(ISLAMIC ASSOCIATION FOR EDUCATION AND ECONOMIC DEVELOPMENT)
MAONI YA UMOJA WA KIISLAMU WA ELIMU, UCHUMI NA MAENDELEO (UKUEM)
KUHUSIANA NA
KATIBA MPYA YA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA
UTANGULIZI
1. UMOJA WA KIISLAMU WA ELIMU, UCHUMI NA MAENDELEO (UKUEM) ni taasisi
ya
kidini isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa rasmi na Mrajisi Mkuu wa
Serikali tarehe 2 Januari, 2002
na kupatiwa hati ya usajili namba 177 ya 2002. UKUEM ina makao yake
makuu hapa Mjini
Zanzibar katika Mtaa wa Kijangwani na inapatikana kwa anuani
zifuatazo:
Makao Makuu ya UKUEM,
Sanduku la Barua 4865,
ZANZIBAR.
Simu: +255 24 223 5546
Fax: +255 24 223 5546
E mail
: info@ukuem-zanzibar.org
Website: http://www.ukuem-zanzibar.org
Kwa Pemba:
Afisi Kuu ya UKUEM,
Sanduku la Barua 3,
Chake Chake,
PEMBA.
Simu: +225 24 245 2230
E-mail: ukuem_ak@yahoo.com
2. UKUEM ikiwa mojawapo ya taasisi za kijamii, inajihisi kuwa ina
wajibu wa msingi wa
kuchangia katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa
Tanzania. Katika kutoa maoni yetu, Kamati Tendaji ya UKUEM imekutana
katika kikao
chake cha kawaida cha tarehe 17 Safar, 1434 (muwafaka na tarehe
30-12-2012) na
kupendekeza mambo yafuatayo:-
1
NENO FUPI KUHUSU MUUNGANO NA CHIMBUKO LA TATIZO
3. Kuwepo kwa Muungano wa Tanzania kumekuwa ni jambo la kupigiwa mfano
kwa
upande mmoja na lenye kutiliwa mashaka kwa upande mwengine kutokana na
kukosekana ushahidi wa kisheria unaothibitisha kuwa umekuja kihalali
kwa mujibu wa Hati
ya Mkataba wa Muungano huo. Masharti ya uhalali wa Muungano huo
yalikuwa ni pamoja
na kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Tanganyika na Baraza la Mapinduzi
la Zanzibar la
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar baada ya kukubaliwa na Marais wa Nchi
mbili (Tanganyika
na Zanzibar). Kuna kumbukumbu za kuridhiwa na Bunge lakini hadi leo
panakosekana
uthibitisho wa kuridhiwa kwa Mkataba huo na Baraza la Mapinduzi la
Zanzibar. Maelezo
ya kuthibitisha madai haya yametolewa na Rais wa Pili wa Zanzibar,
Alhaj Aboud Jumbe
Mwinyi, Mwanasheria wa Kwanza wa Zanzibar baada ya Mapinduzi, Walfang
Dourado na
Katibu Mkuu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi, Salim Rashid.1
4. Hali hii imeusababisha Muungano kuwa na sura ya kutiliwa mashaka na
baadhi ya
watu na wengine kuuchukulia kuwa hauna matatizo kutokana na muda
uliodumu.
Mitazamo hiyo imekuja licha ya kuwepo watu wengi, hususan wale wa
Zanzibar ambao
wameathiriwa na matokeo mbali mbali kufuatia kuhoji kuwepo kwa
Muungano. Ukiwacha
matokeo machache ya kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika kutoka
kwa
Watanganyika, bado Wazanzibari wanabaki kuwa ni majeruhi wa miaka 48
ya kuwepo kwa
Muungano. Wote waliopata joto la kuudadisi Muungano walitokea
Zanzibar. Kutokea Bara,
tumekuwa tukishuhudia jitihada za kuikuza orodha ya mambo ya Muungano
kutoka 11
hadi 22 ya sasa (au 37 kwa uhalisia wake).
5. Kwa uoni wa baadhi ya watu, Muungano ungekuwa hauna dosari kama
pangefanyika
kura ya maoni kwa watu kuuridhia. Uandishi wa katiba mpya unachukuliwa
kuwa ni hatua
ya kuuhalalisha Muungano huo kwa wale ambao wamekuwa na mashaka
kuhusiana na
uhalali wake. Hata hivyo, kwa Wazanzibari, tatizo siyo kuimarisha
Muungano; bali maslahi
ya Zanzibar katika aina yoyote ya Muungano. Uzoefu umetufanya tuone
kuwa muungano
unaotufaa baada ya miaka 48 ni huu tutakaoupendekeza hapa. Aidha kwa
Wazanzibari,
kujua muundo wa Muungano ni jambo muhimu zaidi kuliko nini kiwemo
katika Katiba
ijayo. Madai kuwa Wazanzibari wamepoteza fursa kwa kuzungumzia muundo
wa
Muungano badala ya hadidu za rejea hayaonekani kuwa na msingi wala
mashiko yoyote
ya kimantiki. Hii ni kutokana na kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
inalenga zaidi kulinda
hali iliyopo (status quo) kuliko kutatua matatizo ya msingi yaliyomo
katika Muungano.
1 Kwa maneno yake mwenyewe, Rais Jumbe anasema: "Finally, I had been
in the Revolutionary Council, in
one capacity or another, since its inception in 1964 to January 1984
and I fail to recollect the convening of
such a meeting to the Revolutionary Council, either in Zanzibar or Dar
es Salaam to ratify the Articles of
Union." Uk. 2, The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union 30
Turbulent years, 1994.
2
6. Katika kipindi cha miaka 48 ya Muungano, tume kadhaa zimeundwa,
taarifa kadhaa
zimendikwa, malalamiko lukuki yametolewa yakiwemo yale ya Marais wa
Zanzibar2, vikao
kwa makumi vimefanyika, fedha nyingi zimetumika katika kutatua
matatizo ya Muungano.
Kinachoonekana ni kuwa utatuzi wa tatizo au kero moja ya Muungano
hupelekea kuzaliwa
kero nyengine zaidi ya moja. Matatizo ya Muungano yameanza tokea
mwanzoni mwa
Muungano wenyewe kama anavyothibitisha hivyo Marehemu Babu3. Mifano ya
kero
zilizoebuka na bado zinaendelea kuebuka ni pamoja na:
a.
Uwakilishi wa Zanzibar katika nafasi muhimu za kimaamuzi kama vile
uraisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge, Spika wa Bunge, Wakuu wa
Majeshi
ya Ulinzi na Usalama, Polisi, Usalama wa Taifa, Mahakama ya Rufaa,
Baraza la
Mitihani la Taifa ni mdogo mno au haupo kabisa.
b.
Uwakilishi mdogo wa Zanzibar katika balozi za Tanzania.
c.
Ushirikishwaji mdogo wa Zanzibar katika mahusiano ya kimataifa na
migao ya
misaada ambapo Zanzibar ama hugaiwa kidogo mno au kutopewa kabisa.
2
"Kosa moja ambalo linaendelea kufanywa ni lile la kudhani kwamba
kuimarisha Muungano kuna maana
moja na kuhaulisha shughuli zisizokuwa za Muungano ziwe za Muungano na
kwamba Chama na Serikali ya
Muungano wanaweza kufanya hivyo – bila ya kuzingatia Katiba wala hisia
au matakwa ya Zanzibar.
Dhana hizo ni ama ni za kupotosha kusudi kwa sababu wanazozielewa
wenyewe wafanyao hivyo, au ni
kukataa kuelewa Katiba. Vyovyote vile ilivyo ni mashaka.
Kisheria shughuli yoyote isiyo ya Muungano haiwezi kufanywa iwe ya
Muungano bila ya ridhaa ya Serikali ya
Zanzibar na Serikali ya Tanganyika au na Serikali ya Muungano kwa
niaba ya Tanzania Bara. Mpango wa
Serikali ya Muungano kuwakilisha pia Tanzania Bara umeleta fadhaa na
wasiwasi wa kutosha katika miaka
kadhaa, hasa ya hivi karibuni.
Hata kingekuwa Chama au Serikali ya Muungano vingeweza Kikatiba
kufanya hivyo, na haviwezi , basi
lingelikuwa ni kosa la uadilifu na pia la kisiasa kufanya hivyo, bila
ya ridhaa na makubaliano ya pande zote
mbili za Muungano, wala hicho kisingekuwa kitendo cha kuimarisha, bali
cha kudhoofisha na hata kupotosha
dhamiri na maana ya Muungano.
Najua baadhi wana mashaka na kimya changu na wangependa kujua msimamo
wangu juu ya suala hili la
masahihisho ya Katiba. Msimamo haunihusu kwa sasa, jambo la msingi ni
kwamba lazima Katiba
ziheshimiwe, maadili yafatwe na dhamiri ya Muungano ihifadhiwe.
Dhamiri lazima siku zote ibaki kuwa ni zao
la nidhamu ya hali ya juu kabisa.
Muungano au Umoja hauwezi kuimarishwa kwa upande mmoja kutwaa madaraka
ambayo ni ya pande mbili
za umoja huo. Ikiwa wote tutatekeleza wajibu wetu kwa dhati, haki
haitakuwa mbali kuonekana na kila
upande utakuwa na utaridhika na haki yake. Huko ndiko kuimarisha
Muungano". Malalamiko ya Rais wa Pili
wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe yaliyonukuliwa na Othman Masoud Othman
katika "Masuala yasiyo na
majibu katika Muungano". [Mada imetayarishwa na Kuwasilishwa Katika
Mkutano Maalum ulioandaliwa na
Zanzibar Law Society Kuadhimisha Miaka 41 ya Muungano. Hoteli ya
Bwawani Zanzibar tarehe 23.4.2005].
3"Inaonekana wazi pia, chanzo cha mvutano usiokwisha baina ya Zanzibar
na Tanzania Bara ambao
umeendelea kuwepo katika kipindi chote cha utawala wa Karume nchini
Zanzibar, na ambao sasa leo miaka
23 baada ya kutoweka kwake, umejitokeza tena juu na nguvu zaidi."
Abdurahman Babu, Utangulizi wa
Kitabu Uhasidi wa Marekani kwa Mapinduzi ya Zanzibar cha Amrit Wilson.
3
d. Ujenzi au uwekezaji wa taasisi zote za Muungano kujengwa au
kuwekezwa
Tanganyika ambapo fedha ya Muungano hutumika kwa kutengeneza kazi
wakati
Zanzibar hali ya maisha inazidi kuwa ngumu.
e. Sera zote za kifedha na kiuchumi zinatengenezwa kwa lengo la
kuihujumu
Zanzibar au kuifanya iwe tegemezi zaidi. Mfano mzuri Kampuni za Zantel
kutaka
kupanua shughuli zake Tanganyika, Bandari huru, mfumo wa kodi chini ya
TRA,
nk.
f. Kupangwa na kuamuliwa kwa siasa za Zanzibar huko Tanganyika kupitia
mfumo
wa siasa uliopo.
g. Uletwaji wa watu kiholela kwa lengo la kuharibu demografia za
Zanzibar bila ya
kuzingatia kuwa hivi ni visiwa ambavyo vinapaswa kulindwa kidemografia
na
kimazingira.
h. Utendaji unaoonyesha hisia za utofauti kwa pande mbili kama
wanavyofanya
Jeshi la Polisi kupiga watu kwa Zanzibar au kuweka watu ndani bila ya
sheria.
i. Kutoa maamuzi makubwa ya kisera na kisheria bila ya kuzingatiwa na
maslahi ya
Zanzibar kama mwenza (partner) wa Muungano na badala yake kufanywa
kama
mkoa au wilaya. Mfano mzuri na utendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa.
KWA NINI TUMEPENDEKEZA MUUNGANO WA AINA HII
7. Ni ukweli usiokatalika kuwa Zanzibar ni mkusanyiko wa visiwa vidogo
vinavyokaliwa
na watu wenye asili ya Zanzibar (mwambao wa Afrika Mashariki
wanaofuata dini ya
Kiislamu) wasiozidi 1,000,0004 kwa sasa ambayo imekuwemo katika
muungano pamoja na
nchi inayokaliwa na watu wanaokaribia 44,000,0005 wa makabila na mila
tofauti. Kwa
miaka 48 yote ya Muungano, Zanzibar imekuwa ni mwenza mwenye kupoteza
utamaduni
wake, dini yake, silka zake, uchumi wake, hadhi yake, historia yake na
demografia yake kwa
ujumla. Hali hii inaashiria siyo miaka 50 ijayo bali si zaidi ya 15,
Zanzibar itakuwa haipo
tena katika sura iliyonayo hivi sasa kidemografia na mbano wa
kiuchumi. Kwa lugha
4 Kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya 2012, Zanzibar inakisiwa kuwa na
wakaazi 1,303,568 ambapo katika
Sensa ya 2002 ilikuwa na watu 981,714. Kwa mujibu wa Settlement
Structure Plan 1993 – 2015, (Zanzibar
Revolutionary Government, Commission for Land and Enviroment, 1993)
Zanzibar ilitakiwa kuwa na idadi ya
watu 824,749 kufikia mwaka 2015. Inawezekana ni kwa sababu ya
kukosekana udhibiti wa uingiaji wa watu,
zaidi ya idadi hiyo imefikiwa miaka mitatu kabla!
5"Baada ya kusema maneno hayo sasa nipo tayari kuzindua rasmi matokeo
ya awali ya Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2012. Kwa heshima na unyeyekevu mkubwa natangaza kuwa
kwa mujibu wa Sensa ya
Watu na Makazi iliyofanyika kwa siku 14 kuanzia Agosti 26, 2012,
Tanzania ina watu 44,929,002 ambapo
Tanzania Bara kuna watu 43,625,434 na Zanzibar kuna watu 1,303,568.
Katika Sensa ya tatu ya mwaka 2002
tulikuwa milioni 34.4 hivyo tumeongezeka kwa watu milioni 10.5
ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 2.6
kwa mwaka. Naomba taarifa hizi zitumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa
ambayo ni kuboresha maisha ya
kila Mtanzania." (Hotuba ya Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa taarifa
za Sensa ya 2012 aliyoitoa tarehe 31
Dis, 2012 hapo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar-es-Salaam.http://
www.thehabari.com/habaritanzania/
uzinduzi-matokeo-ya-sensa-idadi-ya-watanzania-sasa-ni-44929002)
4
nyepesi ni kuwa muundo wa Muungano uliopo hauzingatii kwa namna yoyote
demografia
na utamaduni wa Zanzibar na unatumiwa kuihujumu Zanzibar kwa namna
ambayo baada
ya muda utaiondoa kwenye ramani ya dunia. Hatudhani kuwa lengo la
Muungano lilikuwa
ni kuifuta Zanzibar katika ramani ya dunia kiutamaduni na
kidemografia.
8. Sanjari na tatizo hilo, idadi ya watu wanaoishi Zanzibar kwa eneo
ni kubwa zaidi
kuliko sehemu yoyote katika Bara la Afrika kwa sasa. Kwa mujibu wa
takwimu za mwaka
1994, Zanzibar ilikuwa na watu 318 kwa kila kilomita mraba moja wakati
ikiwa na idadi ya
watu 742,000 (Settlement Structure Plan 1993 – 2015). Ikiwa idadi hiyo
kwa sasa
imeshakuwa mara mbili kulingana na Sensa ya 2012, Zanzibar kwa sasa
itakuwa na
takriban watu 600 kwa kila kilomita mraba moja ya kilomita mraba za
Zanzibar ambazo ni
2,648. Muelekeo ni bado kuletwa watu zaidi kutoka Bara kuja Zanzibar
kwa maisha ya
kawaida, kufanya kazi katika taasisi za Muungano na kwa kazi za
kusambaza dini.6 Udogo
wa Zanzibar au uhaba wake wa ardhi unalazimisha kuwepo kwa ulinzi
imara katika mfumo
wowote utakaokuwepo wa uingiaji wa watu kwa lengo la kuhifadhi ardhi
chache na
utamaduni wake. Hoja hii si ngeni kwani kuna nchi kadhaa ambazo zimo
katika miungano
lakini zimelazimika kukataa au kuchelewesha baadhi ya itifaki kwa
lengo la kulinda maslahi
yake. Mfano mzuri ni Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
ambamo haijaridhia
itifaki ya ardhi au Uingereza ambayo imekataa kutumia Euro katika
Umoja wa Ulaya.
a. MUUNDO WA MUUNGANO
UKUEM inapendekeza kuwepo kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
kwa upande
mmoja na Jamhuri ya Tanganyika kwa upande wa pili. Serikali mbili hizo
ziingie katika
mkataba wa muungano kwa maeneo ambayo yatakubaliwa na pande mbili
zilizo huru.
Mfumo unaopendekezwa ni ule wa Muungano wa Umoja wa Ulaya ambapo
mataifa yote
yanabakia huru na kuwa na uongozi wake kamili wa ndani (kama ni Rais/
Mfalme au Waziri
Mkuu, mabunge ya kila nchi na mahakama zao huru). Mambo mengine ya
kuzingatiwa
katika muungano huo wa mkataba ni:
(1) Muundo wa Serikali
Kuwepo na Serikali ambayo itasimamia na kushughulikia mambo ya
Tanganyika pekee
na pawepo na Serikali nyengine ya Zanzibar ambayo itasimamia masuala
ya Zanzibar
6 Angalia kumbukumbu za Kikao cha Mkutano Mkuu wa TANZANIA CHRISTIAN
FORUM (TCF) kilichofanyika
ukumbi wa mikutano cha TEC; Desemba 6, 2012. "Uangaliwe uwezekano wa
umoja wa TCF kwa kila taasisi
kujipanga na kupeleka huduma ya Injili huko Zanzibar kwa kutuma
wamisionari na kuwahudumia kwa ajili ya
kazi ya Bwana. Hii itarasimisha Muungano katika Kanisa sambamba na
Muungano wa Jamhuri." [Mkazo wetu
sisi].
5
Pekee. Sambamba na Serikali hizo pawepo na Tume au Kamisheni ya pamoja
ambayo
itaratibu matakwa na mkataba wa mashirikiano wa nchi mbili.
(2) Viongozi Wakuu wa Serikali (nchi ya Tanganyika na nchi ya
Zanzibar)
(a) Kiongozi mkuu wa Serikali ya Tanganyika atakuwa ni Rais ambaye
atajulikana
kuwa ni rais wa Tanganyika na pia atachaguliwa na wananchi wote wa
majimbo
ya Tanganyika.
(b) Kiongozi mkuu wa Serikali ya Zanzibar atakuwa ni Rais wa Zanzibar
ambaye
atachaguliwa na wananchi wote wa majimbo ya Zanzibar.
(c) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano itakayosimamia mambo
yanayohusu
Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika kwa pamoja ambaye
atakuwa
mmoja kati ya viongozi wakuu wa Serikali mbili hizo na mwenziwe
atakuwa ni
msaidizi wake ambapo watapishana kwa kipindi cha miaka mitano mitano.
(3) Kamisheni au Tume itakayosimamia maeneo yanayohusu Serikali mbili
Kuwepo na Tume itakayokuwa na makamishna wasiozidi 10 ambao
watashughulikia
mambo yanayohusu Serikali mbili. Mwenyekiti wa Kamisheni hii atakuwa
mmoja wa
viongozi wake wakuu (maraisi) ambao watapishana kwa vipindi na
patakuwepo na
uwiano wa watendaji baina ya Serikali hizo mbili. Tume hii itakuwa na
vyombo vya
utendaji kulingana na mahitaji ya kitaalamu ambavyo vinakuwa na
uwiyano wa
watendaji wake kwa wastani wa Watanganyika watatu kwa Wazanzibari
wawili. Hata
hivyo mambo yote ya kimaamuzi yatakuwa kwa uwiyano wa nusu-kwa-nusu.
(4) Maeneo ya mashirikiano
Mashirikiano kati ya nchi mbili yanayopendekezwa hapa chini yatatakiwa
kutawaliwa na
itifaki (protocol) kwa kila eneo la mashirikiano. Itifaki inayohusika
itaweka wazi haki,
fursa, mfumo wa utendaji, majukumu au wajibu wa kila mshirika,
taratibu za uchangiaji
wa gharama za uendeshaji na mambo mengine ambayo yatarahisisha
utendaji wa
mashirikiano hayo. Maeneo yanayopendekezwa ni:(
a) Hati au Mkataba wa Mashirikiano kati ya Jamhuri ya Tanganyika na
Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar.
(b) Tume au Kamisheni ya Mashirikiano
(c) Mambo ya nje (kinachokusudiwa hapa ni kila nchi kuwa na mamlaka
yake kamili
kama ilivyo katika mfumo wa Umoja wa Ulaya na itifaki zitachagua
maeneo ya
kuwa na msimamo wa aina moja).
6
(d) Ulinzi (kila nchi itakuwa na jeshi lake na patakuwepo na itifaki
ambayo itaeleza
maeneo ya mashirikiano. Ulinzi uliokusudiwa hapa ni ule wa mipaka na
mambo
yaliyobaki kuhusiana na usalama wa ndani yatabaki kwa Polisi ambao
watakuwa
chini ya mamlaka ya kila nchi).
(e) Hali ya hatari
(f) Utumishi katika maeneo ya mashirikiano
(g) Mahakama ya Rufaa kwa mambo yaliyoanzia katika mahakama za kawaida
(si
Mahakama ya Qadhi).
(h) Hali ya hewa.
(5) Ushiriki wa wananchi katika kupanua maeneo ya mashirikiano
Kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna suala lolote linaloingizwa katika
orodha ya
mashirikiano kinyemela, mkataba wa mashirikiano utaweka wazi maeneo ya
msingi ya
mashirikiano na maeneo yatakayobaki hayataongezwa katika eneo hilo
isipokuwa kwa
kibali cha wananchi kwa kupitia kura ya maoni ambayo itaungwa mkono na
theluthi
mbili ya wananchi wenye haki ya kupiga kura kwa kila upande. Suala
hili la
ushirikishwaji wa wananchi katika kuamua masuala ya mashirikiano,
litazingatiwa na
kufanyiwa kazi hata wakati itakapotokea kutaka kupunguzwa kwa jambo
lolote liliomo
katika orodha ya mambo ya masharikiano. Utaratibu wa kupunguzwa kwa
orodha
utatofautiana na ule wa kuongezwa. Wananchi wa upande mmoja iwapo
watapiga
kura ya maoni na theluthi mbili za wapiga kura hao wakiamua kupunguza
jambo,
Serikali zote mbili zitafungika na maamuzi hayo na jambo hilo
litafutwa katika orodha.
(6) Vikao vya mashirikiano kutofautiana na vikao vya kila nchi
Taasisi zitakazoanzishwa kwa ajili ya kusimamia mashirikiano ya nchi
mbili zieleweke
wazi, majukumu yake yafahamike kimkataba na mfumo wake wa utendaji
usichanganywe na taasisi za kila nchi. Vikao vyote vya mashirikiano
vitaendeshwa kwa
misingi ya nchi mbili zilizo sawa bila ya kujali ukubwa wa nchi au
idadi ya wananchi wa
nchi hiyo.
(7) Ujenzi wa taasisi za mashirikiano
Taasisi zote za mashirikiano zitakuwa na ofisi zake katika sehemu zote
mbili kwa
uwiyano unaokubalika ambapo iwapo makao makuu yatakuwepo upande mmoja,
jitihada zitafanywa kujengwa kwa ofisi kuu katika sehemu ya pili.
Taasisi hizi
zitatengewa watumishi kwa uwiyano kutoka pande zote mbili kulingana na
mahitaji ya
taasisi hizo.
b. KATIBA ITAMBUE KUWEPO KWA MWENYEZI MUNGU
7
Katiba iseme wazi kuwa Tanganyika ni nchi inayotambua kuwepo kwa
Mwenyezi Mungu
na wananchi wake wana dini zao ambazo Serikali na vyombo vyake
vinawajibika
kuziheshimu na sheria au vitendo vyovyote vile vinavyolenga kuipa
upendeleo dini moja
dhidi ya nyengine au kuteua watu wa dini moja katika taasisi zake
vitakuwa ni kosa la jinai
na kiutumishi. Wananchi watakuwa na haki ya kufungua madai katika
Mahakama kuu
iwapo watahisi pana dalili au mambo ambayo yanavunja jambo lolote
kuhusiana na suala
la imani ya Mwenyezi Mungu au dini. Sheria zote ambazo zinalenga
kutambua ukubwa wa
dini moja kuliko nyengine ziwe ni batili kama ile ambayo ilimtia
hatiani Muislamu kwa
sababu alisema Yesu si Mungu katika kesi mashuhuri ya Jamhuri dhidi ya
Dibagula7.
c. NCHI ZINAZOUNDA MUUNGANO WA MKATABA
Ni muhimu sana kufahamika kwa kizazi kilichopo na kitakachokuja
baadaye kuwa kabla ya
Muungano wa tarehe 26 Aprili, 1964, Zanzibar ilikuwa ni nchi huru na
ikijulikana kama
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Tanganyika ilikuwa hivyo hivyo na
ilijulikana kama
Jamhuri ya Tanganyika. Ukweli huu ni lazima uwekwe bayana ndani ya
Mkataba wa
masharikiano wa nchi mbili (au Katiba mpya).
d. MAHAKAMA YA KADHI KWA UPANDE WA TANGANYIKA
Suala la kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi kwa upande wa Tanganyika lina
umuhimu wa
pekee katika kuonyesha katiba inayojali matashi ya wananchi wake.
Mahakama za Kadhi
zimekuwepo karibu sehemu yote ya Afrika ya Mashariki kabla ya
kupatikana kwa uhuru.
Serikali ya Tanganyika huru kufuatia sababu zisizowekwa wazi na
watawala wa wakati ule
waliamua bila ya hoja madhubuti kufuta Mahakama hiyo kwa kile
kinachoonekana kuwa ni
kukubaliana na maagizo ya viongozi wa kanisa8. Katika katiba ijayo
inapendekezwa
kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi ambayo itakuwa kama taasisi ya Serikali
inayofahamika
rasmi katika taasisi ya umma chini ya tawi la mahakama la dola.
7
Criminal case No. 197 of 2000- Republic vs Hamisi Rajabu Dibagula.
8
"Kwa namna nyingi St. Mary's na St. Francis ya Pugu zilichangia
uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa Katoliki
na wale wa Serikali. Kwanza vyombo hivi vya Kanisa vilitoa elimu
iliyowasaidia hao wahitimu kufikia ngazi hizi
za uongozi. Pili, urafiki kati ya walimu wa St. Mary's na St. Francis
pamoja na urafiki kati yao na wanafunzi wa
vyuo hivi viwili ullchangia mshikamano wa viongozi Serikalini. Tatu,
mawazo na fikra za watu hao juu ya
ujamaa yalielekezwa na elimu yao ya Kikatoliki. Muhimu zaidi ni kwamba
shughuli za mazingira katika shule
za bweni zimewezesha hadi sasa kukua kwa uhusiano kati ya viongozi wa
Kanisa na wa Serikali na Chama.
Hali hii imefanya matendo, msimamo na uamuzi wa viongozi wa Serikali
ufanane mara kwa mara kwa
namna moja au nyengine na mafundisho na mwenendo wa Kanisa." Dr. John
C. Sivalon, Kanisa Katoliki na
Siasa ya Tanzania Bara 1953 hadi 1985, uk. 16. Angalia pia Hamza Njozi
katika Muslims and the State in
Tanzania, 2003, uk 19 "They reorganized themselves under the East
African Muslim Welfare Society
(EAMWS). Westerlund (1980) said that it would probably never be known
why Nyerere decided to ban that
Muslim organization. Sivalon (1992) has revealed that it was actually
the church leaders who had requested
Nyerere to ban that Muslim body, which he did."
8
Mfumo unaopendekezwa ni sawa na ule wa Zanzibar (Katiba ya Zanzibar ya
1984) au
Katiba Mpya ya Kenya ya 2010. Katiba hizi zinatambua kuwepo kwa
Mahakama Kuu ya
Kadhi pamoja na Mahakama za chini ambazo zinawahudumia wananchi
wanaofuata imani
ya Uislamu. Aidha Mahakama hizi zinatakiwa ziendeshwe kwa fedha ya
Serikali kutoka
Mfuko Mkuu wa Serikali na siyo kama "faith-based NGO" chini ya BAKWATA
au taasisi
nyengine binafsi au Waislamu kwa pamoja.
e. ADHABU YA KIFO
Katiba inayokuja ni lazima ioneshe utukufu ya uhai wa maisha ya
mwanadamu na viumbe
vyengine. Maisha ya binadamu ni lazima yalindwe kwa hali zote na
yasitolewe isipokuwa
kwa mujibu wa sheria ambayo itataja wazi kuwa "kuua nafsi kwa
kukusudia". Mtu yeyote
ambaye ataua nafsi kwa makusudi huyo ni lazima naye auliwe kwa lengo
la kuhifadhi
maisha ya watu wengine. Hakuna nchi yoyote duniani iliyoondosha adhabu
ya kifo kisha
ikifanikiwa na ikaepuka kutumbukia katika wimbi la mauaji ya raia wake
mara kwa mara.
Kampeni iliyopo ya kupingwa adhabu ya kifo na wale wanaojiita watetezi
wa haki za
binadamu ambao wanalenga kumtetea muuaji na kumdharua binadamu
aliyeuliwa kwa
jina kuwa adhabu hiyo yaitekelezeji nchini kwetu, tunadhani si sahihi.
Marais kushindwa
kuwajibika binafsi siyo udhaifu wa sheria. Kwa kuepusha tatizo la
marais kuidhinisha
adhabu ya kifo, mahakama ziwe na uwezo kwa adhabu ya kifo sawa na
adhabu nyengine.
Hukumu ya mahakama iwajibishwe kutekelezwa na vyombo vya dola (Chuo
cha
Mafunzo/Magereza) moja kwa moja kama ilivyo kwa adhabu za kifungo na
faini na sharti
ya kupata idhini au ridhaa ya rais ifutwe moja kwa moja.
Kinachoonekana hapa ni marais
kuwa dhaifu wao na siyo adhabu hivyo mahakama itakapompata muuaji na
hatia ya
mauaji na kumuhukumu kifo, hukumu hiyo itoshe na itekelezwe baada ya
muda fulani.
Rais anaweza kupewa uwezo wa kuidhinisha katika kipindi cha miezi
mitatu hadi sita; na
kama atashindwa, hukumu hiyo iwe itoshelezwa kwa kule kutamkwa na
mahakama na
watekelezaji wa sheria wawajibike kutekeleza baada ya muda wa rais
kupita.
f. UMOJA WA KITAIFA KWA KUEPUKA MAMBO YANAYOASHIRIA UDINI
Kwa lengo la kuondosha hisia za upendeleo uliorithiwa tokea wakati wa
ukoloni (kama
kupumzika siku ya Jumapili ili kutoa nafasi ya Wakristo kwenda
makanisani, Jumamosi
iliyokuja baadaye kwa ajili ya Wasabato) pana haja kwa Katiba ya
Tanganyika kupiga
marufuku ya matumizi ya siku kama hizo kwa mapumziko na badala yake
zitafutwe siku
zisizonasibishwa na dini kuwa ni siku za mapumziko. Vyenginevyo,
mapumziko yawe
Ijumaa na Jumamosi (ambapo Waislamu watapata moja na Wakristo watapata
moja).
Madai kuwa mapumziko ya Jumamosi na Jumapili ni jambo la kimataifa si
sahihi kwani
suala hilo asili yake ni nchi za Magharibi ambazo ndizo zilizoanzisha
mfumo wa ukoloni
katika karne ya 19 na 20. Mojawapo na mambo yaliyokuwepo katika
Makubaliano ya Berlin
9
lilikuwa ni kuingiza silka na utamaduni ya nchi za Ulaya katika
makoloni yao (civilization) na
kutoa nafasi maalumu kwa wamisionari na shughuli zao.9 Kwa kuwa asili
ya sikukuu hizi ni
wao na inafahamika kuwa lilikuwa na bado lingali kosa kufanya kazi
siku za Jumapili10
katika baadhi ya nchi hizi (zikiwemo za Ulaya na majimbo ya Serikali
za Marekani) kwa
sababu ya kuhamasisha ibada, uingizwaji wa siku hizi kama siku za
mapumziko
unafungamana moja kwa moja na dini ya Kikristo.
Sambamba na hili, mahusiano ya dola na taasisi za kidini uwe wa pande
zote mbili.
Mahusiano ya Serikali na Ubalozi wa Vatikano ni lazima yapigwe
marufuku au
vyenginevyo, Serikali ya Tanganyika ikubali ombi la Waislamu la
kujiunga na Umoja wa
Jumaiya ya Nchi za Kiislamu (Islamic Organization Conference).
Pamekuwepo na madai
9 They will protect and favour, without distinction of nationality or
of religion, the religious, scientific or
charitable institutions and undertakings created and organized by the
nationals of the other Signatory
Powers and of States, Members of the League of Nations, which may
adhere to the present
Convention, which aim at leading the natives in the path of progress
and civilisation. Scientific missions, their
property and their collections, shall likewise be the objects of
special solicitude.
Freedom of conscience and the free exercise of all forms of religion
are expressly guaranteed to all nationals
of the Signatory Powers and to those under the jurisdiction of States,
Members of the League of Nations,
which may become parties to the present Convention. Similarly,
missionaries shall have the right to enter
into, and to travel and reside in, African territory with a view to
prosecuting their calling. (ARTICLE 11 of
Convention Revising the General Act of Berlin, February 26,1885, and
the General Act and Declaration of
Brussels, July 2,1890 [Zinapotajwa dini katika waraka huu imekusudiwa
dini ya Kikristo kwani ndiyo iliyokuwa
dini ya mataifa yanayohusika na Mkataba huu kama inavyoelezwa hapo "to
all nationals of the Signatory
Powers". Inawezekana ni Ukatoliki, Morovians, Lutherans, Anglicans
nk.] Imenukuliwa kutoka kwenye
mtandao http://wysinger.homestead.com/berlin-conference-doc.html.
10 Wakielezea neno "Sunday", asili na historia yake, katika mtandao wa
Catholic Encyclopedia kuna maelezo
yafuatayo: "The obligation of rest from work on Sunday remained
somewhat indefinite for several centuries.
A Council of Laodicea, held toward the end of the fourth century, was
content to prescribe that on the Lord's
Day the faithful were to abstain from work as far as possible. At the
beginning of the sixth century St.
Caesarius, as we have seen, and others showed an inclination to apply
the law of the Jewish Sabbath to the
observance of the Christian Sunday. The Council held at Orléans in 538
reprobated this tendency as
Jewish and non-Christian. From the eight century the law began to be
formulated as it exists at the present
day, and the local councils forbade servile work, public buying and
selling, pleading in the law courts, and
the public and solemn taking of oaths. There is a large body of civil
legislation on the Sunday rest side by
side with the ecclesiastical. It begins with an Edict of Constantine,
the first Christian emperor, who
forbade judges to sit and townspeople to work on Sunday. He made an
exception in favour of agriculture.
The breaking of the law of Sunday rest was punished by the Anglo-Saxon
legislation in England like other
crimes and misdemeanours. After the Reformation, under Puritan
influence, many laws were passed
in England whose effect is still visible in the stringency of the
English Sabbath. Still more is this the case
in Scotland. There is no federal legislation in the United States on
the observance of the Sunday, but nearly
all the states of the Union have statutes tending to repress
unnecessary labour and to restrain the liquor
traffic. In other respects the legislation of the different states on
this matter exhibits considerable variety. On
the continent of Europe in recent years there have been several laws
passed in direction of enforcing the
observance of Sunday rest for the benefit of workmen." [Imenukuliwa
kutoka kwenye mtandao wa Catholic
Encyclopedia kwa jina la http://www.newadvent.org/cathen/14335a.htm%5D.
Angalia maelezo yanayolingana na
hayo katika mtandao wa http://en.wikipedia.org/wiki/Sunday
10
kuwa Ubalozi wa Vatikano ni sawa na kuwepo kwa balozi nyengine zozote
wakati OIC ni
taasisi ya kidini ambayo ina azma ya kupambana na dini ya Kikristo
kulingana na katiba
yake. Hakuna asiyefahamu kwamba Vatikano ni dola ndogo11 iliyozungukwa
na nchi ya
Italia (ndani ya Rome) ambayo inaongozwa na Papa na ina raia na
wafanyakazi ambao
wote kwa sasa ni wanaume. Malengo makuu ya Vatikano ni kusimamia na
kueneza
mafunzo ya dini ya Kikristo kulingana na imani ya Ukatoliki. Mabalozi
wote wanaoiwakilisha
Vatikano katika nchi huwa wana mahusiano ya moja kwa moja na uongozi
wa Kanisa
katoliki katika nchi wanazomuwakilisha Papa na wanawajibika kwake
kidini na kisiasa.12
Tanzania kuwa na mahusiano na nchi ambayo imeanzishwa kwa maslahi ya
dini moja
kunailazimisha kukubaliana na yale yanayotakiwa na Waislamu ya
kujiunga na OIC kama
zilivyofanya nchi kama Gabon (1974), Uganda (1974) na Mozambique
(1994) ambazo
zinawezekana kuwa raia wake ni sawa na walivyo wa Tanzania au kuwepo
kwa Wakristo
wengi zaidi 13.
Jambo jengine lenye kulingana na hili ni kuwepo kwa MoU kati ya
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Makanisa ambapo Serikali imekubali kutoa
upendeleo
maalumu kwa makanisa katika kutenga nafasi za masomo katika vyuo vyake
pamoja na
kufanya mgao wa fedha ya umma inayochangiwa na walipa kodi wa dini
zote. Katiba
iagize rasmi kuwa hapana mazingira yoyote ambayo Serikali itatoa
upendeleo wa aina hii
kwa dini moja bila ya kuhusishwa kwa dini nyengine. Katiba iagizwe
kutungwa sheria ya
kuwafidia wale wote ambao wamenyimwa fursa hiyo kinyume na maagizo ya
Katiba
iliyopo ambayo inapiga maarufu upendeleo wa kidini.
Mfumo wa kisekula uliopo (wa kumkataa Mungu) ni lazima ufahamike kuwa
umelengwa
zaidi kuuhujumu Uislamu kuliko dini nyengine yoyote. Dini nyingi
hazina mafunzo ya kina
11
Vatican City is the smallest independent state in the world in terms
of inhabitants and size. It occupies an
area of 44 hectares. The borders are represented by its walls and the
travertine pavement curve that joins
the two wings of the colonnades in St Peter's Square. Beyond the
proper territory of the State, Vatican
jurisdiction also covers some extraterritorial areas within and
outside Rome. Imenukuliwa kutoka
http://www.vaticanstate.va/EN/State_and_Government/
12 Ambassadors are officially accredited not to the Vatican City State
but to "the Holy See", and papal
representatives to states and international organizations are
recognized as representing the Holy See, not
the Vatican City State. Though all episcopal sees may be considered
"holy", the expression "the Holy See"
(without further specification) is normally used in international
relations (and in the canon law of the Roman
Catholic Church)[3] to refer to the See of Rome viewed as the central
government of the Roman Catholic
Church. (Imenukuliwa kutoka http://en.wikipedia.org/wiki/Holy_See
13 Mozambique kwa mujibu wa mtandao wa CIA ina Waislamu asilimia 17.9
tu kwa mujibu wa sensa ya 1997
wakati Uganda ina Waislamu asilimia 12.1 kwa mujibu wa sensa ya 2002.
(Angalia mtandao wa Shirika la
Kijasusi la Marekani (CIA) linavyoeleza https://www.cia.gov/library/publications/the-worldfactbook/
geos/mz.html na https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/ug.html).
11
kuhusiana na mavazi, maingiliano ya jinsia mbili na hata mfumo wa
ibada za kila siku.
Kutokana na kuwa Uislamu unamuhitaji Muislamu kutekeleza hayo kwa
masaa yote ya
maisha yake, Katiba ilazimishe sheria zote zitakazotungwa kuheshimu
mavazi ya waumini
wa dini zote na pasiwepo na vipingamizi vyovyote kwa watendaji wa
Serikali kujaribu
kuhujumu suala hilo. Sambamba na suala la mavazi Katiba iagize sheria
nyengine kutoa
fursa kwa Waislamu kutekeleza ibada zao kwa siku ya Ijumaa kwa muda
utakaowekwa na
pasiwepo na mtendaji ambaye atajaribu kufanya jambo la kuhujumu muda
hao kama vile
mitihani katika maskuli/vyuo au mikutano ya lazima na mambo ya aina
hiyo.
g. TUME ZA UCHAGUZI
Tume ya uchaguzi iundwe kwa utaratibu wa kuchaguliwa watu wenye sifa
za kitaaluma na
uzoefu kwa njia ya kuomba kazi kwenye Kamisheni ya Utumishi wa Umma na
maombi
hayo yatazingatiwa na Tume hiyo na wale wenye sifa kwa shughuli
tofauti za Tume
watachaguliwa. Kamisheni ya kazi yenyewe nayo iwe ni chombo
kinachoaminika na chenye
watu wenye sifa zinazostahili. Uteuzi wa Mwenyekiti, Wajumbe na Katibu
wa Tume ya
Uchaguzi ufanyike kwa njia za wazi ambapo sifa na vigezo vitaelezwa
hadharani kwa nini
ameteuliwa mmoja na kuachwa mwengine. Uteuzi wa wajumbe wa Tume ni
lazima
uzingatie jiografia ya nchi, dini na jinsia. Mfumo wa sasa wa Rais
kuteua wajumbe wa Tume
hiyo ufutwe. Tume nayo itakuwa ikiajiri watendaji wake kila
panapotokea haja ya uchaguzi
na isihusishe kabisa watendaji wa serikali katika shughuli zake kama
inavyofanyika sasa kwa
maafisa tawala kuwa maafisa uchaguzi wa wilaya.
h. KINGA YA RAIS KUTOSHITAKIWA
Kinga ya Rais kutoshitakiwa haina haja kuendelea kwa makosa ya jinai
au kiutumishi
atakayoyafanya akiwa madarakani. Kinachopaswa kufanyika ni kuwepo
chombo
madhubuti na kinachoheshimika ambacho kitapokea madai ya watu binafsi
kwa makosa ya
jinai au madai na kuyachunguza makosa hayo. Pale itakapobainika kuwa
pana kosa la
kujibu basi kosa hilo lipelekwe katika mahakama na kusikilizwa kama
madai mengine.
Chombo kinachopendekezwa hapa ambacho kinaweza kupewa nafasi ya
uchunguzi wa
madai ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kwa makosa yote ya jinai na
madai. Mfumo
unaopendekezwa hapa ni sawa na ule wa Israili ambapo hata Waziri Mkuu
anaweza
kuchunguzwa na Muendesha Mashitaka na akibainika kuwa ana shitaka la
kujibu
anapandishwa mahakamani.
Baraza la Wawakilishi au Bunge linapendekezwa kuachiwa na uwezo wake
wa sasa wa
kumshitaki Rais kwa makosa ya kiutawala (utumishi) pale litakapohisi
kuwa Rais amevunja
sheria yoyote ya kiutawala kama mtendaji mwengine yoyote wa Serikali.
12
i. MAWAZIRI KUTOKUWA WAWAKILISHI AU WABUNGE
Kwa lengo la kutoa nafasi nzuri ya utumishi Serikalini, wawakilishi au
wabunge wote
wasiruhusiwe kuwa mawaziri na wala manaibu waziri. Rais awe na uwezo
wa kuteua watu
nje ya BLW/Bunge kuteua watu ambao atawahisi wanafaa kushika nafasi za
uwaziri na
unaibu waziri kwa kuzingatia uwezo wao wa kitaaluma, uzoefu, jiografia
ya nchi, dini na
jinsia. Watumishi hawa wote waidhinishwe na BLW/Bunge kabla ya
kuchukua nafasi hizo
na kula kiapo cha uaminifu na kutunza siri. Rais atakuwa na uwezo wa
kuwaondosha
wakati wowote akihisi pana haja ya kufanya hivyo na BLW/Bunge litakuwa
na uwezo wa
kumtaka Rais kuwawajibisha watendaji hao kwa utendaji mbovu au makosa
mengine ya
kiutumishi kupitia azimio maalumu. Mawaziri hawa na Manaibu wao
watakuwa wajumbe
wa BLW au wabunge wakati wakiwa wanahudumu kama mawaziri au manaibu
waziri tu.
Wakiachishwa kazi na Rais au kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na BLW/
Bunge; itakuwa
wamefukuzwa kazi moja kwa moja (Serikalini na BLW/Bungeni). Azimio la
kutokuwa na
imani na mtendaji yoyote wa Rais linaweza kufanya kazi iwapo litaungwa
mkono na nusu
ya wajumbe wa kikao halali cha BLW/Bunge.
j. UTEUZI WA WATENDAJI KATIKA SERIKALI
Uteuzi wa watendaji wote wa ngazi za juu za Serikali – kuanzia Wakuu
wa Mikoa, Wilaya,
Wakurugenzi, Watendaji wakuu wa mashirika ya umma na idara za Serikali
wateuliwe na
Rais na waanze kazi baada ya kuidhinishwa na Kamati Maalumu ya BLW/
Bunge.
Wawajibishwe na Rais pale watakaposhindwa kutekeleza majukumu
yaliyopangwa au
kuainishwa katika nyaraka zao za ajira kwa kila mwaka. Viashiria ya
mafanikio yao viwe ni
utendaji wao na utekelezaji wa yale watakayokabidhiwa wakati wa
kushika dhamana hizo.
Vigezo vya kisiasa, urafiki, unyumbani na vinavyolingana na hivyo viwe
ni mwiko kwa
uhalisia na siyo kwa maandishi kama ilivyo sasa.
k. WAWAKILISHI/WABUNGE KUWAJIBIKA KWA WANANCHI KABLA YA MUDA WA UHAI
WA BARAZA/BUNGE
Uzoefu umeonyesha kuwa wawakilishi/wabunge wamekuwa wakiwadanganya
wananchi
kwa ahadi mbali mbali ili kupata kura. Viongozi hao mara baada ya
kuchaguliwa huhama
majimboni mwao na kuwasahau wananchi hadi baada ya miaka mitano ambapo
hufika
hapo na kwa njia za hadaa na rushwa hufanikiwa kupata nafasi hiyo
kimaajabu. Katiba itoe
uwezo kwa wananchi ambao watafikia idadi fulani kuitishwa kura ya kuwa
na imani na
muhusika katika kipindi cha katikati iwapo watahisi kuwa mbunge huyo
hana manufaa
kwao. Iwapo zitapatikana sahihi hizo Tume ya Uchaguzi inaweza
kusimamia kuitishwa kwa
kura ya maoni ya wananchi dhidi ya mwakilishi/mbunge huyo na kama
atashindwa kwa
zaidi ya nusu atalazimika kujiuzulu na uchaguzi mpya kuitishwa katika
jimbo hilo.
13
Inawezekana kuonekana jambo hili kuwa litakuwa ni mzigo kwa Serikali.
Hilo ni kweli lakini
ni katika gharama za kawaida za demokrasia. Kutowakilishwa wananchi ni
gharama kubwa
zaidi kuliko kutumia fedha kuwapatia wananchi mwakilishi/mbunge ambaye
ataweza
kuwawakilisha na kulisaidia taifa kwa kuisimamia vizuri Serikali.
l. KATIBA KUJALI UTAMADUNI NA MAADILI YA WANANCHI
Katiba itakayoandikwa inapaswa kuheshimu mila, silka na utamaduni wa
wananchi na siyo
kuingiza vipengee ambavyo vitakuwa vinajenga mazingira ya kuimarisha
na kupalilia mila
na utamaduni wa nchi za Magharibi. Uhuru wa wanaume kusuka nywele au
kuvaa herini
na wanawake kuvaa kama wanaume au nguo zinazoudhalilisha ujanajike;
huu si
utamaduni ambao unapaswa kupaliliwa au kujengewa mazingira ya
kuimarika. Katiba
ambayo itaruhusu uhuru wa ndoa za jinsia moja na watu kuzini kwa jina
la uhuru wa
kutenda baada ya kufikia utu-uzima au kuridhiana mtu na mke au mume wa
mtu
haupaswi kuwekwa wala kupewa nafasi katika katiba ijayo.
Katiba iseme wazi na bila ya kimeme kuwa mambo hayo hayatakuwa na
nafasi katika jamii
ijayo itakavyoongozwa na katiba hiyo. Matendo yote ambayo kiwazi
yanapingana na mila
na utamaduni wetu hayo yatakuwa ni makosa na sheria ziagizwe kuyawekea
adhabu kali.
(Talib Juma Ali)
AMIR
UMOJA WA KIISLAMU WA ELIMU, UCHUMI NA MAENDELEO
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments