[wanabidii] Taarifa ya Wizara kuhusu upatikanaji wa dawa za kutibu Malaria

Saturday, February 02, 2013
Utangulizi

Kumekuwepo na taarifa kupitia baadhi ya vyombo vya habari kwamba kuna
upungufu mkubwa wa dawa mseto za kutibu malaria aina ya ALU katika
vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.Taarifa hizo zilimnukuu
Mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali la SIKIKA, katika mkutano na
wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika mjini Dar es Salaam hivi
karibuni.

Ufafanuzi

Taarifa alizotoa Mkurugenzi wa SIKIKA, chanzo chake kimetokana na
kunukuu taarifa zinazopatikana kutoka katika mfumo wa kielektroniki wa
wizara ambao unafuatilia takwimu za dawa za malaria katika vituo vya
huduma ujulikanao kama 'SMS for Life'.

Mfumo huu unatoa taarifa za upatikanaji wa dawa za kutibu malaria aina
mbili tu ambazo ni Alu na Quinine, na sio dawa nyingine za kutibu
Malaria.

Hivyo basi, dawa zingine zote pamoja na zile za msaada, ambazo
zinapokelewa na kusambazwa katika hospitali zote nchini hazitolewi
taarifa kwa kutumia mfumo huu wa "SMS for Life". Hivyo kusababisha
wakati mwingine kuonekana hakuna dawa wakati dawa hizo zipo vituoni.

Hali halisi

Dawa za Alu zilizopokelewa mwezi Januari 2013;-
Vidonge vya watoto dozi 2,400,000 ambazo zitatosheleza kwa miezi 5
Vidonge vya watu wazima dozi 5,688,720 zinatosheleza matumizi ya miezi
14

Shehena nyingine za dawa za Alu zinatarajiwa kufika nchini mwezi
Machi, 2013.

Aidha, kufikia tarehe 31 Disemba 2012 kulikuwa na dawa za Alu za
watoto dozi 1,315,967 ambazo zilitosha matumizi ya miezi 2. Vile
vile, kulikuwa na dozi za Alu 2,283,610 za watu wazima ambazo
zinatosha matumizi ya miezi 2 na nusu.

Hitimisho

Wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba kwa sasa kuna dawa za
kutibu malaria vituoni za kutosha. Vile vile, Bohari kuu ya Dawa (MSD)
inaendelea na usambazaji wa dawa hizi katika vituo vyote nchini.
Aidha, taratibu za kuagiza na kuleta shehena zaidi ya dawa za malaria
kutoka nje ya nchi zinaendelea ili kuhakikisha kuwa dawa za kutibu
malaria zinapatikana kwa muda wote.

Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
01/02/2013

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2JkbwoB1Z

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments