HATUA  TULIYO  CHUKUA  BAADA  YA  KULIONA  TANGAZO  HILI  NI  KUUFAHAMISHA  UONGOZI  WA  MTANDAO  WA  ZOOM    TANZANIA, KUHUSU  TANGAZO  HILO  LA  KITAPELI  ILI  KUWANUSURU   WANANCHI  WENGINE  ZAIDI   NA  TUNASHUKURU  ZOOM  TANZANIA  WAMEPOKEA  TAARIFA  YETU  NA  KUAHIDI  KULISHUGHULIKIA  TATIZO  HILO  KWA  KULIONDOA  KATIKA  TOVUTI  YAO .

MAELEZO   YA  KWENYE   FOMU   YA  MATAPELI  HAWA
UDHAIFU   WA   FOMU   HII  :

1.  Namba  zao  walizo  zitoa  kwenye  fomu  hizi  za  kitapeli, hazipatikani  muda  wote, wakati  namba  zetu  zinapatikana  muda  wote.
2.   Katika  fomu  yao  ya  kitapeli, hawajaandika  location  ya  ofisi  zilipo, hawajaweka  sanduku  la  barua,  blog  adress   wala  namba  za  simu  zinazo  patikana.
3.   Hakuna  logo.
4.  Hakuna  sahihi.
5. Hakuna  jina
6. Hakuna  muhuri.

Tulipo  jaribu  kuwapigia  kwa  namba  walizo  ziweka  kwenye  mtandao  ambazo  ni  +255 22 524 3785  tukajibiwa  ya  kwamba  namba  hizo  hazipo  (  the  number  your  dialing  are  not existing  ).

Na  tulipo  jaribu  kuwapigia  kwa  namba   0763906931  nazo  zikawa  hazipatikani  muda  wote.

Taasisi  yangu  kwa  kushirikiana  na  jeshi  la  polisi,  tunafanya  msako  mkali  dhidi  ya  mtu  ama  watu  hawa  na  tunaahidi  ya  kwamba  tutawakamata  ndani  ya  muda  ambao  si  mrefu  sana  na  kuwafikisha  kwenye  vyombo  vya  dola.

OMBI:  Kama   na  wewe  ni  miongoni  mwa  walio  tapeliwa  na  watu  hawa, tafadhali  wasiliana  nasi  kwa simu   0782405936  ili  tushirikiane  katika  kuhakikisha  wahalifu  hawa  wanatiwa  mbaroni  na  kufikishwa  katika  vyombo   vya  sheria. 

TAMKO  LETU :  Tunalaani  vikali  kitendo  kilicho  fanywa  na  ama  kinacho fanywa  na  wahalifu  hawa, kwani  mbali  na  kuiba  pesa  za  Watanzania  masikini  kama  wao,  kitendo  hiki  kinachafua  jina  la  Taasisi  yetu  ambayo  inafanya  kazi  zake  kwa  kushirikiana  na  wananchi.


ANGALIZO  KWA  WANAOTAFUTA  KAZI : 
  

i. Unapo  tuma  maombi  ya  kazi  katika  sehemu  yoyote  ile  halafu  ukaambiwa  utume  pesa  ili  kupatiwa  kazi  hiyo, jua  kwamba    huo  ni  utapeli  na  kazi  hiyo  haipo.

ii.  Hakikisha  unazifahamu  ofisi  za     taasisi  hiyo  zilipo  kabla  ya  kuchukua  maamuzi  yoyote  yanayo  husisha  pesa.  

iiii.  Ni  vyema  kufanya  uchunguzi  ili  kujiridhisha  kama  taasisi  hiyo  kweli  ipo.

iv.  Unapoona  tangazo  la kazi, na  kuvutiwa  nalo, jitaidi  kuwapigia  simu  walioweka  tangazo  na  kuwauliza   maswali mawili  matatu kuhusu  kazi  hiyo.  

HATA  HIVYO:  Tunashukuru kuwa mpaka sasa  ni  mtu  mmoja  tu  ndie  aliyeripoti  kutapeliwa  na  watu  hao  kwa  jina  la  Taasisi  yetu.  Hii  ina  maana  kuwa  Watanzania  wengi  wameelimika  kwa  sasa, inawezekana   watu  wengine  walilishitukia  tangazo  hili  na  kuachana  nalo.


Source: http://www.wavuti.com/4/previous/2.html#ixzz2ME6tXd1l

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments