[wanabidii] MSHIKE MSHIKE KITUO CHA POLISI NA DALADALA MWENGE

Thursday, February 28, 2013
Kuna Kamata Kamata inaendelea kituo cha daladala mwenge na askari wa
kituo cha polisi mwenge baada ya kutonywa na wasamaria wema kuhusu
baadhi ya watu kupatiwa unifomu za askari jamii wa kituo hicho
kufanyia kazi ambazo sio halali .

Taarifa zaidi zinasema askari hao jamii ambao ni feki wamekuwa
wanajihusisha na vitendo viovu ndani ya kituo cha daladala na maeneo
jirani ya kituo hicho kama kuibia abiria na uhalifu dhidi ya madereva
na wafanyakazi wengine wa daladala .

Kamata kamata hii imesababisha kutuo cha polisi mwenge kuvamiwa na
vijana hawa wanaotuhumiwa kwa ajili ya kushugulikia wenzao ambao
tayari wameshawekwa rumande kwa kukutwa na unifomu au wakifanya kazi
ndani ya kutuo kama askari jamii .

Mpaka sasa hivi hakuna maelewano maana watu wameanza kurushiana maneno
na kutishiana .

Taarifa zaidi zinasema vikundi hivi vya askari jamii vinaendeshwa na
mabaousa ambao ndio wamejipachika uongozi ndani ya vituo mbalimbali
vya daladala mkoani dar es salaam .

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments