[wanabidii] TAARIFA KUHUSU URATIBU NA UZINDUZI WA KANDA YA KASKAZINI

Thursday, February 14, 2013
TAARIFA KWA UMMA

KIKAO CHA KAMATI YA URATIBU WA KANDA NA UZINDUZI WA KANDA YA KASKAZINI

Kufuatia azimio na maamuzi ya Baraza Kuu la CHADEMA lililofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam, iliamuliwa kuwa chama kishushe mamlaka
ya uendeshaji kwenye mfumo wa kanda kama zilivyogawanywa.

Itakumbukwa kuwa azimio hili ni sambamba na sera ya CHADEMA kuhusu
mfumo mpya wa utawala (majimbo) na mapendekezo ya chama kwa tume ya
mabadiliko ya katiba kuhusu kuigawanya nchi katika majimbo 10 ya
kiutawala/kiserikali.

Katika mgawanyo huu, Kanda ya Kaskazini ilipangwa kuwa na mikoa ya
Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Mkoa wa Arusha ulichaguliwa kuwa makao makuu ya Kanda ya Kaskazini.

Tarehe 16 na 17 Februari 2013 kutakuwa na kikao cha kwanza cha Chama
Kanda ya Kaskazini ambacho kitajumuisha wabunge wote kutoka mikoa ya
kanda hii, akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe
(KUB), viongozi wa chama wa mikoa.

Pia kitahudhuriwa na Wenyeviti na Mameya wa halmashauri zinazoongozwa
na CHADEMA pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya chama, wanaoishi kwenye
kanda ya kaskazini pamoja na mwasisi wa CHADEMA Mzee Edwin Mtei.

Aidha siku ya tarehe 17 Februari kikao kitajumuisha viongozi kutoka
majimbo yote ya Kanda ya Kaskazini, takribani majimbo 30 na kuleta
wajumbe zaidi ya 200 katika Jiji la Arusha.

Siku hiyo hiyo ya tarehe 17 Februari tutakuwa na uzinduzi wa kanda
yenyewe na kuitambulisha timu ya uratibu, utakaohitimishwa na mkutano
mkubwa wa hadhara.

Tunawaomba wananchi/wakazi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wajitokeze
kwa wingi sana kwa ajili ya uzinduzi wa kanda yao hii na pia kuunga
mkono mpango huu wa chama ambao mbali ya kukifanya chama na viongozi
kuwa karibu zaidi na wananchi pia katika kufanya shughuli za kisiasa
kwa ufanisi wa hali ya juu na kwa kiasi kikubwa umeshusha madaraka na
mamlaka ya uendeshaji na usimamizi wa chama kwa watu ngazi ya chini.

Imetolewa leo tarehe 13 Februari 2013.
Arusha.

Amani Golugwa
KNY: Kamati ya Muda ya Uratibu
KANDA YA KASKAZINI (TANGA, KILIMANJARO, ARUSHA & MANYARA)
+255 754 912 914
Email: golugwa@gmail.com

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments