na hekima za watanzania kuyafanyia maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi.
Amesema kama wataamua kutenda haki kila mbunge mmoja wa upinzani
atakapochangia bungeni ni vyema ikafuata michango ya wabunge watatu
toka CCM, maana CCM ina robo tatu(3/4) ya wabunge wote. Nimepatwa na
msituko kidogo na kushindwa kuelewa alichokisema. Naomba niulize swali
lifuatalo: hivi kama kuna hoja iliyotolewa, wabunge wa CCM hawaoni
sababu ya kuchangia chochote katika hoja hiyo maana kwao ni "zidumu
fikra za mwenyekiti" wakati huo huo wapinzani wakawa na hoja za
kuuliza au kuboresha wasiruhusiwe kwa sababu ya uwiano na hivyo hoja
hiyo ipite bila kupingwa?
Sina uhakika na taratibu za bunge zinasemaje lakini katika hili
namuona mh. sana kama kasema kitu kinachoweza kulifanya bunge
kushindwa kuwa chombo sahihi kuwawakilisha wananchi. Kuchangia hoja ni
pale ambapo mbuge husika ana jambo la kusema, kama hana basi hana na
hivyo watachangia wenye hoja. Tunawafahamu wabunge wengi haswa wa CCM
ambao muda wote ni watu wa kulala bungeni tu. Kwa mtindo wa Ndugai
itawabidi hata wasio kuwa na hoja yoyote kupoteza muda bure bungeni
alimradi kuleta uwiano anaohuitaji Ndugai. Bunge linagharimu pesa
nyingi ya walalahoi hivyo si vyema kuleta mambo ya kiswahili bungeni.
Watanzania tumekwishaona umuhimu wa wabunge wanaosoma makablasha na
kuweza kugundua vitu vya aibu ndani ya bajeti na mambo mbalimbali
bungeni. Hawa si wabunge wanaotokana na uwiano anaotwambia Ndugai bali
ni wale wanaojitoa kwa wananchi huku wengi wakiwa wachumia tumbo. Kama
utaratibu alioutoa Ndugai ni sahihi basi tumepata somo kwamba wakati
wa uchaguzi ni bora tukawaingiza wabunge wengi wa upinzani kadri
iwezekanavyo ili waweze kutusemea matatizo yetu kwa vile wabunge hao
wachache wameweza kuibua hoja na maswali muhimu kwa ajili ya ustawi wa
taifa letu. NDUGAI UMEFANYA LA MAANA KUTUSTUA KWAMBA KUWAINGIZA
WABUNGE WENGI WA CCM NI KULIDUMAZA BUNGE. ASANTE SANA MHESHIMIWA
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments