[wanabidii] KATIKA HILI MWANABIDII MWENZETU H.KIGWA UMECHEMSHA

Tuesday, February 05, 2013
Ndugu yetu na mwenzetu Dr.H.Kigwangala jana nimekusikia bungeni
ukimuita mbunge mwenziyo Tundu Lissu mgonjwa wa akili na kwamba
aliwahi kuwa mteja wako katika kazi zako za udaktari. Na kwamba kwa
vile ni siri yako na mgonjwa huwezi kusema kila kitu. Mbona
umekwishaweka hadharani hiyo siri? Nijuavyo mimi wagonjwa wa akili
ambao hawajapona wanabaki hospitalini chini ya uangalizi wa madaktari.
Ina maana huyo Lissu katoroka au ni mazingira gani yametumika
kumruhusu ajichanganye na watu wenye akili kama wewe huko bungeni?

Sikuamini nilichokisikia toka mdomoni mwa kijana anayejinadi kugombea
nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM. Sikatai inawezekana Tundu Lissu
aliwahi kuwa mgonjwa wa akili lakini mazingira uliyoyatumia kutuelezea
ugonjwa wake hayaonyeshi kama kuna chembe ya ukweli. Kigwangala
unasema Tundu Lissu ni mgonjwa hadi leo kwa maana nyingine ulivyomtibu
hakupona, ukiwa daktari mwenye ujuzi na maadili sahihi kwa nini
hujamwambia spika zikafanyika taratibu akarudishwa hospitali atibiwe?
Kumbe pia ndiyo maana uliukimbia udaktari kwa vile wewe ni daktari
asiyekuwa mahiri, unaowatibu hawaponi na wala huchukui hatua zozote
kuwasaidia kutibiwa.

Kigwangalla kumbuka kabla ya hilo skendo la jana umewahi kushikiana
bunduki na Bashe. Tunajua fika kwamba amani na utulivu kwa mkoa wenu
wa Tabora ni tatizo na kwamba kukaa na bunduki ni sehemu ya maisha ya
kila siku kama tulivyomuona Ragge akipanda jukwaani akiwa nayo kiunoni
huko Igunga. Kuna haja ya kuzifanya wilaya zote za Tabora kuwa mikoa
ya kipolisi ili kurudisha amani na utulivu. Sijui kwa nini HK hujatoa
hoja kama hizi bungeni ili wanatabora wote wakapewe ulinzi na
serikali.

Kwa tunaofuatilia vizuri hoja za Tundu Lissu hakuna kitu cha kutufanya
tuamini kwamba Tundu Lissu ni mgonjwa wa akili labda tunachobaki
tukijiuliza ni je kweli huyu Kigwangala ni daktari kweli wa kusomea au
ndo wale madaktari wababaishaji na pengine ndiyo maana alikimbilia
siasa baada ya kugundulika kuwa ni kanjanja. Hivi kati ya Lissu na
Kigwangalla mgonjwa wa akili ni nani?

Nikiwa mwanabidii mwenzio nakushauri ujenge utamaduni wa kujibu hoja
unazoulizwa kwa ufasaha bila kutokwa na maneno yasiyokuwa na staha
kama mgonjwa wa cerebral malaria. Kwa mwendo huu sijui kama
utafanikiwa kujenga umaarufu unaoutafuta badala yake unaharibu kila
sifa tuliyofikiri unayo.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments